Wakati wengine wanasherekea siku ya wapendanao duniani ! lakini kwa mwanamichezo Oscar Pistorius imekua kinyume ! badala ya furaha ni msiba! Leo asubuhi na mapema huko Pretoria, Afrika kusini Polisi walitia mkononi mwanamichezo nyota aliyejipatia umarufu katika michezo ya Olympic Bw.Oscar Pistorius (26),ametiwa nguvuni na polisi wa nchi hiyo kwa madai ya kumuua mpenzi wake model Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi!

Inasemekana leo asubuhi milio ya risasi ilisikika nyumbani kwa mwanamichezo huyo mjini Pretoria  na polisi walipofika walimkuta mpenzi wa mwanamichezo huyo Bi. Reeva Steenkamp (30)  ambae pia ni model ameshauwawa.Polisi wa Afrika kusini wanategemea kumfikisha mahakamani bw.Oscar Pistorius (26) kwa mashtaka ya mauaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kuna nini humo TFF??Lazima kuna "KITU".Tunaomba kufahamishwa hicho "KITU" kinacholeta mtafaruku wote huu.

    David V

    ReplyDelete
  2. ALICHOKIFANYA HUYU JAMAA NDIO MAANA YA SIKU HII YA LEO ....WATU WENGI WANADHANI KUWA NI SIKU YA WAPENDANAO ILA SIVYO HII SIKU KIHISTORIA BI YA MAUWAJI YALIYOFANYWA NA BWANA MMOJA MSPAIN ...ALIUWA WATU WENGI SANA NA BAADAE AKATOWA AGIZO IITWE SIKU YA WAPENDAO

    SASA KWA SISITUSIOJUWA KITU TUNAOFUATA KILA CHA ULAYA NDIO HIVYO TENA KILA WAFANYACHO WAZUNGU HATUULIZI WALA KUFANYIA UTAFITI TUNAFUATA TU .....

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu umeongea ya maana.Maana ss baadhi ya wabongo huwa tunafuata mikumbo na ukijaribu kuwafahamisha watu wanaona kama uzushi.

    ReplyDelete
  4. Haaa unakuta watu na miguo yao myekundu eti wanafurahia mapenzi hata bila kuelewa maana ya valentines du!

    Huyu mwanamke sijui alijiaminisha nini kwa huyu mwanaume jamani by the looks in his eyes the guy seems to have grudges!

    ReplyDelete
  5. Tukio hili ni Upande wa Pili wa Sarafu ya Mapenzi:

    MAPENZI SI LELEMAMA!

    Mapenzi yana mambo mangi sio Raha na furaha kama wengi wanavyofikiri, mapenzi yamekaa kama 'homa za Vipindi' yanapanda na kushuka.

    Mfano wawili ktk siku za awali kicheko hadi jino la mwisho ,katikati wanakuwa wanadumaliana hakuna tabasamu,
    mwishowe wananuaniana na kuishia kutimuana!

    Mfano Mwanamuziki Hayati Remmy Ongala aliimba:

    Penzi, Mwanzo HUWA TAMU KAMA ASALI, kati kati ya Mapenzi huwa CHACHU KAMA LIMAO, na mwisho wa Penzi huwa CHUNGU KAMA SHUBIRI!

    Hivyo msione watu wanaamua kukaa singo, mkaona kama labda jamaa Sio Rijali ama nini ni kutokana na karaha kama hizo za upande wa pili wa Sarafu ya Mapenzi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...