Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa,akiongea na waandishi wa habari kuhusu kununua bidhaa mbalimbali katika duka la shoppers Plaza kupitia huduma ya M pesa.
Sasa M-Pesa imewarahisishia wateja wanaofanya manunuzi katika duka la Shoppers Plaza(Supermarket)ya Msasani na Masaki jijini Dar es Salaam. Vilevile utapata Tsh 1000 kama muda wa maongezi bure mara baada ya kufanya manunuzi kupitia huduma ya M pesa.
Ili kuweza kulipia manunuzi dukani hapo ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya:
Kwanza chagua bidhaa unayotaka kununua,na Muuzaji katika kaunta ya malipo atakutaarifu jumla ya bei unayotakiwa kulipia. Hatua inayofuata ni kubonyeza *150*00# kwenye simu yako ili uweze kupata Menu ya M-Pesa halafu fuata hatua zifuatazo.
Bonyeza 5 kuchagua Nunua Bidhaa
· Bonyeza 1 kama unafanya manunuzi Shoppers ya Msasani au bonyeza 2 kama ni Shoppers ya Masaki
· Ingiza namba ya tili ambayo ni aidha 660660 kama ni Shoppers Msasani au ingiza 607060 kama ni Shoppers Masaki
· Weka kiasi
· Weka namba ya siri
· Bonyeza 1 kuthibitisha au 2 kubatilisha
Baada ya manunuzi kufanyika, utapata ujumbe mfupi au SMS kukujulisha malipo yameshafanyika. Muuzaji atapata ujumbe wa manunuzi kwenye komputa yake na atakupatia risiti kama kithibitisho cha manunuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...