TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Taarifa
iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza
Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.
Mheshimiwa
Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
Aidha,
Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na
Uokoaji nchini.
Taarifa
iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha
ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013.
Aidha,
taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Bwana Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji
nchini.
Taarifa
iliyotolewa mjini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Y. Sefue, leo, Januari 30, 2013 inasema kuwa uteuzi wa Bwana Nyambacha
ulianza Jumanne ya Januari 22, mwaka huu, 2013.
Aidha,
taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Nyambacha alikuwa Kaimu
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
30
Januari, 2013
Aksante JK. Umetambua masikitiko yetu wanawake na wanaume wakereketwa wa usawa kijinsia, husika wadhifa wa Dr. Asha Rose, hasa kutokana na uwezo wake na wadhifa mkubwa aliyokuwa nao UN. Ni matumaini yetu, Viongozi na Watanzania kwa jumla tutaendelea kumuwezesha katika ngazi za maamuzi ya juu zaidi, kwa sababu uwezo ameudhihirisha, na sababu zipo.
ReplyDelete