Chezea biashara huria weye. Hapo ni katika mgahawa wa wasafiri wa ndani (mikoani) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo hilo andazi la mviringo maarufu kama doughnut linaenda kwa bei hiyo hapo chini. Hicho kikombe cha kahawa ni 1,500/-

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. makubwa ukila usikii njaa wiki nzma au?

    ReplyDelete
  2. pole sana usiku huu nawewe unakwenda wapi? ungeanzia kariakoo .bonge la halfcake 250/- kahawa 100/-usingetumia hata buku!

    ReplyDelete
  3. Inategemea na gharama za pango labda, otherwise huo ni wizi uliohalalishwa, na mnunuzi anaibiwa kwa hiari yake.

    ReplyDelete
  4. Mgahawa huo wako dunia gani,hata Davos[swiss] andazi halijafikia bei hiyo,fair trade,rubbish;

    ReplyDelete
  5. doughnut!!!!!!!!!! Hilo linaitwa kafie kwenu. hata jiwe lina sura nzuri. Loooo, Hivi hata tundu ya doughnut hamwezi kuicopy na kupaste.

    ReplyDelete
  6. Tatizo nini? Kwani lazima ule hapo?Malalamiko kila siku wewe Tuachie wenyewe nyie nendeni huko huko kwenye nafuu.

    ReplyDelete
  7. WAPI BEI ELEKEZIIIII???? kwa kweli huu ndio wizi uliotukuka..watu hawaoni hata aibu jamani??

    kuna haja ya kutafuta kitengo cha kushughulikia hizi bei za vyakula migahawani kama ilivyo kwa EWURA na SUMATRA...

    ReplyDelete
  8. upuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuzi

    ReplyDelete
  9. Nahisi mmiliki wa mgahawa alibase sana na exchange rate ya ama UK Stg Pound au US Dollar. Kwa bei zake (madafu)ukiibadilisha kwenda ktk pesa hizo za kigeni, na maeneo kama hayo (airports)duniani, mjasiriamali huyu hajakosea kabisa. Anaweza asiwe na nia ya kumkomoa mtu, ila tu angezogeza hiyo biashara yake pale jirani njia panda na au maeneo yanayofanana nayo, hapo inabidi tulalamike. Ni maoni yangu tu

    ReplyDelete
  10. Tatizo la nchi yetu wafanya biashara wanatufanya wajinga.acha hiyo ukienda south Africa ,mr price no Duka la masikini wasio weza kununua nguo Maduka mengine lakini uku ndo matajiri wanaingia

    ReplyDelete
  11. Jamani yaani siku moja nilikua nasafiri, sasa kwa pilika sikuweza kula nyumbani mapema nikasema nitakula airport na nilikuwa na mtoto, kwa kweli nilichoka na bei za pale, naungana na mdu aliyesema utafikiri ukila hapo basi utashiba wiki nzima. kwa kweli vimigahawa vya airport yetu ni wezi wakubwa

    ReplyDelete


  12. Yaani mnakosa kazi kaisaa kazi kujadili ujinga hahahaha haha bure kabisaa

    hamjui kama hapo ni airport lazima bei iwe juu kama hutaki nenda kanunue kkoo hujalazimishwa mwenzenu analipa kodi na ukisha nunu risiti unapewa kabisaa ina TIN number tena anatumia fiscial device

    acheni ujinga jamani think wise

    ReplyDelete
  13. aah hizo sehemu za kina ankali na mafisadi wenzake ndio wanaziweza teh teh teh teh hata huku ughaibuni hilo andazi halijafikia bei hiyo tunanunua mandazi 4 kwa euro 2 ni sawa na hiyo buku 4 ya huko ina maana kila andazi ni sent 50 sawa na buku moja ya huko tz

    maisha mema watanganyika.

    ReplyDelete
  14. JAMANI PICHA YA DOUGNUT GANI INASHEPU KAMA MAVI?HUYU SHEFU ANATUAIBISHA KAUZIE MANZESE.

