Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyesha kitufe kuashiaria kuzindua
rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa
uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said
Meck Sadik.
Home
Unlabelled
JK azindua utoaji wa Vitambulisho vya taifa katika viwanja vya Karimjee leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huku ni kupoteza hela tu! Kwani passport hazitambuliki kama cheti cha uraia? Kwa nini kuwe na passport na cheti cha uraia? Sielewi!
ReplyDeleteKwahiyo mdau utatembea na hiyo passport yqko kila sehemu.? Hampendi maendeleo nyie!! Nchi zilizo endea tayari wanavyo.. We sema tumechelewa ila usiseme unapassport!
DeleteJe umeifikiria gharama ya kuchapisha kitabu cha passport na kuilinganisha na gharama ya kuchapisha kadi ya ID?
DeleteNipo radhi kuwa nazo zote mbili, kwani passport nitaibeba pindi tu ninaposafiri, lakini kadi ndogo ninaweza kutembea nayo mfukoni kila siku bila kuchoka, na wala kuichakaza.
Hongera kwa hatua hii. Lakini muwe makini msije mkakosea majina ya watu. Pia maneno ya Kiswahili yaendane na Kiingereza. Kwa mfano MAJINA YA KATI na Middle Name haviendani (ingekuwa Middle Names).
ReplyDeleteMimi naona sikihitaji hichi kitambulisho kwa sababu tayari ninacho kitambulisha cha nchi yangu ambacho ni cha MZANZIBARI na ni kitambulisho tosha kabisa ,naona mmechelewa sana kwa hilo. Pia hicho kitambulisho kilikuwa kiitwe cha MTANGANYIKA na sio cha MTANZANIA kwa sababu ZANZIBAR tayari tunavitambulisho vyetu hatuhitaji tena kitambulisho chengine.
ReplyDeleteHongereni NIDA na Wadau wengine wote kufikia hatua hii.
ReplyDeleteWewe unayesema unacho cha mzanzibari hilo ni shauri lako. Si lazima uwe na hiki, usiongee kilevi levi, una maana gani unaposema cha mtanganyika? nina wasiwasi kama ubongo wako unafanya kazi sawasawa. Kama huhitaji kwanini unapoteza muda wako kusoma mambo ambayo hayakuhusu? Rais wako Shein mwenyewe atapatiwa cha kwake, kwani Zanzibar ni nchi tangu lini?
ReplyDeleteHongera sana ndugu MZANZIBARI kwa kuwahi kupata kitambulisho. Ni hatua kubwa sana kimaendeleo. Jitahidini muwahi na muwe na mambo mengine meeengi, zaidi ya Vitambulisho!ua
ReplyDeleteNataka nimweleweshe huyo mtoa maoni wa kwanza, kwa ufupi, kitambulisho hiki atakuwa nacho kila mtu ambaye ni mtanzania, wakati hiyo passport yako wanazo wachache tu kama wewe, bibi na babu yangu hawana je hao utawatambuaje kama ni raia, huhitaji kwenda shule kujua hili brother.
ReplyDeletelakini leo waliondaa jukwaa wamechemsha tuliongalia live kitambaa walifunga vibaya pic ya muheshimiwa ikawa inaonekana nusu ila mmejitahidi
ReplyDeleteKuweje Kitambulisho cha mwananchi kiwe na mwisho wa kutumika. Expiry Date. si wizi huuuuu. Kitambulisho cha kura, passport, kitambulisho cha bank(s), kitambulisho cha uraia, kitambulisho cha Bima ya afya, kitambulisho.... nitateba kikapuuuu!!
ReplyDeletePesa ziende katika elimu, afya na kilimo. Alama kufaulu darasa la saba mwaka huu imeshushwa hadi 75 points kutoka 250. Tuwe na vipau mbele vyenye maendeleo ndugu zangu na Mungu atakurehemu!
Mwadu wa Zanzibar anony wa Thu Feb 07, 11:41:00 pm 2013
ReplyDelete...Nani inaonekana hujaelimika,
Wewe huna tofauti na mtu anaemkana baba yake mzazi, kwa kuwa wakati mtoto anazaliwa anakuwa hajitanbui anakuja kujistukia akiwa mtu mzima.
Kwa taarifa yako hata ukiingia ktk web ya mataifa ni wazi huwezi kukuta Orodha ya nchi za Dunia ikiwemo Zanzibar, Utakuwa THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA!
Mduu wa Zanzibara sio (Zanzibar), hicho Kitambulisho chako ni KITAMBULISHO CHA UKAZI LAKINI HAKUNA TAIFA LA ZANZIBAR, KUNA ZANZIBAR KAMA SEHEMU YA ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA''
ReplyDeleteHIYO HATA MHE. MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD NA MHE.JUMA DUNI HAJI WANAFAHAMU, KAMA UNABISHA KAWAULIZE!
UTAKE USITAKE NDIYO HIVYO!!!
Ujanja mwingi mbele kiza!
ReplyDeleteMdau wa Tatu wa Z'Bar tatizo kubwa la wengi wa Wapinga Muungano ni akili na uelewa wa mambo!
Kama hilo lingekuwa Swala la utata Mhe. Sheikh Maalim Seif Shariff Hamad akiwa ni Mzanzibar (KAMILI NA HALISI ZAIDI YAKO WEWE, AMBAYE UNAONEKANA KABISA UTAKUWA NJE YA NCHI UKIWA MKIMBIZI AMA MBEBA MABOKSI) ,Maalin Seif angekataa kuchukua kitambulisho hapo kama unavyomwona amechukua cha kwake.
Kwa kitendo hicho ni KUWA MUUNGANO HAUVUNJIKI NA UNAKUBALIKA NA WENYE AKILI KAMA SHEIKH MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD!
Wewe mdau wa juu na majigambo yako ya passport, hivi ni watanzania wangapi wanazo hizo passport?
ReplyDeleteNa wengine hata si watz wanazo, kwa hivyo usiringe nazo sana.
kitambulisho kina umuhimu kuliko uwezo wako wa kufikili na wanatengeneza database ambapo kwa walioendelea kunakuwa na criminal records na mambo ya msingi.
ReplyDeleteIla kwa uelewa wa kiwango chenu wachache labda hatuhitaji. Hasa kutokana na kuishi katika karne ya ujima
Wewe Mzanzibar Mbeba Maboksi Mkimbizi upo nje wala huna sifa za kupata Kitambulisho cha Taifa cha Matanzania, kwani sifa hizo kwa sasa huna ulishazipoteza kwa kupewa Ukimbizi nje ya nchi!
ReplyDeleteSIFA ULISHAZIPOTEZA KWA KUPATA UKIMBIZI NJE YA NCHI.
WEWE KWA SASA SIYO MZANZIBAR NA WALA SIYO MTANZANIA!
KITAMBISHO CHA UTAIFA AMEPATA MAALIM SHEIKH SEIF SHARIFF HAMAD, KAMA UNAVYOONA HAPO AMBAYE NDIYO MZANZIBAR MAKINI NA KAMILI SIYO WEWE bwege!!!
Mzanzibar uliyepinda anony wa 3 juu Thu Feb 07, 11:41:00 pm 2013
ReplyDelete..HIVI VITAMBULISHO WATAFIKIRIWA HATA MADIASPORA MLIOKUWA WOTE HUKO MAJUU NA WEWE LAKINI KWA MASHARITI YA KUWA NA NIA NJE NA KUSHIRIKI KTK KUIJENGA ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA'' NA SIO KUIBOMOA KWA KUFIKIRIA KUUVUNJA MUUNGANO KAMA NIA YAKO ILIVYO!
licha ya hilo, wewe sifa za kupata Kitambulisho hiki huna, na hicho cha Uzanzibar Ukazi sio cha UTAIFA ni cha UKAZI, zaidi ya hapo kwa sasa Kimebaki kama KADI YA UANACHAMA WA ASP AMBAYO HAIFANYI KAZI, ULIKIPATA WAKATI ULIPOKUWA HUJAONDOKA TANZANIA NA KWA VILE UMESHAPATA UKIMBIZI NJE HAKIPO VALID TENA,,,
Mzanzibar wa tatu (3)
ReplyDelete1.Usipopata Kitambulisho hicho cha Utaifa hutopiga Kura Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015!
