Mkuu wa benki kuu ya Zambia ndugu
Mizinga Melu amesema benki kuu ya Zambia
(BoZ) imeandaa (workshop) ambayo itailezea kwa ufasaha benki inayofuta sheria
za kiislam. Benki kuu ya Zambia ikiwa kama msimamizi mkuu itasimamia matayarisho
hayo wakati timu ya wakaguzi (regulator) itakapokua tayari. ‘Wakati wowote
unapoleta huduma mpya, ni muhimu kua sote tunazungumzia kitu ambacho
tunafahamiana na tuanaweka malengo alisema mr Melu.
BoZ imenukuliwa ikisema ‘huduma
za benki zinazaofuta sheria ya kiIslam zitawasaidia watu kupata mikopo isiyokua
na riba kwa ajili ya kuzalisha mitaji yao’ na wakati huohuo inatoa changamoto
kwa wajasirimali ambao wako tayari kuanzisha benki hizo nchini Zambaia.
Uchunguzi wa karibuni uliofanywa
na benki kuu ya Zambia umeonyesha kwamba asilimia 80 ya mawasiliano
yaliyofanywa yalionekana kuunga mkono huduma hizo na kuzikaribisha. Benki
nyingi za biashara zinategemea kuanzisha huduma hiyo ikiwemo Standard Charted
Bank na kuna soko kubwa la huduma hizo nchini Zambia na Africa kwa ujumla.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na
benki zinazofuata sheria za kiislam wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com
Benki za Kiislam ni nzuri kwa wafanyabiashara.
ReplyDelete