Athumani Nyamlani kugombea Urais TFF peke yake

Ni wagombea wawili tu kati ya 10 waliokatiwa na kukata  rufaa  dhidi ya pingamizi  kadhaa walizowekewa ndio wamerudishwa kwenye kugombea nafasi katika uchaguzi mkuu wa chama cha soka nchini TFF, Globu ya Jamii inaweka wazi.

Mgombea nafasi ya Urais Bw. Athumani Nyamlani na mgombea Ujumbe wa kamati ya Utendaji Bw. Shafii Dauda ni wagombea pekee walioweza kushinda rufaa zao na kujisafishia njia kugombea nfasi hizo katika uchaguzi mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika  Fenruari 24, mwaka huu.

Yusuf Manji- Ndani
Jamal Malinzi - Nje
Vile vile, katika kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya ligi ni Yusuf Manji wa Yanga  pekee aliyepenya baada ya mgombea mwingine, Bw Hamada Yahaya wa Mtibwa Sugar, kuchinjwa kwa kuwa yeye si mwenyekiti halali ya klabu hicho kwani alikasimishwa madaraka na alipaswa kuitisha mkutano mkuu wa klabu kumhalalisha kuwa mwenyekiti.

Ndio kusema siku hiyo ya uchaguzi nafasi ya Urais na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi kutakuwa na kura za NDIO na HAPANA kwani wagombea wake hawatakuwa na upinzani.

Michael Wambura - Nje
Maamuzi hayo ambayo yametolewa usiku huu na mwenyekiti wa kamati ya Rufaa Bw. Idd Mtinginjola ni ya mwisho na wagombea hao hawaruhusiwi kukata rufaa katika kamati yoyote ingine.

Majeruhi wakuu waliochinjiwa baharini katika kindumbwendumbwe hicho ni pamoja na Bw. Jamal Malinzi aliyekuwa anagombea Urais, pamoja na  Bw. Michael Wambura aliyetaka kuwa Makamu wa Rais.

Shafii Dauda - Ndani
Bw Malinzi kachinjwa kwa kile kilichotajwa kukosa kuwa na uzoefu wa miaka mitano, pamoja na kukosa uadilifu kufuatia kupinga kwake maamuzi ya TFF katika mchakato wa mabadiliko ya katiba ya shirikisho hilo.

Mwandishi wa Globu ya Jamii aliyekuwa eneo la tukio hadi matokeo hayo yanatangazwa muda mfupi uliopita anatanabahisha kwamba Bw. Wambura kachinjiwa baharini baada ya kutojisafisha na maamuzi ya Jaji John Mkwawa mwaka 2008 dhidi ya mashtaka ya kukosa uadilifu, na hakuyakatia rufaa kujisafisha kwenye chombo cha CAS.

Warufani wengine waliopigwa chini ni waombaji wa nafasi za ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda mbalimbali, ambao ni Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Omari Abdulkadir (Dar es Salaam), Eliud  Mvella (Iringa na Mbeya) na Omary Mnkwarulo (Kigoma) aliyewania Urais.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kupinga mamuzi ya TFF ni kukosa uadilifu? Kama ni hivyo hapakuwa na sababu ya kuwaomba wajumbe wa mikoa kuridhia maamuzi ya TFF. Kuwaomba kulimaanisha kwamba walikuwa na uhuru wa kutoa maoni yao vinginevyo uamuzi huu unamaanisha kwamba kupinga mawazo au maoni ya TFF taifa ni kukosa uadilifu. Kwa lugha nyingine maamuzi ya rais wa TFF ni amri au sheria yakipingwa ni kuvunja sheria!!!! Nchi hii bila kuacha mizengwe na "uswahili" hatuwezi kupiga hatua ktk soka. Inaelekea kuna watu fulani hawatakiwi ktk uongozi wa TFF kwa gharama yoyote.

    ReplyDelete
  2. abubakar dsmFebruary 12, 2013

    ni kweli hao waliongia na viongozi wanaoondoka hawataki bw malinzi na wambura waingie kwa garama yoyote kwani watagundua uozo na ubadhilifu wa fedha ndani ya tff.huu ni uonevu wa wazi.kwann wasiwaweke halafu wakakose kura mbele?wanajua wanaweza kushinda.utawekaje mgombea 1?si ndo kumpitisha huko.haki itendeke jamani

    ReplyDelete
  3. we tff sio nchi usitujuuishe wengine kwenye mambo yasiotuhusu.

    ReplyDelete
  4. Mambo ya Putin ndani ya TFF hayo, unafanya mchezo.

    ReplyDelete
  5. hawa wambura na Malinzi wangesababisha vurugu kubwa kwenye uongozi wa soka Tanzania,na tumshukuru Mungu amewaondoa mapema kupitia pingamizi.Wamepewa nafasi ya kwenda na mawakili wao kwenye kikao na hivyo haki imetendeka.Ninawashauri warudi kwenye michezo waliyotokea,yaani ngumi kwa upande wa Malinzi na Kriketi kwa Wambura.Michezo hiyo bado inahitaji mchango wao hivyo waende huko badala ya kung'ang'ania soka

    ReplyDelete
  6. Hivi bado tupo kwenye Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea?

    Kwa nini Mgombea Uraisi wa Chama cha Mpira TFF awe mmoja na hana Mpinzani?

    ReplyDelete
  7. Ehhh makubwa!

    Mgombea Uraisi yupo peke yake hana Mpinzani!

    Amekuwa ni JINI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...