Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo diwani wa kata ya
Kipawa, Bonnah Kaluwa, alisema lengo la mradi huo ni kuboresha Mazingira
ya elimu ya Msingi na Sekondari kwenye kata yake.
Aidha
Kaluwa alifafanua kuwa Uboreshaji huo wa mazingira ya Elimu unafanyika
kwenye Shule saba za Msingi na Sekondary za kata hiyo kwa kuwapatia
madawati, maji safi na salama, kujenga vyoo na madarasa pamoja na
kuwapatia wanafunzi na walimu vifaa vya elimu.
Awamu
ya kwanza ya Mradi huo ilizinduliwa Machi 17,2012 ambapo kwenye awamu
hiyo kulifanyika kampeni za kuhamasisha wadau kuchangisha pesa na
kufanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh.155.5Million, ambazo zilitumika kwa
kununua madawati 500 ya Shule ya Msingi, 480 Shule za Sekondari na viti
100 vya shule ya awali pamoja na kufanikiwa kuchimba kisima cha maji
katika kila shule.
Awamu hii ya pili ya mradi itajihusisha zaidi kwenye ujenzi wa vyoo na madarasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...