Raila Odinga na Uhuru Kenyatta wanazidi kushikana makoo katika kinyang'anyiro cha Urais wa Kenya, ambapo hadi saa nne na dakika 35 ni mjimbo 78 tu kati ya 222 yaliyokuwa yansubiriwa. Mshindi hapo lazima apate asilimia zaidi ya 50 ya kura zote. Vile vile mshindi lazima apate asilimia 25 ya kura katika mjimbo yote 47
Kuna kila dalili kwamba hadi leo jioni mshindi atajulikana na kwa jinsi mwenendo wa matokeo ya  kura katika majimbo kibao unavyokwenda, mbio za kuelekea kwenye mstari wa mwisho yeyote kati yao anaweza kushinda.
Saa 4:35 Matokeo jimbo la Jomvu: Kiyiapi 60, Karua 103, Dida 196 Mudavadi 572, Muite 18, Kenneth 285, Odinga 23,221, Kenyatta 7,332
Saa 4:30 Kisauni: Kiyiapi 106, Karua 175, Dida 395 Mudavadi 757, Muite 34, Kenneth 532, Odinga 39,096, Kenyatta 10,894
Saa 4:28  Mvita: Kiyiapi 63, Karua 107, Dida 4,177 Mudavadi 647, Muite 35, Kenneth 1,067, Odinga 34,992, Kenyatta 17,575
Saa 4:23 Mavoko: Kiyiapi 127, Karua 170, Dida 59, Mudavadi 606, Muite 54, Kenneth 547, Odinga 42,285, Kenyatta 15,109.

Hadi hivi sasa msimamo ni kwamba
Uhuru Kenyatta ana 4,812,981
Raila Odinga ana 4,217,845

Wakati huo huo, mgombea wa Chama cha Musalia Mudavadi sasa hivi ameongea na wanahabari na kukubali matokeo kwamba hana matumaini tena ya kushinda na kawatakia heri Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wanaoongoza na kupelekana puta katika dakika hii ya majeruhi. Pia ameweka wazi kwamba yuko tayari kufanya kazi na yeyoye atayeshinda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Blog ya Jamii asante sana kwa updates.Ndivyo uchaguzi wa urais unatavyokuwa kuwa hivi ili nchi iwe na maendeleo.Siyo Uchaguzi haujafanyika mshindi ameshajulikana.


    David V

    ReplyDelete
  2. Kazi ipo!

    Kwa gharama na tekinolojia iliyotukuka ktk Uchaguzi huu sijategemea hadi leo tarehe 8 Machi, 2013 Raisi wa Jamhuri ya kenya hajapatikana wala kujulikana!

    ReplyDelete
  3. Dahhh kwa sakanyoka ya Uraisi iliyotokea nchini Kenya huyo atakayeshinda kwa kweli atakuwa ni mwadilifu saana!

    Kenyatta na Odinga wanatoana kamasi vilivyo!!!

    Atakua na lipi la kujiachia wakati amekipata Kiti kwa mbinde?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...