Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania, Mhe. Sospeter Mhongo, akiwa Ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe, akiangalia Kitabu cha wageni kilichopo Ofisini hapo, kabla ya kusaini Kitabu hiko.
Mheshimiwa Waziri Sospeter Mhongo (kulia) akiongea na baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji mapema leo kwenye Mkutano wake ambao aliufanya kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London, (kulia),Mhe. Balozi Peter Kallaghe, akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mhe. Waziri, alipokuwa akiongea na Wawekezaji hao wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta hiyo ya Nishati na Madini.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Kigeni na Wajasiliamali wa Kitanzania, kwenye Sekta ya Nishati na Madini, wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini Tanzania, Mhe. Sospeter Mhongo, alipokuwa akiongea nao mapema leo.
Mheshimiwa Waziri Sospeter Mhongo (kati), akiwa kwenye picha ya pamoja Wawekezaji, (kushoto) Bwana Manubai Teraiya, mwakilishi wa Lloyds Eastern Group na (kushoto) ni Dada Gillian Raini Mwakilishi wa Kampuni ya East Africa Ventures.
Mheshimiwa Waziri, akibadilishana mawazo na Wawakilishi kutoka Kampuni ya Margin Capital ya Uingereza, mara baada ya kumalizika mkutano na Wafanyabiashara na Wawekezaji hao.picha na Rashid Dilunga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...