Mheshimiwa
Spika, naomba kutoa Hoja kwamba kutokana na Taarifa zilizowasilishwa
leo na Wenyeviti wa Kamati za Katiba, Sheria na Utawala; Kamati ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa; na Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati
ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya ndani ya Bunge lako Tukufu ambazo zimechambua
Bajeti ya Mafungu ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili
Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2012/2013 na
Mwelekeo kwa mwaka 2013/2014.
Vilevile, naliomba Bunge lako Tukufu likubali
kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Taasisi zilizo chini yake
pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2013/2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...