Machafuko makubwa yametokea leo katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.

Habari za kuaminika kutoka eneo hilo la tukio lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa dini ya kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo.


Imeelezwa kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinja ng'ombe mmoja na mbuzi wawili eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya waislamu.


Tukio hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama kuwasili katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la kuifunga.

Wakati wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lilipambwa kwa maandishi BWANA YESU ASIFIWE,YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.

Kutokana na hali hiyo wakristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao walitumia mapanga na majambia.


Hata hivyo wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.


Mbali na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na Said Ntahompagaze(45),Sadick Yahaya(40),Yasin Rajab(56),Vicent Damon(22),wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika hospital ya wilaya ya Geita.

Hata hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.


Jeshi la polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa 4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.


Mkuu wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya kidini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Haya mambo yameanza lini? Mbona kila mtu ana uhuru wa kuchagua nyama imechinjwa na nani,iwe
    mkristu au mwislamu. Nakumbuka Mzee Ruksa alieleza kirefu kwa sheria ya nchi na hadithi za vitabu vya dini miaka ya 90s. Sasa kipi kipya hapa? Waombeni wazee wenye busara zao wawaelimisha hawa wajinga.

    ReplyDelete

  2. Mmmmmmmh,sasa tunakwenda pabaya....

    ReplyDelete

  3. Mh! Toka lini! , kuna mkono hapo.

    ReplyDelete
  4. Hapa si bure tangia lini Geita?kukawa na waislam wakereketwa?kiswahili chenyewe hawakijui naona huu mkono unatoka nje ya nchi,na tukikaa kimya tutakua next Nigeri

    ReplyDelete
  5. Masikitiko makubwa sana.Vita ya aina hii haina mshindi! Aliyeanzisha sakata la kitoweo kuchinjwa kikristo/kiislamu ana damu mikononi mwake ankal!

    ReplyDelete
  6. mbona viongozi wa nchi hatuwasikii wakikemea??

    ReplyDelete
  7. Disgusting. What is it we are not being told here? is it about religeous tolerance really? Tumekuwa tunavumiliana miaka yote kwa maswala haya ya aliyechinja nani nini iweje leo? we need a better explanation to this. Si swala la ukristo/ uislamu sasa kwa mtindo huu. We have a right to be told the truth behind all these. tunaelekea wapi? kwa nini? please, whoever is concerned, we need to know. These are human lives, Tanzanian lives we are talking about here, not some animals!!! please tell us...we need to know.

    ReplyDelete
  8. Hii ni matokeo ya Umaskini hasa wa busara, hali na mali. Nyama kisingizio. Ukristu/Uisilamu Kisingizio. Haya hayawezi kutokea Msasani, Oysterbay, Upanga ...

    Wanajamii wa Chato, mjue wakati ninyi mkichinjana; viongozi wa Taifa wanakula Kuku kwa mrija. Kilio cha Kuku!

    ReplyDelete
  9. hawa watu wanatakiwa kuelimishwa kuwa mtu anahaki ya kufanya jambo lake analotaka ila tu asivunje sheria, wakristo kuwa na bucha zao sawa kabisa kwani tatizo ni nini hasa, hivi sababu ni hiyo kuwa na bucha yao na nyama walizochinja wao au kuna ajenta ya siri imejificha?kumbukeni mlichoma makanisa wajkristo wakanyama sasa na wao iko siku watachoka watasimama kujitetea.

    ReplyDelete
  10. Hizidini zingine zinatupeleka pabaya. Sijawahi kusikia wakristo wakipigana kwa sabb za kidini. Hawa wanaopigana na waislamu si wakristo.

    Wakristo walishaamini kuwa waislamu ndio kazi yao kuchinja na waliamini na wakalikubali. Kama leo imetokea hawa wanaijiita wakristo wakaona ni upuuzi, basi, wajitafutie dini nyingine. Wakristo hawapiganii dini , wao huamini kuwa Mungu ni muweza yote, binadamu hana nguvu ya kumpigania.

    Kichaa akikuvua nguo ukamkimbiza ukiwa uchi, wenye akili wataamua nani kichaa zaidi.

    ReplyDelete
  11. Kweli Mungu anahitajika hapa, kwani tunakokwenda pabaya. Lakini haya yote yaliandikwa kuwa siku za mwisho zitakuwa za hatari, upendo wa wengi utapoa kwa sababu ya kuongezeka maasi. Jamani tutubini tumrudinieni Mungu ili tupone.

    ReplyDelete
  12. Tunamhitaji Mungu

    ReplyDelete
  13. KWA HALI HII....TUNAKWENDA WAPI!

    Aliyeanzisha MADA hii ya UCHINJAJI achukuliwe HATUA KALI..., kwani imetuletea mapokeo mabaya ikiwepo hili! Leo Geita kesho hatujui itakuwa wapi. Nchi yetu hii hajafikia viwango vya kimataifa wandugu, tusihukumiane bure. Tunaomba suala la kuchinjwa liachwe kama kawaida kila mtu achinje anavyotaka.