2.Hicho Kitambulisho ulicho nacho cha Uzanzibar ni Kitambulisho cha Ukazi na sio cha Utaifa.
Kama unavyomwona Maalim Sheikh Seif Shariff Hamad amesha chukua cha kwake kwa sababu yeye ni mwelewa ZAIDI KULIKO WEWE na anafahamu ya kuwa bila hicho huwezi kupiga KURA!
Msimcheleweshe bwege Mzanzibar,
ReplyDeleteWewe Bwege wa Zanzibar anony wa tatu hapo juu Thu Feb 07, 11:41:00 pm 2013
Hapo unapotumia haya maoni kwa Michuzi unatumia Computer fungua katika google serach ingiza maneno haya kwa wakati tofauti:
-list of countries of the World
-list of nations of the world
-country of zanzibar
-nation of zanzibar
HAPO NI WAZI NO.1 NA NO.2 HUWEZI KUKUTA ZANZIBAR KATIKA LIST HIYO YA NCHI NA MATAIFA YA DUNIA...(labda utumie computer ya asilia ambayo ni mtungi wa maji, au sinia la maji)
PIA UKIINGIZA ZANZIBAR KAMA NCHI AU TAIFA UTAIKUTA NDANI YA ''THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA''
Thu Feb 07, 11:41:00 pm 2013
ReplyDeleteMzanzibar mnaokataa Muungano mjiorodheshe majina yenu wote tukikamilisha utoaji Vitambulisho vya Taifa tutawajaza kwenye Boti na kuwamwaga kwenye visiwa visivyo na watu Bahari ya Hindi mkaishi huko!
Mzanzibar anony Thu Feb 07, 11:41:00 pm 2013 kama Hutaki Kitambulisho KUNYA basi tuone kweli ya kuwa dhati unapinga Muungano!
ReplyDeleteMadrassa gani umesomea wewe?
ReplyDeleteRudi Maadrassa ukasome, bado hujaelimika!
Mzanzibar wa 3 juu anony Thu Feb 07, 11:41:00 pm 2013 wenzio wamesoma wameelimika lakini wewe unetoka kapa.
Wazanzibar waelewa waliosoma wakaelimika katika Madrassa hizo hizo ulizosomea wewe ambao sasa ni Masheikh wanapanga foleni kuandikisha Vitambulisho vya Uraia wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa kuwa ''HAKUNA NCHI INAYOITWA ZANZIBAR''...UTAKALIA KUTI KAVU!
du wadau wa leo mbogo ila mmenifurahisha saaaaaana ila huyo mzenji kachemka.
ReplyDeleteelimu ni kitu muhimu sana katika maisha hao wanaolalamika kuwa watabeba vitambulisho vingapi maana kuna cha bima cha kura nk
ReplyDeletehuku ughaibuni tunabebba zaidi ya vitambulisho 10 ukiachilia mbali na kadi za kawaida kama kadi za punguzo la bei madukani ukijumlisha unaweza kuwa na kadi hata 30
chukua pochi lako weka vitambulisho vyako muhimu na vingine wacha nyumbani.
Wewe Mzanzibar anony Thu Feb 07, 11:41:00 pm 2013
ReplyDeleteMuungano (NDOA) imefanyika mwaka 1964 mtoto JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA akazaliwa.
Mtoto JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ,huku wazazi wake wakiwa wanaishi wa furaha , mtoto amekuwa mtu mzima wa miaka 49 akiwa na afya bora sasa na amejaaliwa UTAJIRI wa mali lukuki kama hizo hapo chini na maeneo yake:
-ALMASI,Mwadui Shinyanga.
-DHAHABU,Nchi nzima.
-CHUMA,Liganga Songea.
-KAHAWA,Kilimanjaro,Kagera,Ruvuma.
-KARAFUU,Unguja na Pemba.
-HISTORIA YA KALE,Nchi nzima.
-MALI ASILI NA MISITU,Nchi nzima.
-ARDHI YENYE RUTUBA, Nchi nzima.
-MAKAA YA MAWE,Songwe,Kiwira Mbeya
-URANIUM,Songea na Singida.
-MAFUTA, Baharini yote na Pemba.
-GESI,Baharini,Lindi an Mtwara.
-BATI NGUMU/ NICKEL, Ruvuma.
-MANGANESE,Ruvuma.
...Na utitiri wa mali zingine nyingi tu!
Sasa wewe ndugu wa Ukoo (Mzanzibari mjinga) unataka NDOA ya wazazi ivunjike ili mtoto awe na jukumu la kuhudumia wazazi waliotengana, je Wewe Mzanzibari mjinga unafikiri USTAWI WA JAMII (UMOJA WA MATAIFA) watakubali kuivunja ndoa bila hoja za msingi?
Mdau wa Zanzibar wa 3 anony Thu Feb 07, 11:41:00 pm 2013
ReplyDeleteHicho Kitambulisho cha Uzanzibar ulichokuwa nacho ni SAWA NA KADI LA KLINIKI LA KUZALIWA, tena afadhali Kadi la Kliniki lina Viwango.
Hivyo Vitambulisho vya Zenj hata Ubora wa Viwango vya Kimataifa havina vipo local.
La muhimu kinaonyesha wewe umezaliwa huko Mchamba wima Zanzibar hilo ndilo la muhimu.
KWA VILE NI WAZI ZANZIBAR SIO NCHI, NI SEHEMI YA NCHI YA TANZANIA.
Kama unabisha ukiwa Bongo Tanzania nenda Ofisi yeyote ya Ubalozi ukaulize kama Zanzibar ni nchi uone majibu ya Wazungu,,,hiyo haitoshi kama upo ukimbizini kwako Majuu au kama unabeba Maboksi (ingawa itakuwa ni vigumu MBEBA MABOXI kufanya hivyo kwa kuwa hadi sasa unaishi nje ya Sheria Huko Majuu) kaulize kwenye WIZARA YA MAMBO YA NJE HUKO ULIKO KAMA ZANZIBAR NI NCHI AU NINI USIKIE!
HIYO HATA UKIWA MUSCAT-OMAN WAULIZE WAARABU WATAKWAMBIA ZANZIBAR SIO NCHI BALI NI SEHEMU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
''MAKAME'' UPO HAPO?
Naona jamaa mnamshambulia bure jamaa wa Zanzibar lakini ana point. Siyo kwa vile jamaa wa Bara hapa mpoo kibao kutoa maoni katika kumpinga, ndiyo kusema mko sahihi, la hasha! Watu wanaojua Demokrasia ya kweli watakwambia, kwa Demokrasia ya kweli kutimia lazima maoni ya wachache nayo yasikike. Ndiyo maana hata Taifa kama la Marekani, kwenye Bunge lao ingawa Democrati walishinda uchaguzi lakini hakiwezi kupitishwa kitu mpaka Wabunge wa Republicani wasikike. Siyo kosa la jamaa kuwa na kitambulisho, ni Taifa lenyewe ndiyo wababaishaji, kwa nini jamaa alipie mala mbili au hangaike kupata ktambulisho kingine wakati anacho cha Zanzibar tayari? Na hapo hapo tunazungumzia Passpoti, kama inasema wewe ni raia wa Tanzania ni lazima mtu upate kibali kingine kama si usumbufu? Na wale wanaopiga kelele eti haiwezekani kujitenga, mbona Zanzibar wana serikali yao? Vile vile wana timu ya Taifa ya mpira, (Zanzibar Heroes) ambao waliwafunga wa Tanganyika?(NASEMA MAPEMA FUNGUKENI, LETENI KELELE ZENU, MAANA JAMAA MKISHINDWA MJADALA MNAANZA KELELE NA MATUSI) Nakuomba ubanie Mithupu.
ReplyDeleteNani kasema Duniani kuna DEMOKRASIA ya 3% KWA 97%?
ReplyDeleteHata kama itakuwa 51% kwa 49%,
Akizidiwa 2% Mzanzibari hawezi kupewa, Hiyo hata Marekani hakuna!