    ReplyDelete
  15. Hapo panawafa watu wenye hera zao. Sio sisi tunaoishi maisha ya kutumiachini ya dora 1 kwa siku

    ReplyDelete
  16. Wee, Anonymous said.... Sun Feb 03, 12:09:00 pm 2013, Mimi niko hapa LONDON, Uingereza hizo sio bei zake hata Heathrow Airport sijaona bei kama hiyo converted into UK Stg Pound au US Dollar. Hii ni kutapeli watu. Wanaweza kununua kwa sababu wana njaa au Wazungu kununua kwa sababu ni chakula walichokizoea.

    Hata kama ni Airport rates, Dar es Salaam haiilingani na Heathrow (UK)
    au JFK Aiport (USA).

    ReplyDelete
  17. Andazi na Ghahawa inauzwa ktk 'Duty Free shop' hapo Dar JNIA ndo maana bei ni kubwa.
    Mdau
    Amsterdam

    ReplyDelete
  18. Umelazimishwa kula? umetaka mwenyewe kuibiwa.

    ReplyDelete
  19. Kwanza hizo bei ni rahisi sana maana ulanguzi kwa wasafiri ni kawaida hata pale El jaziira wako hivyo na wale wauzao vinywaji ktk mabasi ndo usiseme. Ufisadi kula kona. Man eat man.

    ReplyDelete
  20. mnaongea sanaaa, bei za viwanja mbona hamuongei au bei za pango pale kariakoo mbona hamuongei,kwani hizo bei zinasimamiwa na nani? au ndio globalization? hii nchi imelogwa,chezea kubadilishana udongo weyeee.kafara la kufa mtu labda Yesu arudi.

    ReplyDelete
  21. Bongo akili kichwani,

    La muhimu ukijiandaa na safari kula zako Gengeni moja kwa moja huko Vingunguti,Ukonga Banana au nje ya Uwanja wa Ndege kwa kuwa Bei za ndani ni kwa Wasafiri LUXURY WA DARAJA LA KWANZA na walio kuwa Mabosi wanaoaminika hawana hela za mawazo!

    ReplyDelete
  22. Kahawa zinazouwa Tsh.50/= na Vijana wa Mabirika mikononi kwetu Keko Magurumbasi Uwanja wa Ndege Tsh. 1,500/=?

    Hiyo bei ni PAMOJA NA VIWANGO VYA WIZI badala ya VIWANGO VYA UBORA!

    ReplyDelete
  23. Sasa mnabisha nini Kahawa kuuzwa Tsh.1,500/= kwa kikombe?

    Mnajuaje kama Waandaaji wameichanganya na poda la mizizi ya 'MKUYATI' ndani yake?

    ReplyDelete
  24. Wafanyabiashara wengi Tanzania hasa hivyo vimigahawa wanadhani ni ujanja kuwagonga watu ndio maana biashara zao hazikui zinabakia palepale hvyo vyakula vyote wanavyouza hapo ni JUNK FOOD kwasisi tuliotembea sehemu mbalimbali duniani na hata wazungu wajanja hawanunui hivyo vyakula vilivyo jaaa mafuta na wanga kwa wingi tunaviita vinnenepesho sio vyakula vizuri kwa afya yako. Wasio elewa atawapata wajanja wanao elewa hawatanunua hata mmoja
    Mdau UK

    ReplyDelete
  25. sasa ww mdau wa LONDON unayenibishia kuwa heathrow haifiki bei kulingana na hizo, je kile kikombe cha kahawa, au capuccino pale Cafe COSTA au Starbucks cha zaidi ya 2 pounds, je ukiibadilisha kwa madafu bado tu haifikii kama siyo kuizidi hiyo sh 1,500/=? Kama ni hivyo, je unaweza unaweza kupata kahawa pale heathrow ya 60pence ambayo ni sawa na hiyo 1500 ya bei ya hapo Kipawa? Kama kweli ww upo UK, 60p ni bei wanayouzia kajikombe ka kawaha ktk bookies kama Coral. Na kama kweli ile migahawa yenye majina itakapouza kwa hiyo 60p, basi nahisi siku hiyo mateja, ma-homless woooote wa UK wataenda kalala kuhemea hapo. KWA HERII

    ReplyDelete
  26. huu ni wizi, hata Washington DC andazi kama hilo ni shilling 1500 tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...