Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,(kulia) akimkabidhi zawadi ya Kasha Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Yussuf bin Alawi bin Abdullah,akiwa kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,baada ya hafla ya chakula maalum,kilichoandaliwa kwa ujumbe huo,katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar
Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Yussuf bin Alawi bin Abdullah,akitoa hutuba fupi ya shukururani zake kwa kuandaliwa chakula maalum,akiwa na ujumbe wake katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,(kushoto) alipokuwa akitoa hutuba fupi ya kuwashukuru wageni wa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Yussuf bin Alawi bin Abdullah,(kulia) baada ya kushiriki katika hafla ya chakula maalum,katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar.
'Chakula cha usiku' kweli Waarabu watakubaliana nacho?
ReplyDeleteHivi sasa Lugha yetu ya Kiswahili imepanuka sana, kwa haraka haraka unaposikia neno 'chakula cha usiku' unakuwa umeshafika mbali zaidi ya maana yenyewe ilivyo.
Nadhani Wageni wakielekezwa Kiswahili kwa undani zaidi watapendekeza wale cha mchana!!!
Bwana Yusuf bin Alawi waziri wa mambo ya nchi za nje wa Oman ana miaka 30 au zaidi katika wizara hio. Mkongwe wa mambo ya kisiasa yake ni mambo kimya kimya kunapotokea mgogoro wowote duniani. Ni mmoja wa wana siasa wachache ambao siasa yake ni kutoingilia mambo ya nchi zingine katika mambo yake ya ndani. Tunakumbuka vita vya ghuba Oman iliomba Iraq na Kuwait wakae meza moja ili kuepuka balaa la kuingiliwa na mataifa makubwa nadhani mwisho wake mnaujua ni nchi zote mbili kuteketea watu na mali!
ReplyDelete