Baada ya Maji kupungua katika eneo la Chipite ambalo lilijaa maji na kusababisha Abiria zaidi ya 500 na Magari zaidi ya 200 kushindwa kupita eneo hilo na Kufanya gari nyingi ziendazo na Kutoka Mtwara,Masasi,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Liwale,Nanyumbu na Tunduru kufanya safari kwa kuzunguka wilaya ya Newala sasa hali imeanza kubadilika na gari nyingi kuanzia jioni zimeanza kupita ingawa kwa Mashakamashaka ili kusaidia kupeleka na kutoa huduma kwa Jamii Kufuatia hali hiyo.

 baadhi ya wasafiri waliokwama wametupia lawama kwa Wakala wa Barabara Tanroads na Kitengo cha Maafa kutotoa Ushiriakiano wowote kuhakikisha Abiria wanakuwa salama ikiwa pamoja na kutafuta jitihada za haraka kuwavusha ili kuepusha Maafa yatakayochangiwa na uwepo wa msongamano kwa muda mrefu Hali ya usafiri sasa iko kama kawaida kuelekea katika wilaya Tajwa hapo Juu.Picha na Mdau Abdulaziz Lindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Miye nashindwa kuelewa TANROADS wanafanya nini? Kwa sababu kama inafahamika kwamba kina cha maji kinafikiaga hichi hapa pajengwe daraja ambalo halitakuwa na uwezekano wa kuathirika na angalau kiwango hicho cha maji. Tatizo hili laweza kuikumba barabara ya kilwa ukitokea mtoni mtongani kuja mbagala misheni. Tujitahidi Watanzania wenzangu kutatua matatizo wenyewe scientifically bila kusibiri wahisani. La sivyo ukoloni waja tena kwa sura nyingine....

    ReplyDelete
  2. Khah! Nakubaliana kabisa nawe Anony wa kwanza. Pia mie kinachonishangaza nilisikia Daraja la Mkapa ndio suluhu ya tatizo hili, duh sasa vp limepita wapi au wamelichenga hili eneo? Hebu naomba kuwauliza nyie TANROADS hivi hamuwezi kufanya kama pale kwa Mtogole-Tandale, DSM. Pale palikuwa korofi sana, sijui ni ninyi au Manispaa naona wametengeneza mlima yaani sasa hivi maji yanapita naona bila wasiwasi. Poleni ndugu zetu.

    ReplyDelete
  3. Natumaini hawa wanaopita kwa mguu wanajihadhari na mamba maana hapo mamba ni wengi. Tuombe Mungu awaepushie!

    ReplyDelete
  4. "Chipite" ina maana usipite!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...