Kikosi cha timu ya Tanzania.
Wachezaji wa Taifa Stars wakisalimiana na wenzao wa Cameroon.
Kikosi cha timu ya Cameroon kikiwa katika picha ya pamoja.
Beki wa timu ya taifa ya Tanzania, Erasto Nyoni akijaribu kumzuia kiungo wa pembeni wa Cameroon, Bedimo Henri wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samata akimtoka beki wa kushoto wa timu ya Cameroon, Benoitte Assou-Ekotto wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Tanzania imeshinda 1-0.
Mbwana anampiga chenga beki wa Spurs! Kumbe bongo tuna vipaji bwanaa!!
ReplyDeleteAhhh!,
ReplyDeleteHii ndio ile ile Cameroon 'Endomitable Lions' tunayoijua au wamewakilishwa na Lipuli F.C ya Ludewa-Iringa?
Hivi ni kweli Cameroon kamilia au Cameroon walicheza na sisi wakiwa macho makavu au wamefumba macho?
Mdau wa kwanza,
ReplyDeleteTukiacha majungu,
Tukiacha maslahi binafsi,
Tukiacha ujinga,
Tukajipanga kila kitu kinawezekana kama tunavyoona Mbwana Samtta anampiga chenga Benoitte Assou-Ekotto Beki wa Spurs na akazamisha Bao kimiani!
Wewe #2 wape vijana moyo bwana.Vijana wanajituma,nadhani tuko kwenye mwelekeo mzuri.Kama unafuatilia mpira wa miguu,utagundua kwamba kuna mapinduzi makubwa kwenye mpira wa miguu sasa hivi duniani.Na ndiyo maana Cameroon hawa hawa walitolewa na Cape verde wakati wa kuwania nafasi ya kucheza AFCON 2013 inayoelekea ukingoni sasa hivi.Sasa angalia kikosi cha Cameroon kilichoanza jana halafu tafakari mwenyewe.
ReplyDeleteEffala Komguep-Coton sport(Cameroon)
Assou Ekotto(Tottenham H-Uingereza)
Aminou Bouba-CotonSport(Cameroon)
Ngoula Patrik(Unsportive de Douala-Cameroon)
Nyom Allan- Granada(Hispania)
Pierre Wome (Huyu amecheza Ulaya tangu 1996,sasa yupo nyumbani Coton Sport)
Kingue Mpondo- FC Kairat(Kazakhstan)
Bedimo Henry- Montpellier(Ufaransa).
Tchami Herve-Budapest Honvéd FC(Hungaria),
Olinga Fabric-Málaga CF(Hispania)
Aboubak Vicent-Valenciennes(Ufaransa)
David V
Tatizo letu ni kujidunisha na kuwa na fikra za kitwana.Kwanini wao waweze wana nini nasisi tushindwe tuna nini. Vema sana taifa stars, tunajionea fahari kwa juhudi zenu, endeleeni na moyo huo huo.
ReplyDeleteWadau tubadilike na tuipongeze taifa Start na kocha Kim na benchi lake lote la ufundi,vijana wanajituma sana na tunapoelekea ni patamu,soka limebadilika sana na kwa mwendo huu huenda tukacheza fainali zijazo za kombe la Afrika na dunia.Wabongo tuvute subira matunda yataonekana,mfano mzuri ni Burkina Faso,je nani angekubali kuwa wangeiondoa Ghana na kucheza fainali za Afrika?Je mmewaona akina Drogba walivyoadhirika?Mpira wa sasa sio majina ila ni vipaji na kila kitu kinawezekana,big up mdau ughaibuni!
ReplyDeleteWadau mnaoponda Taifa Stars lazima mjue kuwa mechi hizi za kirafiki za FIFA sharti lake moja ni lazima timu zichezeshe kikosi kamili cha taifa na si timu B, kwa hiyo hao ndio Cameroon wenyewe hasa. Na kwa nini Watanzania tunaponda juhudi za timu yetu? haya ni mafanikio ya kocha Poulsen anajua kuunda kikosi imara cha kudumu cha Taifa Stars, timu hii akiendelea nayo Poulsen itakuja kuwa tishio Afrika nzima.
