Baba mtakatifu Benedikti wa 16
Katika hali isiyotegemewa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki lenye kusadikiwa kuwa na wastani wa waumini billioni 1.2 duniani kote ; kiongozi huyo, baba mtakatifu Benedikti wa 16 ametangaza kujiuzulu. Sababu zilizotolewa kutoka kwa msemaji mkuu wa Vatican Padre Frederico Lombard, washirika la wamisionari Wajesuit ameuthibitishia ulimwengu kuhusu habari hizo kupitia radio Vatican. Sababu za Kiumri na kiafya ni baadhi ya sababu zilizohusishwa na kujiuzulu huko.
Baba mtakatifu Benedikti wa 16 alizaliwa 1927 na kubatizwa jina la Joseph Ratzinger. Amekuwa Pope wa 265 katika mlolongo wa viongozi wa kanisa hilo.
Ratzinger alikuwa na umri wa miaka 78 wakati alipochaaguliwa kuliongoza kanisa hilo mwezi April 2005.
Hakuna Pope ambaye amejiuzulu kwa hiari katika nyakati za hivi karibuni na Pope wakwanza kuachia ngazi alikuwa Pope Gregory XII mnamo mwaka 1415; yapata miaka – 598 iliyopita. Kabla ya yake Pope mwingine aliyejiuzulu kwa hiari ni Pope Celestine V mnamo mwaka 1294.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...