Wewe Mdau wa 27 anony Fri Feb 08, 03:39:00 pm 2013 unayemtetea Bwege Mzanzibari.
unaye muunga mkono mtoa Maoni wa 3 juu HAO JAMAA VISWANI WAPO JUMLA HAWAZIDI 5 Mil., wakati sisi Bara tupo 40 Mil. (jumla Tanzania tupo 45 Mil.)
Hakuna Demokrasia ya kuwabana watu 40 Mil. na kuwapa watu wa 5 Mil.!
Kwanza hiyo hiyo 5 wamegawanyika wengine Wazaznivari wenzao hawataki kabisa kusikia neno KUVUNJA MUUNGANO!
Hivyo hoja zake za Kukataa Kitambulisho ni Itikadi ya Kukataa Muungano.
Huyo Bwege Mzanzibar No.3 hapo juu anayekataa Kitambulisho cha Utaifa wala hayupo mbali!'
ReplyDeleteYupo Dar Es Salaam, maeneo ya ILALA pale panapoitwa hakuna kulala, YUPO KWENYE GENGE LAKE LA UROJO NA LAPTOP YAKE ANAMENYA VITUNGUU NA KUKOROGA UROJO AKIUZA NA VIKACHOLI.
Halafu ndiye huyo huyo anakataa Kuitwa Mtanzania, hataki Muungano, hataki Kitambulisho cha Utaifa!
Kama hamuamini chukueni link yake mtazame IP address zake kwenye maoni yake kwa wale watu wa IT mtaweza kungiza ktk Google map search mtaweza kumrusha humu Jamvini akionekana live!
Mnabisha ?
Bwana MICHUZI tunakushakuru sana na baada yahayo mimi napenda kuwajuilisha wadau inaonekana wamekasirika sana na mdau MZANZIBARI kwanza wameweza kumuita kila aina ya majina lakini kiukweli ni hivi kama ZANZIBAR sio nchi jee timu ya Taifa star ilitolewa na timu gani katika mashindano ya chalenge cup kama sio ZANZIBAR HERO na kama wadau wanabisha mbona hatukuona timu ya MTWARA STAR wala IRINGA STAR. Pili tunapozungumzia nchi wanaosema tuangalie kwenye google kama kuna nchi inayoitwa ZANZIBAR jibu lake ni hili nawaomba wadau wenye akili waangalie kwenye kamusi neno UNITED lina maana gani kwa sababu mimi nahisi neno hilo linawakilisha kitu zaidi ya kimoja ,tusiongee tu kwa hasira au chuki fulani au kwa mapenzi fulani ukweli utabaki kuwa ukweli kama zanziba sio nchi neno UNITED REP OF TANZANIA lisingepatikana na hata ukiangalia nchi za wenzetu kama vile UK ,ukienda SCOTLAND ni nchi tofauti wana bunge lao wana bendera yao wana mpaka paund yao ya kiscotish na hata baadhi ya sheria pia ni tofauti na zinazotumika England,ukienda WELS nihivyo hivyo lakini kuna mambo tuu ambayo nduyo wameungana na ndio ikapatikana UK lakini ni nchi tofauti,na ZANZIBAR pia ni nchi tofauti kwa vigezo hivyo kama tunapenda au hatupendi wana Rais wao ,Bendera yao ,Bunge lao ambalo ndio BLW. Wana Katiba yao na sheria zao jee ARUHA au KIGOMA na wao wanayo hayo. Mfano mzuzi juzi tuu mheshimiwa mmoja wa CHADEMA aliyasema yote hayo na mwisho pia akaeleza pia WAZANZIBARI wanatushangaa sana sisi na akasema ni lazima turejeshe Tanganyika yetu jee na chadema pia hawana akili.Jengine unaposema hata MH.SEIF.SHARIFF. ameshachukuwa kitambulisho cha mtanzania kwa hiyo huyo mdau yeye hana akili tukumbuke pia SEIF.SHARIFF. hawiwakilishi Zanziba nzima yeye ni mtu kama binaadamu wengine tuu hiyo mifano isio na kichwa wala miguu haifai . Mimi nahisi tusimuandame mdau na kumshambulia bure mdau ana points alichoongea ni ukweli kama tunapenda ua hatupendi huo ndio ukweli na wala mdau hakupinga muungano alichoongea ni kweli huu sio wakati wakudanganyana tena ,ukiangalia tuu SCOTLAND juzi tuu wamesema hawataki kuwa tena na UK na wameshaabiwa mwaka wa 2014 watapiga kura ya maoni kama wanataka au laa. Nakushukuru sana BWANA MICHUZI .Tusiongee tuu kwa hasira ila tuangalie na points.
ReplyDeleteMdau Anonymous wa #Fri Feb 08, 07:53:00 pm 2013: Soma tena maana ya Demokrasia. Siyo unavodhani kwamba tukiwa wengi ndiyo kila kitu kinakwenda tunavyotaka siye(Majority), ni lazima wachache(Minority)nao wasikilizwe. Ndiyo ilivyo Marekani. Sasa we jamaa yangu sijui Marekani ghani unaiongelea!!?(Usipotoshe umma). Narudia tena, ingawa Democracts walishinda uraisi kwa wingi, lakini Rais Obama hawezi kupitisha sheria au bajeti bila ya kupata idhini ya Republicans. Ndiyo maana waafrica wengi wanadhani Obama, kwa vile rais, anaweza kutoa amri au misaada kwa Waafrika kama wanavyofanya viongozi wakiafrika. Ni lazima kitu chochote kipitshwe na Senate/Congress kwa sababu maamuzi yana wapa faida au shida wote.
ReplyDeleteNa Anonymous wa #Fri Feb 08, 08:01:00 pm 2013, "MIE NABISHA". Ubabe, uonevu, vitisho, kuvunja haki za wenzako si sahihi. Haki isipopatikana shemu basi zote zinakosa haki.
Kusema kweli ukweli na mie sipendi muungano uvunjike bali naona kuna sauti kibao za huko jamaa wanataka wajitengee, ni sahihi wasikilizwe. Na jamaa mnaosema kwamba hawa jamaa lazima watakuwa Ughaibuni ndiyo maana wanaongea hivyo, basi hapo inaonyesha jinsi wanavyoonewa maana wanaogpa hata kuongea wakiwa kwao kwa sababu labda ya visasi. Je sasa haki yao iko wapi? Mnasema Democrasia, wapi?
Mie ndiye Anonymous wa #Fri Feb 08, 03:39:00 pm 2013
Ninyi WAZANZIBAR wawili watowa Maoni wa No.30 (Fri Feb 08, 10:22:00 pm 2013) na wa No.31(Fri Feb 08, 11:21:00 pm 2013)
ReplyDeleteHata kama kuna MAJORITY na MINORITY, hatukatai!
Isipokuwa ninyi mnaodai ni MINORITY mnataka kulazimisha MAJORITY ikubali matakwa yenu hiyo haiwezekani!, isipokuwa KUSIKILIZWA MTASIKILIZWA,
LAKINI DAIMA HAKUNA DEMOKRASIA YA MINORITY KUILAZIMISHA MAJORITY KATIKA MAAZIMIO.
KWA KUWA DEMOKRASIA INAKAMILIKA KWA VOTING NA % INAAMUA MOJA KWA MOJA MINORITY MNAKUWA MMESHINDWA NA MAJORITY!!!
MFANO TANZANIA NZIMA TUPO 45 Mil. ,yaani BARA NI 40 Mil. na VISIWANI NI CHINI YA 5 Mil.
TENA HUKO VISIWANI HIYO 5 Mil. ZIKIPIGWA KURA NI WAZI UTAKUWA WANAOTAKA UJINGA HUO WA KUVUNJWA MUUNGANO NI WATU LAKI MBILI TU (200,000) HUKU WENGINE ZAIDI YA 4,800,000 (4.8 Mil) WAKIWA WANAUNGA MKONO MUUNGANO.
HIVYO KABLA HAMJAFIKA BARA HUKO HUKO ZANZIBAR MMESHAKUWA MINORITY KWA KUWA HATUWEZI KUWAPA WATU LAKI MBILI (200,000) TUKAWABANA WATU (4,800,000).
