Mrs. Leticia Daudi Lusala
Mungu wetu ni Mwema, ametuliza mioyo yetu katika mwaka huu mzima wa ukiwa na majonzi mengi kwa kumkosa mpendwa wetu Leticia. Ndio maana tunajumuika tarehe 8 na ( ili kushukuru mungu na kumwomba amweke mahali pema peponi amina.
Familia ya Mr. Lusala inapenda kuwakaribisha katika misa ya kutimia kwa mwaka mmoja tokea tulivyompoteza mama yetu mpendwa marehemu Leticia Lusala,itakayofanyika kwa mkesha siku ya ijumaa hii tarehe 8, na siku ya jumamosi tarehe 9/02/2013 kutakuwa na misa katika kanisa la Sinza Katoliki saa 3 asubuhi,halafu safari ya kwenda makaburini kinondoni kwa sala fupi, tunaomba wote tujumuike kumsalia na kumsindikiza mama yetu mpendwa.
Kwa habari zaidi wasiliana na Seraphin 0786303038 na Edward 0754091883
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...