Baada ya Maji kupungua katika eneo la Chipite ambalo lilijaa maji na
kusababisha Abiria zaidi ya 500 na Magari zaidi ya 200 kushindwa
kupita eneo hilo na Kufanya gari nyingi ziendazo na Kutoka
Mtwara,Masasi,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Liwale,Nanyumbu na Tunduru
kufanya safari kwa kuzunguka wilaya ya Newala sasa hali imeanza
kubadilika na gari nyingi kuanzia jioni zimeanza kupita ingawa kwa
Mashakamashaka ili kusaidia kupeleka na kutoa huduma kwa Jamii
Kufuatia hali hiyo.
baadhi ya wasafiri waliokwama wametupia lawama kwa
Wakala wa Barabara Tanroads na Kitengo cha Maafa kutotoa Ushiriakiano
wowote kuhakikisha Abiria wanakuwa salama ikiwa pamoja na
kutafuta jitihada za haraka kuwavusha ili kuepusha Maafa
yatakayochangiwa na uwepo wa msongamano kwa muda mrefu
Hali ya usafiri sasa iko kama kawaida kuelekea katika wilaya Tajwa hapo Juu.Picha na Mdau Abdulaziz Lindi.
Miye nashindwa kuelewa TANROADS wanafanya nini? Kwa sababu kama inafahamika kwamba kina cha maji kinafikiaga hichi hapa pajengwe daraja ambalo halitakuwa na uwezekano wa kuathirika na angalau kiwango hicho cha maji. Tatizo hili laweza kuikumba barabara ya kilwa ukitokea mtoni mtongani kuja mbagala misheni. Tujitahidi Watanzania wenzangu kutatua matatizo wenyewe scientifically bila kusibiri wahisani. La sivyo ukoloni waja tena kwa sura nyingine....
ReplyDeleteKhah! Nakubaliana kabisa nawe Anony wa kwanza. Pia mie kinachonishangaza nilisikia Daraja la Mkapa ndio suluhu ya tatizo hili, duh sasa vp limepita wapi au wamelichenga hili eneo? Hebu naomba kuwauliza nyie TANROADS hivi hamuwezi kufanya kama pale kwa Mtogole-Tandale, DSM. Pale palikuwa korofi sana, sijui ni ninyi au Manispaa naona wametengeneza mlima yaani sasa hivi maji yanapita naona bila wasiwasi. Poleni ndugu zetu.
ReplyDeleteNatumaini hawa wanaopita kwa mguu wanajihadhari na mamba maana hapo mamba ni wengi. Tuombe Mungu awaepushie!
ReplyDelete"Chipite" ina maana usipite!
ReplyDelete