WAZANZIBAR WASIOTAKA MUUNGANO HAWAZIDI 200,000 (4%) NA WANAOTAKA MUUNGANO 4,800,000(96%) SASA HAPO HAPO TAYARI HUKO HUKO VISIWANI WAPINGA MUUNGANO MMESHAKUWA ''MINORITY'' KWA SABABU HATUWEZI KUWABANA WANA MAPINDUZI 96% TUKAWAPA WAVUNJA MUUNGANO 4%!!!
MKIJA BARA HIYO MINORITY YENU NDIO INAZIDI KUZAMA KABISA KWA KKUWA TUTACHUKUA 200,000 GAWA 45,000,000 MARA 100=0.4% !
SASA PERCENTAGE INAZIDI KUZAMA KUTOKA 4% HADI 0.4% !!!MARA 10 ZAIDI!
HIVYO MINORITY YA 0.4% (WAPINGA MUUNGANO) HAIWEZI KUPEWA WAKABANWA (99.4%) DUNIANI HAKUNA DEMOKRASIA KAMA HIYO, HATA MAREKANI UNAKODAI HAWAWEZE WAPA MINORITY AMBAO NI 0.4%!!!
MPO HAPO?
Wazanzibar na Upinzani wenu mkitumia Demikrasia ni kuwa DEMOKRASIA hailazimishwi,
ReplyDeleteMara zote VOTING ndio mwamuzi wa mwisho na mara zote ktk voting mnaopinga Muungano mnashindwa ndio maana hata UN haiwapi uzito madai yenu!
Wazanzibari wa No.30 na No.31 mmeona Kisomo hicho cha Dakitari wa Siasa za Demokrasia No.32?
ReplyDeleteKazi kwenu mzi print data na Maoni hayo muwapelekee Ofisi za Uamsho mkajadiliane, kama ni kuvunja Kundi au mbadili mwelekeo na kuwa Chama cha Wavuvi badala ya Siasa za ku-fosi!
Mfano rahisi wa Demokrasia ni KATIKA UBWABWA WA HITIMA.
ReplyDeleteMNASOMA HITIMA, MNAMALIZA MNASIKIA FATIHAAA DUA UNASOMWA, MARA MNASIKIA WAANDAZI WAANDAZI PANGENI WATU!
MNASIKIA HAYA WANNE WANNE, MNAKAA MARA MNASIKIA KAENI NANE NANE AU KUMI KUMI KWA KUWA MASINIA HAYATOSHI CHAKULA KIDOGO.
KWENYE SINIA MOJA LA WATU WANNE INATOKEA MMOJA ANATAKA UBWABWA UWEKWE PILIPILI WAKATI WATATU WANASEMA USIWEKWE!,,,JE ITAKUWA NI HAKI MMOJA KALAZIMISHA UBWABWA UWEKWE PILIPILI NA KUWABANA MATAKWA YA WATU WATATU?
AU KWENYE SINIA LA WATU 10 WAWILI WAKITAKA UBWABWA UWEKWE PILIPILI ITAKUWA SAWA NA KUWAKATALIA WATU 8 ?
HATA KWENYE MASINIA YA KULA UBWABWA DEMOKRASIA YA 'MINORITY' INAKATAA!
IKITOKEA IKAWA 49% KWA 51% WANAPEWA WENYE 51%.
DEMOKRASIA ZENU ZA UKIMBIZINI HUKO HUKO KWENYE KUBEBA MABOKSI wewe anony wa UK wa Fri Feb 08, 10:22:00 pm 2013
ReplyDelete...Scotland wanadai wapige Kura za Maoni mwaka 2014, hizo ni Demokrasia za akina David Cameron na SERA ZAKE ZA SIASA ZA (KIU..S3...NGE) na KAMWE hazikidhi mahitaji ya Demokrasia za Ki-Afrika na Tanzania !
Utitiri wa MINORITIES za migawanyiko katika kutimiza mahitaji ya demokrasia ATAPEWA NANI AACHWE NANI?
Mfano hao jamaa Visiwani ambao hawazidi 10% ya Watanzania wote ambao wao ni MINORITY wakidai wapewe, halafu itokee wengine 3% wadai mahitaji yao nao pia wapewe.
Hapo MAJORITY inazidi kuminywa na kubanwa, kwa MTAJI wa kuitimiza DEMOKRASIA.
Sasa tutafikaje kwa UTITIRI HUO WA MIGAO YA MAHITAJI NA KUTAKA AMA KULAZIMISHA KUTIMIZIWA?
DEMOKRASIA ZA KUGAWA KAMA NJUGU HATUZIWEZI TANZANIA!
ReplyDeleteMdau wa 30 anony wa Fri Feb 08, 10:22:00 pm 2013, mgawanyo wa kila MINORITY ipate Madai yake itashindikana Tanzania.
Hata huko huko Scotland sio rahisi wakubali hicho kitu ingawa ni wazi wachache sana watataka kujitenga isipokuwa kwa Malengo ya KIUCHUMI wengi watataka kubakia ktk UK.
Maana Uchumi umeyumba Dunia nzima ikiwemo hiyo hiyo UK, hadi Mabosi wakaamua kushusha thamani ya POUND ili kasi ya kupanda gharama za maisha ishuke ukilinganisha na nchi zingine Duniani, pia USWISI imeipunyua Sarafu yake SWISS FRANC ili kupunguza kasi ya kupanda gharama za maisha na kuwa na ushindani na Miji mingine na nchi zingine Duniani ktk masoko ya Hisa na uwekezaji wa Mijini.
Watu huwa wanatapa tapa Kisiasa lakini wakitafakari ki-Uchumi wanajikuta wanauhitaji Muungano ili kuakisi UKUZAJI WA KIUCHUMI (Economic growth),kitu ambacho Wapinga Muungano hawakifikirii.
WAKIDHANI LABDA KUUVUNJA MUUNGANO NDIO SULUHISHO LA UGUMU WA MAISHA YAO NA SULUHISHO LA HALI YA KIUCHUMI, KUMBE NI KUNYUME CHAKE YA KUWA WANAHITAJI KUDUMU KATIKA MUUNGANO ILI KUAKISI UKUZAJI WA KIUCHUMI NA MARA ZOTE UMOJA WA KIUCHUMU NDIO JIBU SAHIHI LA MAENDELEO YA KIUCHUMI BADALA YA UTENGANO.
SIASA HUTAKA ZAIDI NA KUSHAWISHI UTENGANO HUKU IKIDANGANYA YA KUWA NDIO NJIA ZA KUIMARISHA HALI YA MAISHA YA WANANCHI, WAKATI UCHUMI HUSHAWISHI ZAIDI MUUNGANO WA KIUCHUMI NA KISIASA KAMA SULUHISHO LA MATATIZO YA KIUCHUMI NA KISIASA.
SASA WAZANZIBARI WAMEGAWANYIKA KWA KUWA VIONGOZI WANAJUA THAMANI ZA KISIASA NA KIUCHUMI ZA MUUNGANO, WAKATI WENZANGU NA MIMI AKINA ZAYUMBA WAO WANADHANI KUVUNJA MUUNGANO NDIO JIBU LA SHIDA ZA KIUCHUMI, KUMBE SIVYO...KAMA WANAVYOKATAA VITAMBULISHO VYA UTAIFA.
Wazanzibari mnazisahau saaana NEEMA KIBAO ZA MUUNGANO!
ReplyDeleteHebu kumbukeni kwenu hampati neema hizi hapa:
Tunajua wazi sawa Zenj wenzetu ni Ma Alhajj wazuri sana kuliko huku Mrima (Bara), lakini wengi mnapata mahitaji ya ziada kama!
1.GANJA, Ni wazi Wazenj ni Ma-Rasta wazuri sana na wafuasi wa MARLEY wazuri tu!, kule Visiwani Sheria ni kali mno kwenye Ulevi, majani mnapata kwa kujificha sana (TENA MNAVUTIA VYOONI AMA USIKU SAAANA) tofauti na Bara mnavuta KWENYE MASKANI tena mkiwa huru kabisa!
Tena mnapata mazao ya kutoka Mikoa tofauti kwa ubora, tofauti na manyasi ya kwenu sio makali kabisa!
