TAARIFA ILIYOIKIA GLOBU YA JAMII HIVI SASA TOKA JIJINI MWANZA,INAELEZA KUWA KUNA HALI YA HATARI INAENDELEA HIVI SASA JIJINI HUMO KATIKA MTAA WA MISSION BARABARA IENDAYO AIRPORT,KUTOKANA NA WAENDESHA BODA BODA KUANZA KUANDAMANA KUPINGA PATROO INAYOFANYWA NA JESHI LA POLISI LA KUWAKAMATA WALE WOTE WASIOKUWA NA LESENI ZA KUENDESHEA VYOMBO HIVYO PAMOJA NA VIFAA VYA KUJIKINGA.

JESHI LA POLISI LIMELAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI NA RISASI ILI KUZUIA GHASIA HIYO .

"KWAKWELI HALI NI MBAYA SANA HAPA MWANZA HIVI SASA,KWANI RISASI ZINALIA KAMA VITANI,YAANI NIMO NDANI YA OFISI YANGU NA NAONA JINSI POLISI WANAVYOTUMIA NGUVU KUBWA KUPITA KIASI,YAANI NI RISASI TUPU NA NIMEJIFUNGIA NDANI YA OFISI." HIVI NDIVYO ALIVYOKUWA AKISEMA MTOA TAARIFA.

ALIENDELEA KUSEMA "WATU WANAKIMBIA HUKU NA KULE NA WATU WA BODA BODA WAMEFUNGA BARABARA KWA MAWE,YAANI NI BALAA TUPU HAPA MAKONGORO ROAD.WADAU MNIOMBEE RISASI ISIPITE DIRISHANI IKANIKUTA KWENYE MEZA YANGU. MUNGU IBARIKI TANZANIA.JAMANI AMANI IDUMISHWE" 

HIVYO NDIVYO MAMBO YALIVYO HIZI SASA,NA TUTAENDELEA KUJUZANA KADRI TAARIFA ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nyie 'boda boda' ndiyo tunatambua mmejiajiri lakini mnatakiwa kufuata taratibu na sheria za uendeshaji wa hizo piki piki na si vinginevyo.Polisi mpo sahihi lakini msitumie nguvu sana kupita kiasi.Daresalaaam ndiyo usiseme boda boda hii inaku-overtake kushoto,nyingine kulia ,nyingine kwa mbele yako,hujakaa sawa Kibajaji kimekatisha barabara,wakati huo huo daladala imesimama katikati ya barabara inapakia abiria.Burudani kweli kweli.

    David V

    ReplyDelete
  2. Waendesha toyo nao aje ..?? Mbona wataka kutuharibia hali ya hewa ..si wafuate sheria au wanadhani kila siku wanavyofia barabarani tunafrahia kuona damu zao na viungo visivyowezwa kuunganishwa tena..

    ReplyDelete
  3. fanyeni utafiti wa kina zaidi,tatizo la mgongano wa Bodaboda na Mapolisi Mwanza , ni zaidi ya hilo unalo lizungumzia,la Helmet na Leseni au Bima!its a pity!kuna harufu za siasa ndani yake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...