ZAIDI YA ABIRIA 40 WALIOKUWEMO KWENYE BASI LA NEW FORCE WAMEPONA KUFA BAADA YA  BASI HILO KUGONGANA NA LORI LA MIZIGO AINA YA FUSO MAENEO YA PIPE LINE INYALA ,JIJINI MBEYA MAPEMA LEO ASUBUHI. BASI LA NEW FORCE LILIKUWA LINATOKEA MBEYA KUELEKEA DAR ES SALAAM. 



Hili roli aina ya fuso ndilo lililosababisha ajali hiyo kwani lilikuwa lilikuwalinalipita gari lingine bila ya kuangalia kama gari nyingine inashuka mlima na ndipo lilipokutana na basi hilo
Hii ndiyo hali halisi ya ajali hiyo dreva wa fuso kakimbia baada ya kusababisha ajali hiyo
Mtoto Samwel akisimulia jinsi ajali hiyo ilivyotokea kwani yeye alikuwa nyuma ya dereva  amesema yeye mkanda ndiyo uliomuokoa kwani mama aliyekuwa jirani yake hakufunga mkanda ameumia vibaya sana 
Badhi ya abilia waliokuwa kwenye basi hilo wakisubiri usafiri mwingine toka katika kampuni ya new force

Baadhi ya majeruhi hao wameruhusiwa baada ya kupata matibabu
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufani ya Mbeya, Dk. Hamfrey Kiwelu, aliyesimama amesema wamepokea majeruhi 24 na kati ya hao 17 wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na majeruhi 7 wamelazwa hospitalini hapo kuendelea na matibabu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duh. Poleni Swali la Kizushi. Cjawahi skia baada ya ajali hizi kampuni flani ya Insurance imewajibika walao kutibia majeruhi Je ni kweli gari nyingi kati ya mabasi tunayosafiria hayana Insurance covers kwa abiria!? Polisi kila wakikagua gari wanaangaliaga sika ya bima! Je hizi stika ni genuine ama fake!! Mi cjui!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...