Mfano,
-Kijiti cha Mboka,(Tabora)
-Majani ya Meru,Arusha na Machame,Moshi
-Majani ya Newala,Mtawara
-Manyasi ya Mbeya na Iringa
-Manyasi ya Wagosi wa kaya,Mombo na Lushoto (KALI BALAA, UKIFANYA MCHEZO UNAFUNGWA KAMBA KWA KICHAA)
2.GONGO, wengi ndio ni Waumini lakini Glasi mnapiga japo kwa siri!,,,neema hii mnaipatia Bara tu!
3.Akina dada wa Usiku, kule Zenj ni kimtindo sana (BAIBUI NA SHUNGI KIBAO) wakati Bara SURUALI NYINGIII, WENYE MNALIJUA HILI na biashara ni huria fedha zako.
Hivyo hizo NEEMA 3 juu kwa Mzanzibari mwenye akili ni lazima adumishe na kuuthamini Muungano!
LOHHH, MPEWE NINI TENA ZAIDI YA HAPO KWENYE MUUNGANO?
Mdau wa 30 Unayesema kuhusu Scotland kutaka kujitenga + Mdau wa 31 unaesema kuhusu Demokrasia za MINORITY na MAJORITY.
ReplyDeleteHebu angalieni, Tanzaia ina Mikoa kama 40 hivi au zaidi na kila Mkoa una Wilaya zaidi ya 3 !
Sasa nchi nzima itakuwa na Wilaya 40x3=120 au zaidi, sasa hiyo Zanzibar na Pemba yenu ni kama WILAYA MBILI (2),
HEBU SEMENI TUTATOA MINOIRITY RIGHTS KWA WILAYA ZOTE ZAIDI YA 120+ ZA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA?
SI UTAKUWA UTAAHIRA HUO?
DEMOKRASIA GANI YA UYOGA KWA KILA WILAYA KUPEWA INACHOTAKA?
THINK TWICE!!!
Muungano hauvunjiki ng'o !!!
ReplyDeleteKwa kweli ukivunjika mimi Maganga wa Bara ''nitacheka kwa masikio na sio mdomo''!
ili kuthibitisha muujiza mkubwa!
MUUNGANO DAIMA MAPINDIUZI DAIMA!
ZAIDI YA HAPO HATUWEZI KUWAANGUSHA WANAMAPINDUZI AMBAO NI WANA C.C.M WA KWELI!
KWA KWELI WANAMAPINDUZI ZANZIBAR NINAWAKUBALI SAAANA MAKOMREDI HAWA WAKO VIZURI KTK MSIMAMO WA KISIASA!
Mnaokataa Vitambulisho vya Utaifa mtakuwa Stateless persons, yaani mtakuwa kama baadhi ya Raia wa ISRAEL waliokuwa nchi za Ulaya wakati wa vita kuu ya Pili ya Dunia.
ReplyDeleteMfano kama na nchi walizokaa na Walikoelekea,
-Albert Einstein:Swiss-USA
-Enrico Fermi:Italy-USA
-Yehuda Cohen:France-Canada
-Golda Merril:England-South Africa
-Dani Yoni:Sweden:USA
Hao walikaa miaka kadhaa wakiwa hawana Utaifa hadi walipokwenda nchi za Uhamishoni, sasa ninyi Stateless wa Zanzibar mtakuwa mnajitakia wenyewe kwa ubwege wenu.
Mie Mdau nayemsupport Mzanzibar, lakini natoka Tanganyika. Sasa naona nashindwa kucopy na kupaste yaliyosemwa na wengine kwa vile tuko wengi mno na inaonyesha jinsi mjadala ulivyom muhimu.
ReplyDeleteKusema kweli, siwalewei jamaa wanaosema haiwezakani kwa Zanzibar kujitenga ni kichekesho, kwani jamaa hawaoni mataifa yote yaliyojitenga ulimwenguni? Vile vile nimeuliza maswali kibao kwenye maoni yangu naona hamna majibu, Kwafano, Mbona 1).Zanzibari wana timu yao ya Taifa na walitufunga Taifa Stars? 2).Mbona wana serikali yao? 3).Kwa nini paspoti inayojulikana dunia kama utambulisho wa raia wa mtu isitumike kama kitambulisho? Halafu mnaosema Wanzibar wako wachache wanaongea hayo, si kweli, kwani nakumbuka kipindi fulani CUF na watu wa visiwani walikuwa wanapigwa mabomu kwa kuongelea ili swala la kujitenga wakati wa uchaguzi. Sasa naamini kweli lazima ZNZ kuna kuna kitu, gesi au mafuta, maana jamaa wa Bongo mme wanga'nga'nia mno. Kwa sababu hata kama watu walikuwa wachumba, hakakukataa, unalazimisha, kweli hayo ni mapenzi(kwa vile wewe una nguvu-Majority)!!?? Na siye wabongo ni mdomo tu,tunabisha sana, lakini inabidi tusome nyalaka za nyakati. Nakumbuka hata wakati wa kuanzisha vyama vingi watu walikuwa wanapinga, lakini CCM ilipolzimishwa na mataifa ya Magharibi, ikawezakana.
Na mdau wa#Sat Feb 09, 10:22:00 am 2013.
Naona uana miss point, Kuwa majority au minority siyo lazima kundi fulani wawe wengi au kidogo. Inategemeana. Kwa swala ili naona Wanzazibar wenyewe ndiyo walipigie kura, siyo siye wa Tanaganyika. Mfano mzuri utakuwa, kama Afrika kusini wakati wa Apartheid wazungu walikuwa Majority(ingawa wa chache kinamba) kwa vile walikuwa walikuwa na nguvu. Na vile vile Marekani, watu weusi enzi za kufuta utumwa, wangekuwa majority wenyewe(wazungu) bila kufanya busara tungekuwa bado siye watumwa. Na mpaka leo hii kwenye katiba ya Marekani kuna sheria za kuwalinda weusi, zinaitwa Civil rights amendments. Ndiyo maana utaona wanatenga hata nafasi za shule kwa weusi kwa vile wanajua hawana uwezo fulani kuingia hapo.
Wapinga Muungano na Balozi wenu anony wa Sat Feb 09, 09:08:00 pm 2013
ReplyDeleteMsipoteze muda bure kwa kukataa kuchukua Vitambulisho vya Utaifa ni vile mtakali kuti kavu.
1.Ni wazi madai ya kuuvunja Muungano hayana baraka za UN, hayakubaliki wala Shirikisho hali halitilii uzito sual lenu.
2.Kama kuuvunja Muungano kungekuwa sahihi tokea meanze kelele zenu Muungano ungeshavunjika.
3.Dunia inatafuta Kuungana wakati ili kupata maedneleo na ufanisi wa Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii huku inakwenda Karne ya 21 ninyi mnarudi Karne ya 12, tazameni TUNAVYOELEKEA KWENYE MAFANIKIO TUKIWA KTK JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI (EAC), huku wajanja kama SUDAN, SUDAN YA KUSINI NA SOMALIA NDIO KWANZA WANAOMBA KUINGIA EAC NINYI MNA MAWAZO FINYU MNAWAZA KUJITENGA!
4.MSITUMIE MGONGO WA DEMOKRASIA ZA MINORITY ILI KUFIKIA MALENGO YA KISIASA, DUNIA IPO MAKINI NA MAMBO HAMTAFANIKIWA.
5.MTAJIWEKA KWENYE TABU KWA KUKATAA UTARATIBU WA KIRAIA UTAKAO WANYIMA HUDUMA ZA JAMII NA UTAWALA HADI KUKOSA KUPIGA KURA. KWA KUWA
Ni vile mkitazama nukuu hizo (5) tano hapo juu, moja kwa moha ni wazi ya kuwa HAKUNA UWEZEKANO KWA MUUNGANO KUVUNJIKA, MSIPOTEZE MUDA WENU BURE!!!
Mimi Maganga naomba Muungano usivunjike niongeze mke wa 3 wa Ki-Zanzibari!
ReplyDelete-Ningeijua vipi pilau ya samaki wa mchuzi wa nazi, mimi mtu wa Tabora mla ugali wa Dona la mtama kwa majani ya viazi, na mla matogolwa (viazi vikavu) kwa maziwa ya mtindi bila wake wa Kisiwani?
