Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa daraja la kisasa katika eneo la Mbutu,Wilayani Igunga leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa Chujio la maji safi kwa mji wa Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi zaidi ya asilimia 70 wa mji huo watapata maji safi.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mashine ya kuchimbia mashimo ya nguzo
za daraja kabla ya kwenda kukata utepe kwa kuashiria kuzindua ujenzi
daraja la Mbutu,Wilayani Igunga leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanroads,Eng. Patrick Mfugale (alieshika maiki) akumuonyesha Rais Kikwete ramani ya Mradi wa Ujenzi wa daraja la kisasa katika eneo la Mbutu,Wilayani Igunga.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kutoa ushauri kwa kundi la vijana 10
ambao baada ya kumaliza chuo kikuu wamejikusanya na kuunda kikundi cha
ujasiriamali mjini Igunga wakijishugulisha na Kilimo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikagua sehemu ya vyanzo vya mradi mpya wa maji
safi kwa mji wa Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi asilimia 70 wa
mji huo watapata maji safi
Wananchi
wakivuka katika sehemu itayojengwa daraja la kisasa eneo la
Mbutu,Igunga Mkoani Tabora ambao ujenzi wake umezinduliwa leo na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, hatua ambayo itatatua kabisa tatizo la
miundombinu.PICHA NA IKULU
Ewe mwenyezi mungu mwingi wa rehema tusaidie haya mateso yapungue kama si kwisha kabisa, watu wanapata taabu sana ebu weka fikra ktk picha hii ya mwisho hapa chini, tafsiri ya haraka inayopatikana ni kwamba huo upande ambao watu wanaelekea pengine ndio wenye huduma muhimu za kijamii hivyo basi miaka nenda miaka rudi hayo ndio maisha yao hawa watanzania wenzetu wa huko.Mtoto mgongoni, begi kichwani na baiskeli juu.Kwakweli nakubaliana na wote wenye mapenzi mema na hii nchi hasa ktk wazo la kuendeleza mikoa husika kwa rasilimali zinazopatikana ktk mkoa huo kwa nia njema tu na si zote kuziamishia eneo moja ili kufanya watu kwabaki ktk maneo yao na kuyaendeleza, vinginevyo itakua kama ionekanavyo ktk picha hii hapo juu wote wanaovuka huo mto ni watu wazima kwa wazee yaani wale wasio weza kuondoka maeneo hao, yawezekana vijana wote wapo Dar. Hii pia itaepusha kukimbizana na mapolisi huku mjini.
ReplyDeletemiaka 50 baada ya uhuru tunatia aibu wakati baadhi ya viongozi wanamabilioni ya pesa uswis yaani nasikia uchungu sana,,,
ReplyDelete