    ReplyDelete
  14. Hili limetoka wapi? Tanzania haikuanza leo. Tumevumiliana miaka yote na tukijua waislamu wakichinja. Wazee wetu walituachia utamaduni huo tumeurithi bila kinyongo na kwetu imekuwa kama sheria zetu za kimila kuwa tunazifuata japo hazikuandikwa popote pale. Hili pia linajulikana na limetuweka pamoja miaka yote. Tumedumu tukikaribishana chakula majumbani na kama nduguyo ni muislamu lazima utamtafuta mchinjaji. Huko tunakokwenda na agenda hii ina mkono wa mtu! sio bure. Ana nia mbaya nchi yetu tuuane tumalizane wacheke. Ikifikia mahali Bucha za madhehebu/ Hoteli za madhehebu/ na sherehe zote za madhehebu basi hata makazi ya madhehebu yataanza. Nchi vipandevipande! Waliopewa pesa watugawanye watacheka nasi hatutakuwa na umoja huu tena. Hii ni sawa na kula nyama ya mtu kama alivyosema Mwalimu Nyerere! Watoto wetu tunawajengea mfarakano na sijui nchi kama itakalika. Mungu atuepushie hili. Viongozi wa dini wenye nia ya amani wakutane warejeshe hali tuliyoizoea ya kutembeleana/kukaribishana chakula na kuoleana bila kukwazana!

    ReplyDelete
  15. Hii inanishangaza,waikristo walikuwa wakisema,waislam wana udini,vipi miaka yote walikuwa wanakula nyama iliyokuwa inachinjwa na nani.kumbukeni RWANDA NA BURUNDI MAASKOFU NA MAPADRI WALIANZISHA HAYA.Mpaka leo hapajatulia vizuri.Isitoshe waikristo wao wamezoea KUUA NGURUWE NA HATA KULA NYAMAFU AU Mnyama aliyekufa.na ndio maana dhima ya kuchinja wazee wetu wakakubaliana wachinje waislam.HOFU NI KWAMBA MTATULISHA HARAM

    ReplyDelete
  16. Ehhhh haya mambo ya Boko Harram sasa!

    ReplyDelete
  17. Hapo wlitaka wachinje wao ili waweze kujipatia Makongoro, vichwa na (mapu...w.bu) ya ng'ombe na mbuzi!

    Si mnajua ktk Makabila mengi mchinjaji baada ya kumaliza kazi yake anakuwa na haki ya kupewa aina fulani za nyama?

    ReplyDelete
  18. Hapo wlitaka wachinje wao ili waweze kujipatia Makongoro, vichwa na (mapu...w.bu) ya ng'ombe na mbuzi!

    Si mnajua ktk Makabila mengi mchinjaji baada ya kumaliza kazi yake anakuwa na haki ya kupewa aina fulani za nyama?

    ReplyDelete
  19. HAPA NASHANGAA.
    MBONA UKINUNUA SOSEJI AU UKIENDA HOTELINI HAULIIZI NANI ALIECHINJA KABLA YA KULA? NA JE KAMA WALITANGAZA WAMECHINJA WENYEWE , KWANI NI LAZIMA KWENDA KUNUNUA NYAMA KWAO?
    WANGECHUKULIA HILO BUCHA KAMA LINAUNZA 'KITIMOTO' KWA HIYO HALIWAHUSU.

    SAMAHANI LAKINI.NI MTAZAMO TU

    KAMA KIONGOZI NA MTANZANIA MZALENDO NA MWENYE KUJALI UHAI WA WANANCHI WANAOKUZURUNGUKA.TAFAKARI NA UCHUKUE HATUA.

    ReplyDelete
  20. I think the law should be followed: politics and religions aside. The murderers ought to have been arraigned by now. Statements given by the government leaders are not acceptable. The government should take stern actions to prevent this hooliganism from spreading accross the country.

    ReplyDelete
  21. Natanguliza shukrani kwa wote mliotangulia kuchangia mada hii....Mmeonyesha busara kubwa ya kutopendelea upande wowote bali ule wa mtanzania na uhai wake...Dini ni kitu kizuri na silaha ya kuleta amani.....ila ukiwa na uhaba wa elimu yake unaweza kulifanya gobole lionekana baya badala ya mfatuaji.

    Wakristo wana haki ya kuchinja na kula nyama waitakayo...Hakuna mtu mwenye haki ya kuwazuia....wamekuwa wanakula kiti moto kila kona za bar nchini bila matatizo....kwa mtazamo wangu si busara kuchinja nyama kanisani halafu upeleke kwenye bucha la kijiji.....ingekuwa vizuri nyama ile ingegawiwa kanisani kama sadaka au kuuzwa huko.....Hata hivyo....waislamu nao hawana haki ya kuvamua duka wala kupiga na kuuwa watu kama insjulikana vyema kwamba bucha hili ni la wakristo si la wote...kwa maana hapa panauzwa kiti moto na nyama nyingine ambazo mchinjaji ajulikani.....Kama bucha hili ni la mtu binafsi basi yeye ndiye alaumiwe kwa kupokea nyama ambayo ambayo inaleta utata kwa wengine.....Tusitazame faida peke take bila kujua hasara inayoweza kupatikana

    ReplyDelete
  22. Nadhani ipo haja ya Watanzania kuvumiliana!

    ktk nchi hii tukianza kuamsha 'yaliyolala' taifa hili litapasuka vipande vipande!

    Leo tunapigania haki ya kuchinja, kesho ya kuongoza nchi, kesho kutwa nafasi za ajira serikalini, baada ya hapo ardhi, hatimae kila mtu akitaka uongozi akagombee kwao ivi kwewli tutakua na taifa tena sisi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...