-Ningejua vipi kama chai inaweza kuwekwa viungo vya pilau kama nisingekuwa na wake wa visiwani?
-Ningelijua vipi kama chai ya maziwa inaweza kunywewa na samaki badala ya maandazi na mikate, mimi mtu wa Tabora ninae kunywa Togwa la mtama kama sikuwa na wake zangu wawili wa kisiwani?
-Ningeijua vipi Biriani ya mbuzi mimi mwana Tabora wa bara, kama sikuwa na wake wawili wa kisiwani?
-Ningejua vipi kuvaa msuli kiunoni,wakati wa joto la pwani mimi mtu wa bara kama sikuwa na wake wa kisiwani?
Ohhh naongeza mke wa 3 kutoka Zanzibar mwezi Shaaban kabla ya Ramadhani!
Ahhh, jamani Muungano mtamu!
Mkuu Mdau wa Mon Feb 11, 10:09:00 am 2013
ReplyDeletePoint zako hazina point, je Historia inasemaje?
1.kwanza sie wenyewe Waswahili tunasema "lisemwalo lipo na kam halipo linakuja".
2. Unaongelea UN ambao hivi karibuni wamewatambua wa Palestina. Kwanza wewe kama mwanafunzi wa Historia na Siasa utajua ya kwamba UN ni Marekani, UK, Ufaransa, China, na Urusi wakiamua wao kitu basi ni hivyo.
3.Labda sielewi ya kwamba Sudan inataka kujiunga na EAC lakini siye WaTanzania si tunaukataa umoja huo au?!! Halafu sijui unasema nini, kwani hujui Sudani imetoka kugawanyika hivi karibuni?
4.Hamna serikali isiyoendeshwa kisiasa-kila mtu ana haki yake ya msingi, ndiyo kitu muhimu. Kuwanyima wengine kuongea mawazo yao ni kuwanyima haki yao ya msingi.
Swali lako la tano nimelijibu katika swali lako la nne.
Ongea kwa vitisho lakini muda ndio msema kweli.
Mda wa Zenji wa 46 anony Mon Feb 11, 03:30:00 pm 2013
ReplyDeleteWewe chukua nyavu ukavue samaki maji marefu Ras-Nungwi...Muungano hauvunjiki NG'OOO!, utajisumbua bureee na kupoteza muda wako!
''LISEMWALO LAJA KAMA HALIPO LINAKUJA''=====
MIMI NAKUJIBU:
''USILOLIJUA DAIMA LITAKUSUMBUA''==== HUIJUI SIRI YA MUUNGANO WEWE!.
Inaonekana wewe wakati wa Mapinduzi 1964 hukuwepo Visiwani Zanzibar na pia wakati wa Muungano hukuwepo (ULIKUWA OMANI) ndio maana SIRI YA MUUNGANO HUIJUI.
Usitoe hoja bila kufuatilia maendeleo ya mambo ya Dunia, inaonyesha ni jinsi gani ulivyo kuwa mweupe Kimataifa:SUDAN KUSINI IMEJITENGA NA KUPATA UHURU MWAKA 2011 LAKINI SUDAN ZOTE ZIMESHA OMBA KUINGIA AFRIKA YA MASHARIKI:
======================================================================
-SUDAN (Khartoum) NA SUDAN KUSINI (Jubba) ZITAUNGANA TENA KAMA ZOTE ZITAINGIA KTK AFRIKA YA MASHARIKI (EAC) KWA SABABU ZOTE ZIMESHAOMBA KUJIUNGA NA EAC...UNALIJUA HILI?
MAANA YA AFRIKA YA MASHARIKI (EAC) NI MUUNGANO WA SERIKALI ZA NCHI WANACHAMA AMBAPO MAMBO YOTE YA KISERIKALI YATAPANGWA NA KUSIMAMIWA KWA UMOJA WA NCHI ZOTE, JE, HAPO SASA HAZITAKUTANA KISERIKALI?
======================================================================
TENA SUDAN ZOTE (2) ZINA KIU BALAA YA KUTAKA KUWEPO KTK SHIRIKISHO LA AFRIKA YA MASHARIKI (EAC).
-HIVYO, WEWE MKAZI WA WILAYA YA ZANZIBAR AMA PEMBA NA MIMI MKAZI WA WILAYA YA ILALA WAKATI NCHI NZIMA ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA'' INA WILAYA ZAIDI YA 120+ HAIWEZEKANI KILA WILAYA IKATOA MATAKWA NA YAKACHUKULIWA KUWA NI DEMOKRASIA NA YAKATEKELEZWA,,,MATEKELEZO YATAKUJA KWA KUTAWALA WA KIUJUMLA KWA NCHI NZIMA KITU AMBACHO MNACHODAI TAYARI SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESHATEKELEZA NA PIA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMESHATIMIZA, HIVYO HATA MKIENDA UN MTAGONGA UKUTA.
-WAPINGA MUUNGANO MSIFIKIRI KUWA KUJITENGA NDIO SULUHISHO LA KUTATUA SHIDA ZA KIMAISHA, MTAJITENGA SHIDA ZITABAKI PALE PALE TENA INAWEZEKANA NDIO ZITAZIDI. (MKUMBUKE YA KUWA SHIDA ZA NCHI ZINATATULIWA NA UMOJA WA NCHI) KAMA WALIVYOFANYA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA NA ILIVYO MAMLAKA YA MAJIMBO YA MAREKANI, NA JINSI ILIVYO AFRIKA YA MASHARIKI.
-----------------------------------
Hivyo wenye akili daima huungana na sio kutengana, mfano hao Sudan na Sudan Kusini, watajikuta tena wamekutana ktk Serikali ya UMOJA WA AFRIKA YA MASHARIKI (EAC),,,UPO HAPO?....NA HII MAANA YEKE NI KUWA MATATIZO YA NCHI YANATATULIWA NA UMOJA WA MUUNGANO WA NCHI ULIOIMARIKA NA SIO UTENGANO, umeonamwenyewe Mfano huu wa nchi za Sudan
-----------------------------------
INAONEKANA MZANZIBAR NA WAFUASI WAKO MPO WEUPE SANA KTK ILMU YA KIUCHUMI NA MAENDELEO YA MATAIFA.
-----------------------------------
HIVYO NI WAZI YA KUWA:
,,,TUTAKUFA MIMI NA WEWE MUUNGANO TUTAUACHA NA NDIO KWANZA UTAZIDI KUIMARIKA ZAIDI KWA IDADI KUBWA YA NCHI ZINGINE KUINGIA, TENA KAMA INGEKUWA MAISHA YANAJIRUDIA BAADA YA KIFO UNGEKUTA HATA ANGOLA NA MSUMBIJI ZIKO ATIKA KAFRIKA YA MASHARIKI!!!
Mzanzibar wa 46 anony Mon Feb 11, 03:30:00 pm 2013
ReplyDelete..Point zako hazina point.
Wewe ni Mkazi wa kati ya Wilaya zaidi ya 120+ za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (JITAMBUE KAMA MKAZI WA WILAYA NA SIO NCHI KAMA UNAVYO JIFIKIRIA WEWE).
NDIO MAANA HAMFANIKIWI KUUVUNJA MUUNGANO KWA KUWA MPO 'MINOIRTY' SANA!
Matakwa ya Wilaya (MOJA au MBILI) hayawezi kusikilizwa yakatekelezeka KTK NCHI, Wilaya zaidi ya 120+ atasikilizwa nani atatekelezewa nani?
MSIFIKIRI UMWINYI WENU UTASAIDIA MPEWE KIPAU MBELE KWA MADAI YENU YA KIJINGA.
Je, Kila Wilaya ya Bara ikidai mahitaji yake ya Kidemokrasia itakuwaje?
SI ITAKUWA NI VURUGU?
Wadau #Mon Feb 11, 05:17:00 pm 2013 na wa #Mon Feb 11, 05:32:00 pm 2013
ReplyDeleteNaona mnachanganya hoja. Muungano wa Sudan walijagwa kama unavyosema wewe ulitokea 2011 ni kweli sasa huo wakuungana tena katika Afrika Mashariki siyo sawa na uliopo.
