Katibu tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Theresia Mmbando akiwahutubiwa washiriki wa mafunzo ya Uokoaji na Majanga Kutoka taasisi mbalilmbali wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es salaam, kulia ni Meneja Miradi wa Plan International Wilaya ya Ilala Daniel Kalimbiya.
Washiriki wa mafunzo ya Uokoaji na Majanga, wakionesha kwa vitendo jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi, mafunzo hayo yalifanyika Dar es salaam chini ya ufadhili wa Plan International pamoja na Chama cha Msalaba Mwekundu Red Cross.
Mshiriki wa mafunzo ya Uokoaji na Majanga, wakionesha kwa vitendo jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi, mafunzo hayo yalifanyika Dar es salaam chini ya ufadhili wa Plan International pamoja na Chama cha Msalaba Mwekundu Red Cross.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kumbukeni: Amerika iliwajumuishsa akari wa majeshi ya Uganda, Kenya na Tanzania katika uokoaji wa namna hiyo.

    Mafunzo hayo yalifanyika kwa nyakati tofauti kwanza Uganda; halafu Kenya na Tanzania, baadaye.

    Vikosi hivyo vipo tayari kweli?
    Ama zilikuwa ni njama za Amerika kuyafanya majeshi yetu kuwa extensions za uokoaji wa raia wake waliopo kwetu huku?

    ReplyDelete
  2. Mwamerika ni mwingizaji Mkenge mara zote!

    Unakuta zoezi lililokuwa na utata anakabidhi kwa Wafungwa, Wageni ama Wahamiaji!

    Ndio mara kadhaa Amerika imelalamikiwa kuwatumia Wafungwa, Wageni na Wahamiaji ktk majaribio ya Kisayansi hasa kwenye Sekta ya Utafiti wa Madawa na Tiba!

    Mlipata kusikia 'Guinean Pigs'?,,,anayeitwa hivyo ni yeyote binaadamu anayetumika ktk Utafiti wa Kisayansi bila kujali atapata madhara gani!

    ReplyDelete
  3. Hahahah

    Uigizaji wa namna hiyo jamaa aki 'ekti' kama ame athirika na janga, umenikumbusha zoezi moja la Wanahabari pale Hospitali ya Mwananyamala walifika na Maiti ya ku 'ekti' katika gari huku muda wa kupokea maiti ukiwa ume kwisha, ikiwa ni zaidi ya saa 12 Jioni Wana Libeneke walitaka kujua kama Wahudumu wa kupokea maiti wanaweza kuchukua Rushwa?

    Jamaa wakiwasili pale, wakiwa na maiti wao geresha ndani ya gari, Lakini Wahudumu walibumbuluka waka kataa!

    Sasa nikafikiri kwa taratibu za kuhifadhi maiti ni lazima ichomwe sindano za kuzui isiharibike, je endapo jamaa wame chukua mzigo 'rushwa' ingebidi wapige sindano maiti ambayo mtu yungali hai!!!

    Ohhh, nadhani ingebumbuluka kwa kuwa jamaa aliyelala geresha kama amekufa kwenye gari wakati sindano ya DAWA YA MAITI inamkaribia KUDUNGWA MWILINI MWAKE angeruka akala kona na zoezi lingekwama!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...