Kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa hapa jijini Dar,maeneo mengi yamekuwa yakijaa maji kutona na miundominu mibovu katika baadhi ya maeneo ya jiji hili.Pichani ni eneo la Mikocheni A,Barabara ya Mwai Kibaki Road jiji Dar es Salaam ambalo ni eneo korofi sana miaka nenda rudi.
Maji yametapakaa kila kona katika eneo hili.
Majiiii..... Majiiii.... Majiii....
hiyo picha ya mwanzo hawakukosea kuandika "my beach"
ReplyDeleteits a shame maji yanajaa hapo wakati bahari is just few meters away
manispaa zimetoa vibali watu wamejenga ktk mikondo ya maji na wameyazuia pa kupita hayo ndio matokeo yake,..na hapo bado...
ReplyDeleteTuwe makini tunavyoandika kwa Kiswahili, yani tupende lugha yetu ya taifa.Maana yake ni kwamba tukiandike kwa ufasaha kwa kutumia lugha yetu ili kufikisha ujumbe bila kuwa na mkorogo.Mfano katika nakala hii mwandishi kaandika hivi: "...barabara ya Mwai Kibaki Road...". Kwa Kiingereza barabara ni ROAD. Ningekuwa miye ningeandika hivi: "...barabara ya Mwai Kibaki...". Tutumie lugha yetu kwa maendeleo ya taifa letu;hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya kudesa.Kila la kheri
ReplyDeleteMafuriko ya mara kwa mara Dar:
ReplyDeleteNi muhimu tewende na wakati huku tikitazama Dunia inavyokwenda, mambo haya mawili ni MUHIMU kuyatilia maanani ili Dar Es Salaam iwe ni mahala panapowezekana kuishi kutokana na kuwa hapa Dar ndio 'reception' ya nchi, huku nchi ikiwa inaamka kwa kasi ya ajabu kwa umaarufu na mafanikio licha ya changamoto kadhaa.
Ni wazi kwa sasa tunatembelewa sana na wageni nchini haswa kwa suala la uwekezaji na uchumi kwa ujumla.
ILI KUIPANDISHA DARISALAMA KUWA NA DARAJA LA JUU TUKAONESHA 'DIFFERENCE' NA TUKAIUZA KWA BEI NZURI MAMBO HAYA MAWILI NI MUHIMU KWA HARAKA:
1.Dar iwe ni kama Venice Italy, kwa kuweka mifereji kila barabara kwa pembeni sambamba na barabara zote kuu, ili mvua ikinyesha watu watumie BOATS , PIA LESENI ZITOLEWE KWA MARA MBILI YAANI MMILIKI WA LESENI YA GARI AWE NA LESENI YA BOTI, PIA VILEVILE MAGARI YOTE YAFUNGWE MAPANGA BOI UVUNGUNI YA KUKATIA MAJI ILI KILA GARI WAKATI WA MAFURIKO LIGEUKE KUWA BOTI NA KU-SWITCH KWA HARAKA KUTOKA KUWA GARI HADI BOTI!,,,HAPA VETA WATAWAJIBIKA KUYABADILI AU KUYAONGEZEA MAGARO MIUNDO MBINU HIYO.
2.Corporate Social Responsibility (CSR) yaani uwajibikaji wa Taasisi na Mashirika kwa Jamii na wananchi usiishie kwenye kutoa misaada ya mabakuli na vyakula Mahospitalini vipindi vya Sikukuu, bali Mashirika na Taasisi yawekeze kwenye huduma za Vioski vya kugawa Makoti ya Mvua na Mabuti (Gun Boots ) za Misaada kwa watu pindi mvua zinaponyesha ma mafuriko yakatokea Jijini Dar. ama pawe na Jitihada za Wajarisiamali kuanzisha vituo hivyo Jijini kwa ajili ya huduma hizo. ambazo wamaweza kutoza ada kidogo ya kujikimu.
NI MUHIMU TULIWEKE JIJI LA DAR KTK HADHI NA HESHIMA NA SIO YANAPOTOKEA MAFURIKO HUKU TUKIWA NA WAGENI JIJINI TUJISIKIE AIBU KUWAPITISHA MITAANI.
