TAARIFA KWA UMMA

Tunasikitika kuwataarifu kwamba mnamo tarehe 3/02/2013 saa 12:00 asubuhi kulitokea ajali ya moto katika chumba cha mifumo ya mawasiliano kilichopo sehemu ya juu kabisa Jengo la PPF Tower lililoko makutano ya mtaa wa Ohio na Garden Avenue. 

 Moto huo ulidhibitiwa kwa ushirikiano wa vikosi mbalimbali vya zima moto. 

Zoezi hilo la uzimaji wa moto lilitumia kiasi kikubwa cha maji ambayo yalisambaa kwenye maeneo ya ngazi,mifumo ya umeme na mawasiliano. 

 Wataalamu wanaoshughulikia mifumo ya umeme wamefanya ukaguzi na kushauri kusitishwa kwa matumizi ya umeme katika jengo hilo mpaka watakapokamilisha zoezi la ukaushwaji wa maji hayo. 

Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mapema iwezekanavyo. 

 Moto huo haukuathiri sehemu nyingine za jengo hilo zikiwemo ofisi za wapangaji. Tunaomba wapangaji,wadau na watumiaji wengine wote wa jengo hilo wawe wavumilivu wakati zoezi la ukaushaji wa maji hayo inaendelea na kisha umeme kurejeshwa ili waweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida. 

 Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza 

 MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani Mnatakiwa kujenga tabia ya KUKINGA kwa kukagua majengo yenu kwa utaratimu fulani zaidi ya hapo ni upuuzi mtupu. Pia ni wajibu wa mkurugenzi kujumuisha katika taarifa zake ni NINI ATAKIFANYA KUZUIA/AU KUPUNGUZA NAFASI KWA HALI KAMA HII KUTOKEA. Bila hivyo tnaendelea kuwa watoa taarifa baada ya matukio hasi kama haya.

    ReplyDelete
  2. Bora wafanye mazoezi ya kupanda ngazi maana wamezidi vitambi.

    ReplyDelete
  3. huu ndio uungwana tunaoutaka. kukiri na kuomba radhi basi watu wenye utu watakuelewa tu.poleni PPF Tower,haya yapo lakini nashauri muwe mnakagua mifumo yenu mara kwa mara ili kuepuka yanayoepukika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...