Kandarasi wa ujenzi wa mradi kisima cha maji kilichofadhiliwa na
kampuni ya bia Tanzania TBL .Godwin Kalaghe wa kampuni ya Dr Gogo
engineering limited ya jijini Dar es salaam akimkabidhi mkurugenzi wa
mahusiano na sheria wa TBL Stephen Kilindo taarifa za kukamilika kwa
mradi huo.
Mradi wa kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania
katika kijiji cha Makanya wilayani Same chenye thamani ya shilingi
milioni 51.6.Uwepo wa kisima hiki utasaidia kupunguza tatizo la maji
hususani kwa wakazi wa Tambarare katika wilaya ya Same.
Mkurugenzi wa mahusiano na sheria wa kampuni ya bia Tanzania TBL
Stephen Kilindo akisaidia kumbebesha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha
Makanya Asia Zuberi kuashiria uzinduzi wa mradi wa kisima hicho cha
Maji.
MAJI NI BREWERIES LTD
ReplyDelete