Home
Unlabelled
KUTOKA MAKTABA: MAMA MARIA NYERERE AKIWA JKT ENZI HIZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mafunzo ya JKT,
ReplyDeleteSawa kabisa, nafikiri watumishi wengi wa Sekta ya Umma wanahitajika kwenda Mafunzoni kwa haraka, pia Sekta Binafsi hasa Mabenki na Makampuni ya Sheria kama Mawakili na zinginezo.
Pia wasisahauliwe watoa huduma muhimu ktk jamii wa Sekta isiyo Rasmi kama wale 'Vishoka' wa huduma za Pasipoti na masuala ya TRA na Mawakala wa Clearing and Forwarding!
Watu hawa watahitajika kwa haraka waende JKT!
ReplyDelete1.'Vishoka' wa Pasipoti na huduma za TRA.
2.Makarani wa Mabenki
3.Madereva wa Mabasi ya Daladala na Makondakta wao
4.Manesi na Wahudumu wa afya
5.Madalali wa sekta zote
Maboda boda na Mabajaji je, wanahitajika kwenda JKT nao?
ReplyDeleteNi wakati muafaka kuwapeleka Mafunzo ya Mujibu wa Sheria ya JKT hawa Wasanii wa Filamu na Miziki ya Kizazi Kipya!
ReplyDeleteNakumbuka Marekani walikuwepo Wanamuziki ambao walipitia Jeshi na walijikuta wanaenda Vitani Iraq mwaka 1991 watu kama Shaggy,Shabba Ranks na Colonel Abraham.
Wabunge wote na wapunguzwe mishahara!
ReplyDeleteSafi sana Mama Maria alikua mfano,sasa hapa naona litakua jambo la maana sana msasa huu uanzie kwenye majumba ya vigogo au? yaani wake wa vigogo nao waonyeshe mfano? au wadau mnasemaje?
ReplyDeletemimi bado sijaona umuhimu wa JKT. Mifisadi yote ninayoijua mimi hapa mjini imepitia JKT na wale waliopitia JKT sio kwamba wana uzalendo zaidi ya wasiopitia. Tunatakiwa twende na wakati, kwa wakati huu nchi yetu inahitaji nguvu kazi yetu kujitolea, sasa kama mtu una miezi kadhaa ya kwenda JKT kwanini tusiunde Volunteer Service ili miezi hio michache watu wakajitolee mashuleni, kwenye ujenzi na vijijini? Vita vya kulenga shabaha karibu vitakuwa historia na wanaovamia nchi zetu siku hizi hawaji kwa mitutu bali wanakuja wamevaa suti na mikataba mkononi na kuchukua wanachotaka!!
ReplyDeleteKwenda JKT sawa lakini baada ya hapo tumejiuliza vijana wasiokuwa na kazi itakuwaje? Tusije kujikuta tunatengeneza majambazi wataalamu wa kutumuia silaha na mbinu za kivita. Tanzania inaweza kuwa nchi tofauti kabisa na ilivyo sasa kama tusipoangalia sula hili kwa umakini.
ReplyDeleteHivi jamani ile operesheni iliyo pass out jana inaitwaje?
ReplyDeleteMdau wa 9 hahahahahaha!
ReplyDeleteOperesheni iliyo Pass Out jana inaitwa 'Kikwete walipue Mafisadi' !
Duru la Pili wanaingia Kambini wote wenye Kesi za Ufisadi na baada ya hapo ni Mahakamani na vifungo!
Lilikuwa ni Kosa kubwa sana kufunga Mafunzo haya mwaka 1994.
ReplyDeletePana Mdau anasema kuwa Mafunzo ya Majeshi bila kuwa na nafasi za Kazi tutazalisha Majambazi waliokomaa kwa ujuzi wa kutumia silaha.
Hivi hajasikia ya kuwa nchi nyingi na Marekani ina Maunzo haya kwa miaka mingi pamoja na tahadhari na hatari ingekuwa Marekani wamefunga kutoa Mafunzo ya Kijeshi ili kueepuka Uhalifu lakini haijafanya hivyo ndio kwanza inazidisha.
Huyo atakaye hudhuria Mafunzo halafu badala yake akafanya Uhalifu pana Mahakama na taratibu za Kijeshi kuwashughulikia.
Pamoja na hatari hizo, Mafunzo ya Kijeshi yanabaki kuwa ni muhimu kwa nchi.
Kumbuka ktk Mafunzo licha ya mengi yanayofundishwa kama Uzalendo unaosema hakuna sasa, makubwa ya muhimu mengine ni pamoja na:
1.Leadership Skills/ Ujuzi wa Uongozi.
2.Civil Protection/ Kuilinda Jamii.
3.Social accountability/ Kuihudumia jamii na majukumu kwa jamii.
Sasa hebu angalia ni Kiongozi gani atakae kuwa hana sifa hizo (3) hapo juu au uelewa huo na akawa Kiongozi mzuri?
Enzi hizo hazitarudi tena. Watu walimaanisha walichokisema. Walikula walichovuna. Waliongoza kwa mfano. Siku hizi ndumilakuwili tu.
ReplyDeletePamoja na kuandika kwa Kiingereza mdau wa Wed Mar 27, 11:07:00 am 2013:
ReplyDeleteNaona wewe badala ya kushabikia JKT ungeshabikia shule, maana mfano wako wa kufafanisha TZ na Marekani unaonyesha jinsi elimu ilivyokupita(common sense).Unaonekana umesoma lakini kumbe labda uliiba vyeti au umetumia cha ndugu. Hizi elimu zinawaumbua hapa hapa tu. Karma ni hapa hapa tu, kudadeki. Na kwa taarifa yako Marekani hawana mafunzo ya kijeshi kama ya JKT. Kijana anakwenda jeshini kabisa na akimaliza muda wake anatafuta kazi nyingine au anabaki jeshini. Na siyo lazima, kijana lazima anajiandikisha akifika miaka 18 lakini toka hapo ni hiari ya mtu kwenda jeshini(selective services). Labda wakati wa vita zamani ndiyo imetokea watu walilazimishwa kwenda jeshini, vitani. Tuwe tunatoa habari kwa maendeleo yetu sote siyo kuchochea kuni ili kujifikishia malengo fulani.