Wafanyabiasha Wakitanzania washio jiji la London siku ya Jumamosi, tarehe 23, mwezi 2 walitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe.
Lengo la ziara hiyo ni kubadilishana nao mawazo na kuangalia jinsi gani wafanyabiashara hao wanavyoweza kutumia fursa za kiuchumi zinazojitokeza nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo wafanyabiashara hao walimueleza Balozi Kallaghe mafanikio yao na changamoto zinazowakabili kwanye uendeshaji wa shughuli zao za kila siku.
Wafanyabiashara waliotembelewa ni pamoja na Bi. Jennifer Wright anayemiliki biashara ya kuuza na kununua nyumba pamoja na Soloon za nyele, Bw. Augustino Msey mwenye kampuni ya Swahili Travel and Tours, Moona Store (dukani kwa Sadi) wauzaji wa vifaa vya umeme na wakala wa Westen Union, Salumu wa Barking anayemiliki Foro Barbeque Food, na pia Balozi Kallaghe alipata fursa ya kuhudhuria uzinduzi wa kikundi cha jamii cha Istiqama UK. Balozi Kallaghe aliambatana na wanajumuia ya Kitanzania Bw. Haruna Mbeyu na Bi. Mariamu Mungula.
Balozi Kallaghe alipokutana na mmoja wa wafanyabiashara Bi. Jeniffer Wright alisema kuwa yupo tayari kuwasaidia Watanzania waishio Uingereza na waliokuwepo nyumbani kwa kuwapa mafundisho na maelekezo ya kibiashara kutokana na ujuzi aliokuwa nao. Pia Bi. Wright aliomba serikali ya Tanzania ipunguze vizuizi vya biashara ili waweze kuwekeza nchini Tanzania. Nae Mwenyekiti wa Swahili Group Bw. Augustino Msey alisema kuwa kampuni yake inajitahidi kuitangaza Tanzania katika sekta ya utalii. Bw. Msey aliendelea kusema kuwa kampuni yake inafanya mikakati mikunbwa ya kuwekeza nchini Tanzania. Vilevile Forodhani Barbeque Food waliomba serikali waliangalie suala zima la uraia pacha, kwani Watanzania wanapata tabu sana na vizuizi vingi wanapotaka kuwekeza nchini.
Balozi Kallaghe aliwashauri Watanzania wote wajumuike kwa pamoja, na washirikiane kuleta maendeleo na kuwekeza nchini Tanzania na vilevile wanapopata matatizo wasisite kwenda ubalozini kutaka ushauri na kuomba msaada.
Hongera Mhe. balozi Peter Kallaghe kwa kuwafikia wanandugu huko nchini Uingereza.
ReplyDeleteSuala hili la ushiriki wa Madiaspora ktk kuakisi maendeleo nchini Tanzania na kuwajenga huko walipo ni la kupewa uzito mkubwa.
Nchi zilizofanikiwa ktk suala la Diaspora kwa kiasi kikubwa ni Israel, Uswisi na Canada ndizo nchi kongwe kwa kuwa na Jamii ya Madiaspora kwa miaka mingi sana:
Mfano:
1.Waisrael, ni ktk Jamii kongwe sana duniani iliyokuwa mstari wa mbele kusiamia watu wao popote walipo duanini. baada ya vita kuu ya Pili 1939-1945 Waisrael walitawanyika dunia nzima lakini waliweza kujiunga na kushikamana na kwao, licha ya vikwazo na changamoto walizozipata wakiwa uhamishoni kama wengine kulazimika kuishi kwa siri na kuficha kujulikana ni wa Israel.
Udisapora wa Waisrael umeigusa Afrika mfano wale Jamii ya Mafalashas wa kule Ethiopia ambao wameishi kwa Karne nyingi sana pale, huku watu wengine Wahabeshi wakiwa hawajui kumbe Mafalashas walikuwa na mawasiliano na nchi yao ya asili Israel hadi mwaka 1984 wanakuja kufanyiwa mpango wa kurudishwa kwao Israel.
Pia kama tunavyoona ktk Historia ya Kidini Waisrael wamekuwa Madiaspora tokea Karne nyingi huko nyuma mfano walipokuwa Misri chini ya Utawala wa Farao hadi wanakuja kombolewa na Nabii Mussa kurudi kwao Israeli.
2.Waswisi pia ni mojawapo ya Jamii kongwe iliyoweka mawasiliano na Madiaspora wao duniani kwa kuwa Waswisi wametawanyika nchi karibu zote za dunia haswa Marekani na Ulaya nzima tokea Mapinduzi ya Viwanda miaka ya 1890 hadi 1900 hivi lakini wamekuwa na mawasiliano na kwao.
3.Canada pia inasemekana kuwa na Jamii kongwe ya Madiaspora duniani.
Hivyo nchi zote hizo zina Mipango makini juu ya Jamii ya madiaspora na zinahakikisha ya kuwa wanatoa ushiriki ktk maendeleo ya nchi yao, hivyo zimeweka mipango mingi haswa kama hii ya:
(i)-Uraia wa nchi mbili (Pasipoti 2).
(ii)-Sheria ya uandikishwaji ukazi wa nje yanchi.
(iii)-Haki za wakazi wa nje ya nchi kushiriki kupiga Kura.
(iv)-Muunganiko wa Kijamii kwa walio nje na nyumbani kukuza Utamaduni, na kushiriki kuchangia mawazo na kuchangia Mijadala mbali mbali (dialogue).
(v)-Uwekezaji nyumbani.
Hivyo nchi nyingi zimetoa uwezekano wa vitu hivyo muhimu vitano (5) juu ili kutoa nafasi ya ushiriki wa Madiaspora nyumbani.
LA MUHIMU KTK NGAZI YA UNGOZI MADIASPORA KTK NCHI NYINGI KAMA HIZO 3 HAPO JUU HURUHUSIWA KUPIGA KURA ,KUONGOZA LAKINI KWA NGAZI FULANI ZA UONGOZI WA CHINI NA SIO UONGOZI UWANDAMIZI NA WA JUU KAMA URAISI.
HIVYO NA SISI TANZANIA TUNAWEZA KUHARAKISHA KWA HAYO MATANO KWA JAMII YA MADIASPORA WETU.
Ongera Forodhani Barbeque Food kwa kuongelea swala la uraia pacha, naona serikali inalipiga dana dana. Na jamaa wengi wanaogopa kuliongelea kwani serikali imepandikiza mashushu wake dunia nzima, sana sana Ulaya na Marekani. Ukweli utabaki kuwa ukweli, mie pamoja na jamaa wote nao wafahamu hapa Marekani wanasadia sana Bongo, na wakati wote wabongo waliopo hapa wanaongelea nyumbani.
ReplyDeleteNa mdau wa Tue Feb 26, 09:48:00 am 2013 umeongea point, lakini umenipoteza kwenye habari ya uongozi, sijui wala sielewi rais ghani anweza kuuza Taifa lake kwa Taifa lingine?!! Nifafanulie.