Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama Mama Anna Abdallah (mbele katikati) akifuatilia taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Wengine ni wajumbe wa Kamati hiyo na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa tatu kushoto) akitoa taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Dk. Nchimbi alisema hali ya ulinzi na usalama nchini kimsingi imendelea kuwa shwari isipokuwa kwa matukio machahe yaliyogusa hisia za watu kutokana na kutokuwa ya kawaida katika jamii yetu, na kuwa Serikali inayafanyia uchunguzi wa kina matukio hayo.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...