Mratibu wa taasisi ya Shikamana Brittany Karima Cesarini( kulia ) akiwakabidhi vipeperushi vyenye ujumbe wa tuungane kutokomeza unyanyasaji,Wanafunzi Mozes Festo wa shule ya sekondari ya Mbezi Beach na Husna Methew wa shule ya sekondari ya Jitegemee, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa elimu ya kutokomeza unyanyasaji kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam, ufunguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Theater 1 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mratibu wa taasisi ya Shikamana Brittany Karima Cesarini( kushoto ) akiwahutubia wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa elimu ya kutokomeza unyanyasaji kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam, ufunguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Theater 1 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mhadhili wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Vicensia Shule ,Wakili wa kujitegemea Laetitia Petro na mjumbe wa Shikamana Ansia Albert .
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam, wakiwa na vitabu vilivyo andikwa Hali Halisi ya Kijinsia Nchini Tanzania wakati wa uzinduzi wa utoaji wa elimu kwa shule za sekondari juu ya unyanyaaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya utoaji wa mahusiano ya mazuri ya kimapenzi kwa vijana .Shikamana wamedhamilia kuleta mabadiliko juu ya utoaji wa elimu kwa jamii ili kupambana na aina zote za unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...