Jengo la Coco Plaza ambalo kuna Ofisi za CRDB.
Wateja wakipata huduma


Kaimu Meneja wa benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten  Mtei (kushoto) akitoa maelekezo ya huduma mbalimbali wanazotoa katika tawi hilo jipya kwa Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai. Tawi hilo limefunguliwa hivi karibuni katika jengo la Coco Plaza jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Masoko wa benki hiyo, Nasib Kalamba.

Ofisa Masoko wa benki ya CRD, Nasib Kalamba (katikati) akitoa ufafanuzi kwa mteja wa benki hiyo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai kaatika tawi jipya la benki hiyo lililopo katika jengo la Coco Plaza jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Tawi hilo, Godlisten Mtei.
Ofisa wa benki ya CRDB, JacqlineSawe akitoa maelekezo kwa mteja wa benki hiyo katika tawi la Oysterbay lililopo katika jengo la Coco Plaza jijini Dar es Salaam. 
Ofisa Masoko wa benki ya CRD, Nasib Kalamba (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa mteja wa benki hiyo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai katika tawi jipya la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wateja wakipata huduma.
Maofisa wa benki ya CRDB wakiandisha wateha wapya katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten  Mtei (kushoto) akitoa maelekezo
ya huduma mbalimbali wanazotoa katika tawi hilo jipya kwa Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai.
Ofisa wa benki ya CRDB, George Abraham kisaini baadhi ya nyaraka za kibenki.

DAR ES SALAAM, Tanzania

BENKI ya CRDB, imefungua tawi jipya  Osysterbay  jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuwafikia wateja wake, ambapo takribani  wateja 400 wamekuwa wakihudumiwa kila siku katika tawi hilo.

Tawi hilo limeanza kufanya kazi hivi karibuni, ambapo limeonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Osysterbay na maeneo ya jirani.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Kaim Meneja wa CRDB, Godlisten Mtei alisema lengo kubwa la kupeleka tawi hilo ni kuwapa huduma kwa ukaribu wateja wao waliopo katika eneo hilo.

 Alifafanua kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa ni mkombozi kwa wateja mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na watu mbalimbali.

 “Tawi letu linatoa huduma zote za kibenki, na tunazidi kuwakaribisha wateja wetu ili wajionee huduma bora zitolewazo na benko yetu na pia tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za; Mashine ya kutoa na kuweka fedha (ATM) ambayo hufanyakazi masaa 24”alisema.

Mtei alitaja huduma zingine kuwa ni pamoja na TemboCardVisa, Akaunti ya Hundi na ya watoto inayojulikana kama Junior Account pamoja, Malikia akaunti  ambayo ni maalum kwa wanawake na Akaunti ya Akiba.
 Hata hivyo aliongeza kuwa, tawi hilo litakuwa likitoa Akaunti ya Tanzanite, huduma za mikopo mbalimbali na huduma za bima ili kuzidi kuwapatia huduma bora wateja wao.

 Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa likitoa huduma ya kibenki kwa kutumia Simu ya mkononi (SimBanking), pamoja na Akaunti ya Wanafunzi ambayo inafahamika kama Scholar Account.

Meneja huyo aliwataka Wananchi na wateja wapya kutumia tawi hilo pekee katika eneo hilo ili kupata huduma za kibenki badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyombali.
Katika hatua nyingine Meneja Mauzo wa benki hiyo Richard Joseph alisema, katika harakati za kufanikisha wananchi wanajiunga na benki hiyo wameamua kuweka tawi katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam ambapo kwa siku zaidi ya watu 70 wanaojiunga na benki hiy

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera CRDB

    ReplyDelete
  2. Big congrats CRDB. Keep up the good work!

    ReplyDelete
  3. Coco Plaza ipo barabara ya Toure Drive road au barabara ya Ali Hassan Mwinyi Road ? Ankal wewe ni mtoto wa Mjini inakuwaje unashindwa kuwauliza CRDB wakamilishe habari yao hii nzuri.
    Mdau
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Coco Plaza ipo "opposite" na Coco Beach.

      Unajua, ingefaa sana mara kwa mara uwe unatoka huko ughaibuni na kuitembela nchi yako. Siyo?

      Delete
  4. Hongera sana CRDB Ltd kwani ni benki pekee ya kizalendo iliyovuka mipaka ( cross-border) na kiukweli mmefanya kazi nzuri sana kupitia MD-Kimei wenu kwani aliikuta ikiwa loss making to profit making and we can see changes. Congrats.... Ila sasa wekeza kwenye nguvu rasilimali watu wenye utaalamu kwani isije ikatokea kustaafu kwa Kimei na CRDB nayo inastaafu...pls make it as a going concern business...isije ikawa biashara za baadhi ya makabila TZ kusini..akifariki na biashara nayo inakufa.Ukumbuke Kimei kuwalipa vizuri watumishi wako wasijaribiwe na kufanya vibaya...kwakweli mzee upo juu. Hongera wafanyakazi wote na MD wenu

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 5 juu Anony wa Mon Feb 11,02:33:00 am 2013

    Hahahahaha

    Wandugu Majuu baadhi yao Bongo wanai ogopa kama Kaburi!

    Usione ajabu Mdau wa 3 wa Ughaibuni anony wa Fri Feb 08, 03:45:00 am 2013 inawezekana ndio wale wale, unajua kila mtu na siri yake alivyoondoka Bongo.

    1.Pana wengine huwa wanaondoka vibaya sana, unakuta mtu anachangiwa hadi nauli, sasa mtu huyo anapoondoka anakuwa na taswira ya kuwa Bongo mambo ni magumu daima na haiwezekani!

    2.Wengine kipindi chao Bongo waliishi maisha magumu mno ya msoto, pana Sister mmoja niliwahi kusema nae anaishi Brussels-Belgium, yeye anasema Bongo anapaogopa sana!.,,,haamini kama anaweza tena kuishi hapa kutokana na maisha magumu aliyoishi hapo nyuma akiwa nyumbani.

    3.Pana wengine wanaondoka na Misala kibao Bongo, unakuta labda anauza Redio za watu anauza viwanja ama nyumba na magari anapata nauli anaruka, sasa mtu kama huyo kuja Bongo ni mizozo!

    Si ndio ukiona mtu anatutembelea TZ ni jasiri sana na ndio tumwite shujaa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...