TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.
Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania. 
 Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini.
Taarifa iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji nchini.
Taarifa iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM

30 Januari, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Aksante JK. Umetambua masikitiko yetu wanawake na wanaume wakereketwa wa usawa kijinsia, husika wadhifa wa Dr. Asha Rose, hasa kutokana na uwezo wake na wadhifa mkubwa aliyokuwa nao UN. Ni matumaini yetu, Viongozi na Watanzania kwa jumla tutaendelea kumuwezesha katika ngazi za maamuzi ya juu zaidi, kwa sababu uwezo ameudhihirisha, na sababu zipo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...