Serikali inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi waandamizi wa serikali na Taasisi nyeti ikiwemo Usalama wa Taifa kujipatia fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi hao.

Watu hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa maofisa mbalimbali wa wizara, mashirika ya umma na Idara za Serikali zinazojitegemea kuomba pesa ili wawafanye mipango ya kupandishwa vyeo.

Utapeli huo umekuwepo nchini kwa kipindi kirefu sasa , ambapo watu huwapigia simu viongozi wa Taasisi za fedha , Mifuko ya Taasisi za Jamii na watu binafisi wakiomba fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi waandamizi Serikalini wakati si kweli.

Watu hao wamekuwa wakiwatapeli maofisa mbalimbali kuwa wanaweza kuwafanyia mipango ya kupandishwa vyeo endapo watawapatia kiasi cha fedha jambo ambalo halipo katika taratibu za utumishi wa umma.

Utumishi wa umma unazo taratibu zake za kuwapandisha vyeo watumishi wake kulingana na sifa za kada zao na wala haiwezekani kwa viongozi waandamizi kuwachangisha fedha kwa ajili ya kuwapandisha vyeo.

Serikali inawataka wananchi kuwapuuza matapeli hao na watoe taarifa katika vyombo vya dola na usalama mara wapatapo ujumbe wa aina hiyo ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI (MAELEZO) DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ama kweli Bongo Tambarale,

    Kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake, hapo vipi kupandihswa vyeo ni Maafisa Usalama wa Taifa hewa tu, hakuna na Waganga wa Kienyeji?

    ReplyDelete
  2. Tatizo ni kuwa idaadi kubwa ya watumishi wamepata ajira kupitia rushwa. Tz bado hatujaiweza rushwa na inakuwa rahisi kuamini kuwa pesa ndizo zitakupa madaraka. Mdau Ukerewe

    ReplyDelete
  3. Naamini mchezo huo utakuwa unafanyika kwa wengi wanaopandishwa vyeo ndio maana hao majinamizi wameonelea na wao watumie mtindo huo unaofahamika ili kujipatia kipato.ndio maana utakuta watu wanapandishwa vyeo lakini utendaji wao wa kazi ni hoi bin hoi.Hata unajiuliza huyu alipandishwa cheo kwa minajiri gani hata barua tu hawezi kuandika kwa ufasaha lakini kapewa cheo.Hao matapeli hawajabuni kitu cha hewani tu, bali ni kitu kinachofanyika kwa wengi wanaopandishwa vyeo serikalini kindugu au kwa kuhonga wakubwa.Hata hivyo tunashukuru kwa tahadhari hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...