Heri ya mwaka mpya 2013 watanzania wenzangu ,tunauanza mwa huu mpya kwa msimamo mmoja wa kukuza maendeleo ya michezo na sanaa nchini kwetu Tanzania,
Watanzania tuna uwezo mwingi wa kufanya mambo makubwa katika medani za kimataifa, kama vile muziki ,michezo na mambo mbalimbali, ila hatuna ushirikiano ,vilevile pia kudharauliana kwingi, kitu anchofanya mzawa watu hukibeza na kikidharau badala ya kukisapoti. Hivi nani anajua kama kuna Mtanzania toka Zanzibar alikuja Marekani akiwa na umri wa miaka 15 anaitwa FRED MERCRYhttps://www.youtube.com/watch? v=xdCrZfTkG1c&feature=youtube_ gdata_player,mwanamuziki ambaye nyimbo zake mpaka leo hii zinatumika katika michezo mikubwa kama vile Baskett ,football hockey na mingeneyo hapa nchini Marekani katika utangulizi kabla ya mchezo kuanza
Sio huyo tu tuna watu mbali mbali toka nchini ambao wameonyesha vipaji nje ya nchi kama akina Filbert Bayi ,John Bura, Nyambui katika mbio Rashid Matumla ngumi, mpira Peter Tino ,Dilunga , MOGELLA Pondamalli na wengineo walitufikisha katika fainali za kombe la Afrika miaka ya 80 mwingine mwanzilishi wa Bongo flavaDandu muziki wake unapigwa nje mpaka leo.Sasa kwanini tuishie hapo wakati uwezo tunao, ila ni sababu hatuna ushirikiano.Hatuthamini vitu vya nyumbani tumeupa nafasi utamaduni wa kigeni badala wa nyumbani.
Mfano mzuri mimi ni mwafrika wa kwanza ambaye nguo zangu zinavaliwa Dunia nzima , lakini watanzania wenzangu badala ya kuniunga mkono ndio kwanza wanabeza na kudharau nguo, gani hizo kisa Kajumulo katengeneza. Sasa sio wakati wa kuilaumu serikali eti haitusaidii badala ya kujilaumu wenyewe kwa roho zetu za ubinafsi.
Tunasema serikali imetutelekeza vijana, huku tukitaka wazee wote wang'atuke kwenye uongozi je? ni kweli unafikiri tutafika kwa mtindo huu wa vijana kuinga tamaduni za kigeni si tutashia Tanzania kuwa Taifa la kigeni. hivi inakuwaje wasanii vijana wa nyumbani tunashindwa hata kuuzaata hata nakala 200 tu za CD nje ya nchi Wakati huo tunatumia pesa za kigeni kununulia vifaa hivyo vya muziki wakati vinatupotezea hela haviingizi kutoka nje.
Ushauri wangu nikiwa kama mdau mkubwa wa michezo na sanaa nchini kwetu Tanzania, nchi yetu haiwezi kuendelea kimichezo na utamaduni bila ya kuwa na ushirikiano mkubwa baina yetu.Huwezi kumuona Mwingereza kavaa jezi ya Simba ama Yanga au kuona Mwamerika anasikiiza muziki wa Diamond lakini nyumbani kila kijana anatamani awe mwamerika .je vijana mna haki ya kulalamika serikali umewatupa?
Siongei hivi kama mwanasiasa ila nina uchungu na maendeleo ya nchi yangu .Nipo huku ugenini kwa ajili ya maslahi ya nchi yangu,sijaiba wala kufanya biashara haramu, ninachotaka ni kuonyesha kwamba kumbe kuna watanzania ambao wanaweza kufanya biashara nje ya nchi na wakakubalika.
Hizo ni salamu zangu kwa mwaka huu 2013 tupige harambee ya michezo na sanaa ili mataifa mengine yatujue ,mpaka sasa nimeshauza zaidi ya milioni 20 nguo za kajumulo lakini ni watanzania wachache wanaunga mkono je Addidas, Nike , Puma na Kappa wasingesaidia nchi zao kimichezo wangefika wapi ?
HIVYO NAOMBA USHIRIKIANO...
HERI YA MWAKA MPYA
ALEX KAJUMULO



Jina la kisanii ni Freddy Mercury; ni Mzanzibar mwenye asili ya Kihindi alikuwa akipiga na bendi ya Queen ya UK. Alihamia UK akiwa na umri wa miaka 15 na alikufa kwa AIDS akiwa na urai wa UK. Ughaibuni kufanikiwa ni bahati tu, kuna wenye vipaji wengi tu. Vijana wa kiTZ wasipoteze wakati wao kusaka vipaji bali wasake elimu.
ReplyDeleteREKEBISHA data zako,Fred Mercury alikuja uingereza tokea zanzibar na sio marekani
ReplyDeleteFreddie (Freddy) Mercury si Mtanzania ni Muingereza kwa uraia ila tu alizaliwa Stone Town Zanzibar. Ile restaurant maarufu pale Zanzibar inayotumia jina lake ndio kumbukumbu hai iliyobaki kwa gwiji huyu kwa upande wa Tanzania. Kuacha kuzaliwa tu Tanzania, utambukisho wake, umaarifu na sifa zake zilitambulishwa na Britain (kama British!) na si Tanzania au Zabzibar.