Halafu na mie sitoki visiwani bali natoka hapo hapo Ilala lakini siwaelewi kwa nini manalazimisha muungano, wamesema hawataki, hawataki!! na ndiyo ilivyokuwa Sudan. Sipendi kutengana lakini nyie jamaa HAWATAKI.
Elimu zenu kubwa lakini mnashindwa kuelewa Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili ndiyo initwa United Republic of Tanzania. Jina lenyewe tunafundishwa ni muungano wa nchi mbili. kwa hiyo sijui habari za kila wilaya au mikoa wakimua hivi au vile ni hoja zilizoshindwa.
Mdau wa 49 wa Zanzibar (Mon Feb 11, 10:54:00 pm 2013) utajisumbua bure hangaika na maisha yako.
ReplyDeleteMNALOLITAKA HALITATIMIA,,,,,,,,,,KUVUNJIKA KWA MUUNGANO NI SAWA NA UWEZEKANO WA INZI KUPENYA KWENYE NDIMI ZA MOTO,,,,,,,,,!
1.WEWE NA WENZAKO MIGONGO WAZI, MNAWAZA UWEZEKANO WA KUUVUNJA MUUNGANO WAKATI HAMFAHAMU NI KWA NINI VIONGOZI WENU WASIUVUNJE MUUNGANO, HEBU JIULIZE TOKEA MUANZE KELELE ZENU MBONA HAMJAFANIKIWA?
2.NI WAZI YA KUWA VINGOZI WENU WANA ELIMU ZAIDI YENU WAVUJA JASHO KWA KUWA WANATAMBUA WAZI YA KUWA
****ZANZIBAR INANUFAIKA ZAIDI NA MUUNGANO KULIKO BARA*****
HII SIRI TAFUTA MUDA UZUNGUMZE NA MHE. MAALIM SEIF ATAKWAMBIA, AU HATA KAMA SIO MOJA KWA MOJA KTK MAEONDEZI YAKE UTAGUNDUA KAMA AKILI YAKO INAFANYA KAZI VIZURI.
-----------------------------------
Hivyo wewe na wenzako msipoteze muda Mhcukue Vitambulisho vya UTANZANIA kwa kuwa ni ndoto kuvunjika kwa Muungano kamamnavyotaka.
Zaidi ya hapo, mtajikuta mnakalia kuti kavu kwa kuwa itafikia mtaishi kama punda au ng'ombe.
NCHI ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA'' INATAKA KUINGIA KTK MFUMO WA DIGITALI HIVYO MTAJIKUTA MKO GIZANI KAMA HAMTAKUWA NA NATIONAL ID's KTK KUFIKIA VITU KAMA HIVI:
-KILA MANUNUZI YATAHITAJI UWE NA NATIONAL ID
-KILA UENDAPO SEHEMU YA HUDUMA ZA KIBIASHARA NA KISERIKALI UTATAKIWA NATIONAL ID.
-KILA SEHEMU WENDAYO LAZIMA UTOKE ID NA IINGIZE KTK COMPUTER KUHAKIKIWA.
***********************************
Jambo lingine litakalo wagharimu zaidi ni kuwa MMEFIKIA MUDA MGUMU ZAIDI WA KUDAI KUUVUNJA MUUNGANO KWA KUWA SASA NCHI IMESHAKUWA TAJIRI NA KADIRI SIKU ZIENDAVYO NDIO UWEZEKANO WENU WA MADAI UNAYEYUKA ZAIDI.
***********************************
NENDENI MKALIME!!!
Mtoa Maoni wa 49 za Zenji:
ReplyDelete...Mategemeo yenu ya KUUVUNJA MUUNGANO...NI SAWA NA TAMAA YA FISI ANAEFIKIRI MKONO WA BINAADAMU ANAYETEMBEA UTAANGUKA ILI AJIPATIE!
NINYI WAPINGA MUUNGANO HAMNA TOFAUTI NA FISI MAJI!
Kweli Mzanzibar na wenzako akili zenu finyu! (Anony wa Mon Feb 11, 10:54:00 pm 2013)
ReplyDelete...ninyi na wewe mnafikiri Serikali ya Umoja na Serikali ya nchi ni Tofauti?
...ninyi na wewe mafikiri Serikali ya Umoja na Serikali ya nchi ipi yenyen nguvu?
KUNA UWEZEKANO MKUBWA SERIKALI KAMA YA EU(EUROPEAN UNION)NA EAST AFRICAN COMMUNITY, SUALA LA URAISI LITAKUWA IN ROTATION BASIS,,,YAANI MARAISI WATAKUWEPO WA NCHI NA RAISI WA UMOJA ATAKUWA ANATEULIWA KWA MZUNGUKO MIONGONI MWA MARAISI WOTE KTK NCHI ZA UMOJA,,,UPO HAPO?
WEWE BWEGE SANA, WALA HUNA ILMU, NADHANI HATA MADRASSA YENYEWE HATI HATI HUKUSOMA!
KWA TAARIFA YAKO SERIKALI YA UMOJA NDIO YENYE NGUVU KIMIPANGO NA MAAMUZI,,KALAGA BAHO!
Wewe Mzanzibar na wenzako mabishano yenu ni ya Kishabiki na sio ya hoja.
ReplyDeleteKAMA MUUNGANO HAUFAI MBONA HAMJAFANIKIWA KUUVUNJA?
MARA ZOTE HOJA YA KUUVUNJA MUUNGANO INATUMIWA NA WANASIASA ILI KUWADANGANYA WAJINGA (WAJINGA NI WOTE WANAO AMINI YA KUWA KUVUNJIKA KWA MUUNGANO NDIO KUIMARIKA KWA MAISHA YAO NA UCHUMI),,,MBONA KAMA KUUVUNJA MUUNGANO NI SERA YA KISISA KWA NINI VYAMA VYA SIASA NA VIONGOZI WA ZANZIBAR WANASHINDWA KUTEKELEZA KUUVUNJA MUUNGANO?...SIO AJABU KABISA HATA WALE WENZENU WA UAMSHO WAKIPATA NAFASI YA UTWAWALA NDIO KWANZA WATADUMISHA MUUNGANO BADALA YA KUUVUNJA!
(MTAKE MSITAKE UWEPO WA MUUNGANO NI SUALA LA KIUCHUMI NA KIJAMII NA SIO LA KISIASA HIVYO HALINA JINSI KWENU)
SIKU ZOTE HIZI MNANGOJA NINI?
Wazanzibar ''WAPINGA MUUNGANO'' msijisumbue nendeni mkatafute maisha kwa kujituma ktk kazi!
ReplyDeleteSUALA LA KUVUNJIKA KWA MUUNGANO NI ''MUHALI'' (NI VIGUMU KWA KISWAHILI CHENU CHA MWAMBAO), TUKIO HILO LA KUVUNJA MUUNGANO HALINA UWEZEKANO KAMA ISIVYOWEZEKANA KITENDO CHA MTU KUJILAWITI MWENYEWE!
Wazanzibar msiumize vichwa vyenu kuona tokea muanze kelele zenu tangu Kipindi cha Abeid Amani Karume mlipoanza kudai (ingawa kichini chini kutokuridhika na Muungano,,,mlikuwa mnaendesha harakati hizi kwa siri kubwa chini ya mabwenyenye wa Kiarabu), hadi sasa lakini mnaona hamfanikiwi, ni kwa nini?
ReplyDelete1.KISIASA:
Mnadai kuuvunja Muungano inakuwa ni wakati wa harakati za Kisiasa, na mara zote hii ni sera inayotumika zaidi ki-Siasa lakini baada ya msimu wa Siasa inadorora au inakufa kabisaaa.
2.KIUCHUMI NA KIJAMII:
Mnapokuja Kiuchumi na Kijamii mnajikuta ni lazima muudumishe Muungano!,,,hakuna jinsi,
-Pana mshabihiano wa Kiuchumi Bara na Visiwani ambao hautenganiki, kuuvunja Muungano alipenda Mwarabu lakini hakufanikiwa itakuwa ninyi?
-Ni wazi Familia nyingi zina maunganiko Bara na Visiwani, tumeoleana sana...pana Wazanzibar au Wabara watakaokubali kulazimika kutumia Pasipoti kwenda kwa wake zao au waume zao pande zote mbili?
