Freddy Macha ! na Wimbo wake "Freedom"

Freddy Macha si jina geni kwa watanzania na wadau wasanaa popote pale duniani, unapolitaja jina la Freddy Macha lazima utakugusia vipaji vya matanzania huyo mwenye vipaji vinavyolijaza gunia la sanaa,uandishi wa makala,utunzi na simulizi za hadithi,tungo za mashairi,kuimba nyimbo na muziki n.k, Msanii Freddy Macha mtanzania mwenye makao yake nchi Uingereza,ni msanii aleyeibeba Tanzania sio katika damu tu bali ndani ya moyo wake wote kila anapokwenda Tanzania kaibeba ndani ya moyo wake.

Mzalendo Freddy Macha ni msanii ambaye amepitia anga nyingi duniani kama vile katika nchi za Amerika Kusini,Ujerumani,na Uingereza ndio maskani yake. Freddy Macha mwenye tabia za kuchanginyika na jamii za kimataifa na kwa haraka sana ni mwepesi wa kunasa lugha za kimataifa ! Lugha kama vile Kireno,Kijerumani kwake ni sawa na maji ya kunywa! leo hii anametuletea wimbo wa "Freedom" ambao ameupiga na bendi yake "Kitoto Band" yenye makao kule Uingereza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kitu nachopenda kwako ni kwamba wewe ni diaspora unayeweka jina la nchi yako mbele kwa kila unachofanya. kwa hilo inabidi upewe tuzo ya aina fulani. diaspora wengi hawataki kujitambulisha na tanzania wengi wanataka waonekane 'african american' na walioko england wangependa waonekane wa 'wa carribean' kuliko 'wa africa'!

    ReplyDelete
  2. Macha...thanks for the good music. What a breath of fresh air. Yaani wanamuziki ambao wanajua kupiga vyombo wenyewe na kuimba wenyewe. Liwe fundisho cha muziki wa kizazi kipya kuwa muziki wa Computer na Autotune unakera sana. Na miziki ya kutumia computer inawalemaza sana. Nyimbo zote zina sikika kama zile zile. Autotune huwezi kutofautisha kati ya Ali Kiba na Diamond. Na sijui kama wanaweza wakapiga magitaa...
    Macha tunashukuru.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...