
Jengo la kituo cha mafuta cha Woco oil kilichokam atwa kwa wizi wa umeme

Mmiliki wa White Parrot hotel na kituo cha mafuta cha Woco Oil vyote vikiwa Korogwe mkoani Tanga anatuhumiwa kutumia umeme wa wizi kwa kuharibu mita nne zilizo katika majengo yake ya hotel na kituo cha mafuta.
Mmiliki huyo anasemekana ndie mmiliki wa kituo cha mafuta cha Woco Oil kilichopo Kongowe, Mkoa wa Pwani, ambacho miezi michache iliyopita alikutwa pia anatumia umeme usiopimwa. Na katika hali isiyotarajiwa imefahamika Woco Oil ya Korogwe ndio wanaoliuzia Shirika umeme Tanesco mafuta kwa wilaya ya Korogwe.
Mhandisi wa Tanesco Francis Maze aliyeongoza operesheni hiyo amesema inasikitisha kuona kampuni inayofnya biashara na Tanesko kuwa ni mmoja ya wahujumu wa shirika. Mauzauza hayo yalikutwa pia katika Hoteli ya Hale, na wamiliki wa hoteli zote hizo hawakuweza kupatikana kwa madai wako nje ya Tanga. Ila bado wanatafutwa
Hale view hotel,imeb ainika inatumiwa umeme wa wizi baada ya kikosi maalumu tooka makao makuu ya Tanesco ikiongozwa na mhandisi Francis Maze kufanya ukaguzi wa mita .
Sehemu ya jengo la Hale view hotel
Mita zilizoharibiwa
Jengo la hotel ya White Parrot na camp site iliyokamat![]() |
Mita iliyoharibiwa Hale View hotel |
Huyu ni Mzoefu! kama mnataka watu wote waache WIZI huu BASI nawashauri huyu jamaa ANYONGWE!
ReplyDeletehuyu bila ya shaka atakuwa mtu wa .................. Hao wizi kwao ni mila
ReplyDeletewafanyakazi wa TANESCO wanahusika kuanzia wahasibu , mameneja wa mikoa hadi vishoka, msijifanye hamjui na wala hilo sio jipya.
ReplyDeleteviongozi wenyewe wezi ije kuwa watumishi wa chini waache waibe tu hiyo nchi kila mtu ale kwa uwezo wa mbinu zake
ReplyDeleteBei ya umeme ni kubwa mno.Mimi namtafuta fundi anikorofishie mita kwani naona gharama za umeme ni kubwa mno wakati raasilimali ya kuzalisha umeme ni bure, Mungu aliumba mito ya kutiririsha maji yanayozalisha umeme. Hata hiyo gesini mali ya Mungu, msituzingue.BEI YA UMEME NI KUBWA MNO.
ReplyDeleteMdau wa Wed Mar 06, 07:08:00 am 2013: Mbona hunatisha? Mtu anyongwe kwa kuiba umeme? Hiyo kali.
ReplyDeleteNakubalina na Mdau wa Wed Mar 06, 11:24:00 am 2013
Kweli Bongo watu wengi ni waizi wa aina fulani na wanokamatwa ni hao wa chini. Yaani kila kitu Bongo nao ujanja fulani. Mie namshangaa jamaa anayesema tuandamane kwenda ubalozi wa Uingereza kumpinga yule mama Mzungu, kwa vile kasema Bongo rushwa ni nje' nje' Ni Ukweli. Tukianza na Uongozi wa Taifa wenyewe una utata na asiyejua chama tawala uchaguzi ulinuka rushwa? Rushwa kwa trafiki, hospitali, Uwanja wa ndege, Mahakamani, mashuleni, michezoni. Ni aibu. Nadhani imekuwa kawaida sasa, yaani watu mpaka hatuoni rushwa ni wizi.
Mbona wamekimbilia mikoani?
ReplyDeleteWamulike hapo Dar,mtakayoyaona mtalia,
Viwanda,magodown,majumba yoote makubwa ya biashara,nk wizi kwa kwenda mbele.
Kuna mtandao mkubwa sana wa wizi.Bila mikakati imara tanesco haina jinsi lazima ife.
Naamini tanesco wakijipanga watagundua "Lakuongezwa ktk maajabu saba ya dunia"