Moto mkubwa umezuka na unakiunguza kiwanda cha vipodozi cha ChemiCotex kilichopo huko Africana njia ya Tegeta jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha moto huo hakijafahamika ingawaje inahisiwa kuwa huenda ni hitilafu iliyotokana na fundi aliyekuwa akichomelea kitu ndani ya kiwanda hicho.

Wahusika wakuu wa kiwanda hicho hawakuwa katika eneo husika ili kutoa maelezo zaidi. Taarifa zinasema kuwa magari ya kikosi cha zima-moto yalipowasili, watu walianza kuyarushia mawe kiasi cha kutishia usalama wa watu wengine ambao waliamua kuondoka kutoka katika eneo la tukio.

Jitihada  za  kumtafuta kamanda  wa  polisi  wa  kanda maalum ya Dar es Salaam Suelein Kova  bado zinaendelea baada ya simu yake  kuita bila  kupokelewa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ZAIDI YA MASAA MAWILI YALIPITA ZIMAMOTO HAWAJAFIKA! NDIO MAANA WANANCHI WENYE HASIRA WAKAWAVURUMUSHA KWA MAWE WALIPOFIKA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...