Afisa bidhaa na huduma wa Vodacom Tanzania Bw.Athanas Muhanuzi(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1 Bw. Stanley Maliwa,aliejishindia katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,katikati ni Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.Rukia Mtingwa. Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa kushoto akimsisitiza jambo Bi.Elizabeth Kavishe(kulia)wakati wa kumkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1 aliejishindia katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,katikati ni Meneja wa malipo ya baada wa kampuni hiyo Bw.Ibrahim Kiongozi. Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bwana Michuzi leo usiku kwenye kituo kimoja cha hapa Uholanzi walikua wanaongelea kuhusu mlima kilimanjalo mpaka wakauonyesha ulipo,,wakawa wanauliza ndani ya ukumbi uliojaa watu, ilikua kipindi flani,wakauliza huu mlima ni maalufu saana hapa duniani ni nani anaweza kutaja ni nchi gani na mkoa gani?Aisee wengi wakasema eti ni Kenya wengine Egpte,,lakini nimejisikia furaha kuona dada mmoja mrembo kataja na kusisitiza kwamba huu mlima upo Tanzania tena nchi ya amani tena nzuri saana,Aisee ingawa mimi ni mrundi lakini nimejisikia fleshi kwasababu Burundi ni rafiki wa Tanzania,pia kuna wa bongo wengi wapo ulaya kwa njia ya urundi.Idumu Tanzania na uzuri wake pia kwa afrika yetu.Ni mdau kutoka The Hague.

    ReplyDelete
  2. Chaggas hoyeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  3. aise! naomba niulize: Hii mahela inapatikanaje?

    Juzi j2 niliweka kwenye simu yangu shs 50,000.00 kwa ajili ya kujibu maswali. Nilijibuuuuuu mpaka nikafika mahali wakaniambia nina point 182000. Nikaendelea..si pesa bado zimo? Wakaniuliza tena" je utaweza kukabiliana na changamoto?" hili swali halikuhitaji jibu. Nikaendelea kucheza mpaka point zikazidi 200000. Baadae kimyaaaaaaaa. wakaanza kunitumia swali moja moja kila baada ya muda kama masaa 14 hivi. Sijasikia habari yoyote kutoka voda. Je ni vigezi gani vinatumika mtu kupata ushindi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...