ReplyDeleteLeo nakupongeza David D. kawaida huwa nakupinga kwa mawazo yako mgando kuhusu ndugu zetu wetu walioko Ughaibuni. Kweli, Stars wanaitaji support lakini inabidi tuwe na mikakati mizuri, yaani program za wachezaji toka watoto,na mashuleni vile vile. Na wanawake, Twiga Stars wanaitaji support. Ukiangalia timu zilizo kali ulimwenguni,ukichanganya za Africa, timu zao za wanawake zimeendelea vibaya mno, wakti sie tumisimama. Wengine tunakaa kimya kwa mambo mengi, kwani watu wanapiga kelele ili wasikie una mawazo ghani alafu jamaa wanaiga na kusema wao ndiyo waliobuni, wakati watu wengine wamesomea vitu kwa muda mrefu. Jamnai nasema kila mtu mwenye busala anjau ukiumwa unakwenda kwa Daktari, hata wa kienyeji-TZ tutakapoacha kuwapa watu kazi ambazo sio zao hapo ndiyo tutasonga mbele.
ReplyDeleteDavid V
ReplyDeleteDuuu kwa Kikosi hicho kwakweli najisahihisha mimi mwenyewe nilio post #2 ya kuwa Kazi imefanyika!
Hawakukabiliana na Lipuli F.C!
Vijana wanstahili pongezi!
wewe kaseja fanya mazoezi beba hata nondo kidogo ujaze ona wenzio .acha chips.punguza jig jig..ila kwa mechi ya jana mlijitahidi vijana.
ReplyDeleteMnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Stars jana waliwapa raha Watanzania wanaothamini vitu vya kwao wale wanaothamini vya wenzao na kuangalia mpira wa jana watakuwa wameumia!
ReplyDeletesesophy
Mdau wa nane (8) anony Thu Feb 07, 03:36:00 pm 2013
ReplyDeleteUnaempongeza Mdau mwenzetu Daivd V. humu jamvini lakini unapingana naye kuhusu 'sera ya ndugu zetu wa Majuu'
Mimi nasimama na Mdau David V.nikiunga mkono ya kuwa'''Kinachohitajiwa ni wao wa Majuu kuakisi ushiriki wao ktk masuala mbali mbali hapa nyyumbani'''
Wanaweza kushiriki ama kwa kuja hapa ama huko waliko kwa kuwa Serikali yetu kwa Busara kubwa Imetambua uzito wao na imeunda Idara ya Diaspora ktk Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa lengo hilo la kuwaunganisha na Tanzania na kuakisi mipango mbali mbali ya maendeleo Kiuchumi na Kijamii.
Madiaspora wana mchango mkubwa sana kiuchumi kwa nchi walizotoka wakiwa huko Majuu
Madiaspora wa Afrika waliopo Majuu ikiwemo Tanzania wameweza kutuma Afrika kiasi cha US$ 60 Billion ambapo kama gharama za utumaji zingekuwa chini wangefikisha US$ 64 Billion (Kwa kuongeza US$ 4 Billion zaidi)
Angalia Ripoti ya World Bank 2012 kwenye link hii
http://www.worldbank.org/en/news/press-release/2013/01/28/african-migrants-could-save-US4-billion-annually-remittance-fees-finds-world-bank
Tunawahitaji sana Madiaspora wa Tanzania mfano kama hapo ktk Kikosi cha Taifa Stars tungepata Wachezaji wengi kama unavyoona Kikosi cha Cameroon karibu wote wanacheza Majuu, na pia Kiuchumi ktk sekta na maendeleo yetu nchini kama unavyoona tunahitaji Wataalamu na Wawekezaji wa ktk sekta mpya za Kiuchumi za Gesi, Mafuta na Madini tungepata wandugu zetu Kuwekeza na kuwa Wataalam ingefaa zaidi.
Anonymous wa #Thu Feb 07, 06:32:00 pm 2013 kwahiyo unaungana na mimi kuhusu Madiaspora na sio mawazo ya David D. Kwani yeye anapinga kuhusu watu kuwa na uraia pacha, Tanzania. Hivyo vyote ulivyosema kuhusu Madiaspora, ndiyo nakubalina na wewe, kwamba kweli jamaa zetu tunawaitaji sana. Mie nafuatilia sana maoni ya jamaa humu,David D akiwemo, wenyewe wanaona kama Madiaspora kama hawapo Bongo basi hawana faida kwa Bongo, ambapo si kweli.
ReplyDelete