TUMEUNGANIKA BARA NA VISIWANI!!!
Mdau wa 46 Mfuasi wa kuvunja Muungano...Sipendi kutengana lakini nyie jamaa HAWATAKI.
ReplyDelete...tatizo ni kuwa UWEZEKANO WA MUUNGANO KUVUNJIKA HAKUNA...
Pangeni foleni mpokee Vitambulisho vyenu vya Taifa...daima...''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA''
Mhe. Maalim Sheikh Seif Shariff Hamad wa C.U.F yeye ANAUTAMBUA MUUNGANO NA AMESHA CHUKUA KITAMBULISHO CHAKE CHA TAIFA CHA ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA''
ReplyDeleteSasa hapo Wazanzibar WAPINGA MUUNGANO (hata kuchamba hamjui) mnafikiri bado ndoto zenu za kuvunjika Muungano zipo?
Ahhhh, acheni ubwege wenu!
Mtoa maoni wa 46
ReplyDelete.Sipendi kutengana lakini nyie jamaa HAWATAKI.
Hebu tueleze Mdau kila unachokitaka kwenye maisha yako unakipata?
Kila unachofikiri katika maisha yako kinawezekana kuwa?
Ni wazi unaweza kuwa na utitiri mahitaji LAKINI UWEZEKANO WA MAISHA USIKUPE NAFASI KUPATA!
NDIO KAMA SUALA LA MUUNGANO KUVUNJIKA KWA WENZETU, LINAWASHUGHULISHA SANA LAKINI LIPO NJE YA UWEZO WAO KULIPATA...NA NI WAZI HAKUNA HUO UWEZEKANO!
Muungano haujavunjika na KAMWE HAUTAVINJIKA!
ReplyDeleteASIYECHUKUA KITAMBULISHO CHA UTAIFA ATAUKALIA YEYE MWENYEWE, ITAFIKA WAKATI KILA KITU HUWEZI KUFANYA HADI UWE NA NATIONAL IDENTITY CARD.
Akili Wanzanzibar wapinga Muungano mnazo?
Angalieni, Viongozi wa juu Bara na Visiwani wamesha chukua ninyi mnaleta ujinga wenu hapa.
Mtakuja kugonga ukuta kwa use...ge wenu wenyewe!
wewe bwege wa 46 Sudan na Sudan Kusini zitakutana tena ktk AFRIKA YA MASHARIKI sasa hujui ya kuwa Muungano wa Jumuiya una nguvu zaidi kuliko Uhuru?
ReplyDeleteAma kweli hata Ilmu ya Maddrassa inaonekana hujasoma!
Kilichofanyika ni kutoa Demokrasia tu, mfano kabla hajagfariki John Garang Kiongozi wa Mapinduzi wa Sudan Kusini alishaweka Mkataba na Kaskazini na wakaunda Serikali ya Mseto.
Ndivyo hivyo hivyo hata kama Zanzibar itajitenga italazimika kuingia Umoja wa Afrika ya Mashariki ITAKE ISITAKE!
SASA INA MAANA NDIO ZANZIBAR ITAKUWA IMEFUNGIKA ZAIDI KULIKO ILIVYO SASA (hili ninyi akina gongo wazi hamlifahamu,,,wanajua akina Mhe.Maalim Seif na Mhe.Dr.Shein), KWA KUWA PALE ITABANWA ZAIDI KULIKO 'UMBWETE' INAOUPATA SASA KUTOKA BARA.
KWA MAANA YA ZAIDI NI KUWA ''ZANZIBAR ITALAZIMIKA KUZAMA ZAIDI KATIKA MUUNGANO ******sio na Bara bali wa AFRIKA YA MASHARIKI, ambako itabanwa zaidi*****''
Vitambulisho vya Taifa mnalazimika kuchukua hata kama unatokea Visiwani kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, HAKUNA nchi inayoitwa JAMHURI YA ZANZIAR.
ReplyDeleteNjaa na ugumu wa maisha kwa ninyi ndugu zetu Visiwani inatokana na uzembe wenu wa kufikiri.
Mbona wale Wazanzibar waliokuja kufanya biashara huku Bara hawalalamiki?
Mkiwa kama Raia halali wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, tena safari hii mkipatiwa Vitambulisho kamili, mnayo nafasi ya kutafuta maisha kwa Mikoa yote Bara zaidi ya huko Visiwani ambako sasa mna Mikoa mingine huku bara zaidi ya 30+,,,MSIFIKIRI KUVUNJA MUUNGANO NDIO SULUHISHO LA KUTATUA NJAA NA UGUMU WA MAISHA, INAWEZEKANA MKAVUNJA MUUNGANO NA NJAA NA SHIDA ZENU NDIO ZIKAZIDI!,,,
Kataeni Vitambulisho vya Taifa muone chenu!
ReplyDeleteWazanzibar wenzenu walileta ubishi kama ninyi, wakitaa kuitwa Wa Tanzania.
Walienda Ughaibuni walipofika kule ktk mchakato wa kujaza Fomu huko wakajaza wametokea Zanzibar, matokeo yake walikwama kwa kuwa Ulaya Wazungu walipoingiza taarifa ktk Computer haikupatikana nchi inayoitwa Zanzibar!
SASA NA NINYI HAYO HAYO YATAWAKAUTA KWA KUWA KITENDO CHA KUKATAA ID NI KUWA MMEKANA KUWA SIO WA TANZANIA ,(MKUMBUKE HADI SASA ZANZIBAR NI SEHEMU YA 'JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA') HIVYO HATA HUO UZANZIBAR MTAKUWA HAMNAO TENA!
Ni lazima ifahamike ya kuwa:
ReplyDelete1.HAKUNA NCHI KWA SASA INAYOITWA TANGANYIKA, AMA TANZANIA KWAMWE SIO TANGANYIKA.
2.HAKUNA ZANZIBAR KAMA NCHI BALI ZANZIBAR NI SEHEMU YA TANZANIA.
3.HAKUNA ZANZIBAR KAMA NCHI, HAKUNA TANGANYIKA BALI KUNA ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA''
Kama mnabisha Muulizeni Mhe.Dr. Shein na Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad!
''''Nawashauri msifanye uzembe na ujinga kwa kujinyima haki ya kuchukua Vitambulisho vyenu vya Utaifa ni vile mtajikuta mmeukalia''''
MTAKE MSITAKE MUUNGANO HAUFI BALI NDIO UTAZIDI KUIMARIKA ZAIDI!
Wadau samahani mie mdau naye msupport mdau wa Zanzibar lakini ni mtu wa Tangayika. Kama nilivyosema matusi na dharau inaonyesha jinsi wadau manvyoshindwa hoja. Jamani maswali yako wazi jibuni au wapi siko sahihi. Kumlazimisha mtu siyo Demokrasia. Humuwezi kuwalazimisha wat HAWATAKI muungano wenu uliowekwa na Magamba. Na jamaa wengi humu ni magamba pigeni kelele tu lakini siku zenu ni arobaini.
ReplyDeleteMdau wa Zenjibar No.64,
ReplyDeleteJe, unaweza kupiga U-Turn kiungo chako cha jinsia kama wewe ni mwanaume ukajilawiti wewe mwenyewe?
Kama zoezi hilo utaliweza na pia Muungano utaweza kuvunjika!
Lakini kama wewe au binaadamu mwingine hawezi kutimiza hilo, ama hakuna mtu anayeweza BASI VIVYO HIVYO MUUNGANO HAUWEZI KUVUNJIKA!
Mdau wa 64 juu wewe na Wapinga MUUNGANO NDIO MMESHINDWA HOJA!
ReplyDeleteKama mnao uwezo wa kuvunja Muungano HADI SASA mnangoja nini?
Mzanzibar,
ReplyDeleteLeo kimya Mhe. Raisi wa Zanzibar Dr. Shein anaendelea na kazi ya kuzindua Vitambulisho vya Taifa leo.
Sasa wewe na wenzako endeleeni kukataa Vitambulisho vya Taifa ndio mtajikuta hata Uzanzibar wenyewe mnakuwa hamnao kwa kuwa usipokuwa Raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania KAMWE HUWEZI KUWA MZANZIBAR!
Itakula kwenu!