ReplyDeleteTunapenda kutoa support ila wrwe mwenyewe nio unaonekana kama mbabaishaji mara unacheza mpira , wewe ndio kocha , wewe ndio mwanamuziki , wewe ndio mwekezaji , wewe ndio promoter sasa sijui wee hsa identity yako ikoje . JAribu kuappeal vizuri zaidi kuwa umefanya kazi A, B,c n D , mafanikio yaliyopatikana ni K ,L ,M na N badala ya kukaa na kulaumu . Ushindabni wa kibiaahara ni mkubwa hivyo unaweZA ukawa na nguo nzuri ila jina ni baya likwa haliuziki . Mfano mzuri ni Bridgestone Tyres ,...... onwer wa kampuni hii ni mjapani jina lake ni Hashimoto baada kuanza biashara yake Marekani alipata upingamizi wa hali ya juu nna ubaguzi wa rangi for Nikkei ( Asians Japanese ) biashara yake ikaenda mrama ila hakufa moyo akarudi tena na nguvu mpya akabadili jina la kampuni na kuita Bridgestone hashi ni daraja moto ni jiwe kwa kijapan hivyo he called it Bridgestone aa hivi ni Number One tyre seller ulimwenguni . What i wanna say here it try to do big research first before complaining
ReplyDeletejaribu kuwasiliana na watu wa naming companies uone watakupa ushauri gani halafu ndipo utuletee vitu sokoni kama havitauzika .
Weka jina fupi not more than six words with good emblem mfano KAJU ....
VILE vile punguza kutanga tanga ovyo kabla hujaonyesha kitu cha maana .Never give up the fight
With all due respect kaju, lakini kuzaliwa mjini shule! kwani Freddie Mercury kama wadau wanavyosema ni muingereza and alizaliwa Zanzibar na kupelekwa boarding school India akiwa na miaka saba,kila mtoto wa mjini lazima alisikilza nyimbo zake au kumsikia msanii mwenyewe, jamani muwe- mna google au tembelea wikipedia kupata habari za wato mashuhuri na muache kukurupuka tu na kujiaibisah.
ReplyDeleteFred Mercury asili yake hasa wazazi wake asili yao ni wa-Persian(Iran) walikuwa raia wa Uingereza, waliowahi kuishi Zanzibar na ndipo Fred alipozaliwa. alikuja kuibukia na kuwa mmoja wa wanamuziki maarufu akiongoza kundi lake aliloliita Queen. alikuwa ni mmoja wa wanamuziki waliowahi kujitangaza kuwa ni shoga na alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi. sasa mjomba Kaju next time jaribu kutoa habari zilizo sahihi. na ndio maana watu wanakuwa hawakuamini amini wanakuona kama magumashi( Tapeli). mdau UK.
ReplyDeleteKajumulo bwana! We aliyekuambia Fred Mercury ni Mzanzibari nani?! Huyo jamaa Baba yake alikuwa ni afisa wa Serikali ya Kiingereza Zanzibar na baada ya mapinduzi ya kumtoa Sultan Jamsheed jamaa wakakimbia nchi wakarudi UK na baadae akapelekwa India kusoma. By the way jamaa alikuwa GAY sasa sijui unachosifia ni kitu gani.We jisifie wewe sie tutakusapoti tu kaka.
ReplyDeletewote mmeacha pointi na kuzungumzia Fred (RIP). Oh alikuwa ponjolo, oh alikuwa mgunya. Hii inaonyesha wazi kuwa wasomaji wengi hatuwezi kusoma na kuelewa ujumbe mkuu ni upi. Ila tunatafuta penye kosa ili tukosoe. Kweli Bongo hatunazo!
ReplyDeleteKaju wewe kaza buti, hata hao waliokwenda hatua mia walianza na hatua moja. Wenye akili ujumbe tumeupata. Wajuaji waache wakusahihishe.
Tatizo la si waswahili ndio hilo yeye huyo Fredy mercury katoa kama mfano tu wamtanzania aliyefanya vzuri nje ya nchi. Kweli bongo residence ignorance is your shadow.
ReplyDeleteNdugu yangu kajumulo hebu rudia tena? eti wewe ni mwaafrika wa kwanza ku-design nguo na kuuza duniani? au unamanisha MTANZANIA wa kwanza?
ReplyDeleteWakina CHARLES FREDERICK au Zelda wynn valdes na chata zao wasemaje?
Hongera kajumulo kuwa mwaafrika wa kwanza kudesign pamba na kuuza duniani nimeona hata kwenye Guenes book of record!!!!! lol
ReplyDeletekumbe huyu baba mwehu?
ReplyDeletekama nguo zako zimekosa soko jaribu viatu sasa! alafu utuambie wewe ni mwafrika wa kwanza kutengeza na kuuza viatu ulimwenguni!
ReplyDelete