Familia ya Mzee George P. Mapango na Marehemu Mwashaban A. Liganja tunatoa shukrani zetu kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kwa kutufariji katika msiba wa mpendwa wetu MARIA G. MAPANGO aliyefariki tarehe 04 Machi, 2013 na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni hapa Dar es Salaam tarehe 06 Machi, 2013.

Shukrani za pekee ziwafikie wafuatao, Mke wa Rais wa Awamu ya Pili, Bibi Siti Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, Mkurugenzi na Wafanyakazi wa Inter-Consult Ltd., Bwana Jonas Masabala, Katibu Mkuu Kiongozi, (Mstaafu),Bwana Phillemon L. Luhanjo na Mama Luhanjo, Katibu Mkuu, Ikulu, Naibu Katibu Mkuu, Ikulu, Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu, Wafanyakazi Ofisi ya Rais, Mapadre wa Kanisa la ST. JOSEPH, Marafiki wa Marehemu Mwashaban A. Liganja, Majirani Ocean Road Flats, Madaktari na Manesi Wote waliokuwa wanamhudumia Maria (IA) katika Hospitali ya Emilio Mzena, Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi J.K. Nyerere, Shaaban Robert High School, Al-Muntazir High School, Jumuiya ya Ocean Road na Ndugu, Jamaa na Marafiki

Tarehe 13 Aprili, 2013 kutakuwa na mkesha wa Kisomo na tarehe 14 Aprili, 2013 saa 04.00 Asubuhi kutakuwa na misa ya Shukrani ambapo shughuli zote zitafanyika nyumbani kwao Ocean Road Flats. Karibuni

“RAHA YA MILELE UMPEE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI - AMINA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Such a beautiful soul, Allah amlaze pema peponi Amin, Gone too soon, simjui lakini nimeumia

    ReplyDelete
  2. Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, R.I.P Mjomba Maria. Mbele yako nyuma yetu..... Amen!

    ReplyDelete
  3. Tunakupenda sana. Haupo nasib katika mwili lakini tunaamini Roho zetu zitakuwa pamoja milele na milele. Mungu akupe pumziko la Amani. Amina.
    Dachu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...