Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono. Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho umemwambia mumeo nakupenda lini?. Majibu mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema Leo, wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha akawaambia, kila mtu achukue simu yake halafu amtumie mumewe text yenye maneno. NAKUPENDA MPENZI, kisha wabadilishane simu. Wakaambiwa kila moja asome majibu kwenye simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama ifuatavyo;

 
Simu 1- Samahani nani mwenzangu?
 
Simu  2- He Mama Joji unaumwa?
 
Simu 3- Nami pia daima
 
Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?
 
Simu 5- Sijakuelewa una maana gani
 
Simu 7- Umefanya nini tena? Leo sitakusamehe
 
Simu 8-Chukua taim yako
 
Simu 9-?!?
 
Simu  10- Acha kuzunguka unataka shilingi ngapi?
 
Simu 11 – Hivi naota?
 
Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii mesej ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu leo...kudadaddaddeki....
 
Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na mimi.
 
Simu 14 -  Umeanza lini ?
 
Simu  15-  Mambo ya vijana hayo !
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Du hii kali! Maana ni keeling, wanawake wengi ni vigumu museums wanapenda!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...