HOVYO!!!!!! Halafu mnaendelea kudai eti Bongo tambarare...nyooooo! Hata mitaro tu inatushinda?!
ReplyDeleteBONGO TAMBARAAAAAAREEEEE!
ReplyDeleteHapo Magufuli yupo? Au yeye kazi yake ni kujenga tu barabara bila ya kujali mitalo yake?
ReplyDeleteInasikitisha na ni aibu. Mayor wa jiji anasifiwa sana kwa kazi zake jee hii ya kurekebisha mitaro ya maji wakati wa mvua siyo yake?
ReplyDeleteDar ni mojawapo ya miji iliyokwisha kukosewa, hivyo tufikirie ni jinsi gani tutajenga miji mipya kuendana na mazingira husika na viongozi husika wafanye kazi na wale wenzetu wa chuo cha ardhi katika kupanga hiyo mipya.
ReplyDeleteHii ni hatari kwelikweli nilidhani habari ni jangwani au keko pekee kumbe hata huko. Hii ni dalili inavyoonesha jinsi tulivyoshindwa kuwajibika kwa mambo ya msingi. Hawa watunga sera na watekelezaji wake wako wapi?
ReplyDeleteukweli utabaki kuwa ukweli na hili nasisitiza kama wote hapo juu mlioweka comment naheshimu sana maoni yenu. lakini tukumbuke hili eneo lote hata katika michoro ya master plan ya jiji la Dar es salaam hpakutakiwa kujengwa nyumba wala kuwa makazi ya watu hii ni sehemu ya maji na itaendelea kuwa hivyo hata kama tutakuwa wabishi miaka 100 lakini hapo ni njia ya maji kama ramani za jiji 1962-1969 kama tunabisha basi lakini ukijenga nyumba ni hasara na kila miaka nyumba itadidimia na chumvi ya hapo ni ya milele. ukitaka kujua mengi juu ya THE MSASANI CREEK AND WATER WAY NENDA MAKTABA YA TAIFA HABARI YOTE YA ENEO HILO UTAZIPATA.
ReplyDeletepicha zote labda kasoro moja sijajua wapi ni pale maeneo y mayfair mikocheni.
ReplyDeleteSasa si afadhali kwenda kuishi Mbagala...ha ha ha...hakuna upuuzi kama huu!
ReplyDeleteaaaah mvua popote huleta madhara tu..wakati fulani ailinyesha mvua kwa bibi aka uk mpaka mall kubwa kama ile ya sheffield ilijaa maji so sishangai
ReplyDeleteMdau wa tatu nakubaliana nawe kwa kiasi fulani lakini tatizo linaanza kwa jina lenyewe lilipowa hiyo barabara.
ReplyDeleteJiulize jee hiyo barabara jina lake kamili ni Mwai Kibaki au ni Mwai Kibaki Road? kwa ufupi kibango kimeandikwaje? ikiwa kibango kimeandikwa Mwai kibaki road basi kiasi fulani ni sawa kusema ni barabara ya "mwai kibaki road" kwani hiyo ndio full name ya hiyo barabara.
Kiswahili kigumu jamani!!!!
JAMANI EEEEHHHH KUMBUKENI KUWA DAR IKO UNDER ZERO FROM LEVEL SEA. KWA HIYO UJENZI WA ENEO HUSIKA YAANI MIKOCHENI KULIKUWA HIVYO TOKA ENZI ZA MKOLONI HADI MWISHO WA DUNIA. NIKIWA MSIMAMIZI WA MAJENGO NILISHIRIKI KUWA MSHAURI KATIKA BAADHI YA MAJENGO KWENYE MAENEO HAYO LAKINI WAHUSIKA HAWAELEWI NA WALA HAWATAKI KUSIKIA UKWELI. MATOKEO YAKE NI TUJAZE VIFUSI TUINUWE MSINGI LAKINI MYAKA IJAYO MAJUMBA MENGI YATATELEMKA HUENDA TUKAWA TUMESHAAPITA, YAANI KUIGA DUNIA.
ReplyDelete