Tarehe 10/04/2013 taasisi ya wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Morogoro
(WAVUMO) ambayo ni shirika lisilo la kiserikali na lisilotengeneza
faida, waliandaa harambee kwa maendeleo na kutoa elimu juu ya ugonjwa
wa Ukimwi kwamba Ukimwi sio tatizo la Afya tu bali linahusu maendeleo
ya Jamii kwa ujumla. Harambee hiyo yenye nia ya kujikwamua badala ya
kutegemea wafadhili kutoka nje iliweza kufanikiwa kupitia watu na
jamii mbalimbali ya Morogoro kutokana na mioyo yao mizuri na kwa
michango yao. Mgeni rasmi alikuwa Mh. Mkuu wa Mkoa aliyewakilishwa na
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Manispaa Mheshimiwa SAID AMANZI.
Shirika ili la Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Morogoro (WAVUMO) pia liliandaa chakula cha usiku katika kufanikisha harambee hiyo. kauli
mbiu ilikuwa, "MLO WA JIONI KWA KUOKOA MAISHA / A DINNER A LIFE
SAVED".
Harambee hii ilifanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha 11,000,000/=,
mradi wa soda kreti 15, friji kubwa, meza mbili na viti nane kutoka
pepsi, vilevile ilifanikiwa kupata plot za Ardhi kwa ajili ya mradi wa kilimo cha
umwagiliaji cha mpunga ambacho kitakuwa kinaendelea kutunisha mfuko
wa WAVUMO.
Shirika la WAVUMO linawanachama zaidi ya 500 na linahudumia wagonjwa
wa Ukimwi zaidi ya 3000 kwa manispaa ya Morogoro. Shirika lina miaka
12, kwa sasa linaongozwa na Mwenyekiti Bw. Ally Ramadhani.
Kwa maelezo zaidi kuhusu harambee hii na taasi ya WANAOISHI NA VIRUSI
VYA UKIMWI MOROGORO (WAVUMO), Wasiliana nao kupitia +255 714 255 688,
au +255 767 245 688.
Zoezi la Harambee likiwa limefunguliwa rasmi na Mgeni rasmi, kutoka kulia ni Mratibu wa Harambee, Mourine-Hawa Msangi na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Manispaa Mheshimiwa SAID AMANZI.
Mr. Signfrid Kayombo na Mr Mujungu Wajama ambao ni Wawakilishi kutoka TUNAJALI wakiotoa mchango wao.
Mr. Juma Ayoub Bitagera kutoka NIC akitoa mchango wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...