Hawa ndio watu watatu kati ya wanne wanaoonekana katika picha ya hpo chini. walibeba vibuyu vyenye udongo  wa Tanganyika na Zanzibar na Chungu kilichotumika na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuchanganyia udongo huo ambapo mara baada ya zoezi hilo ndipo jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi miaka 49 iliyopita. Kutoka kushoto ni Mama Sifaeli Chuma aliyebeba kibuyu chenye mchanga wa Tanganyika, akifuatiwa na Bw. Omar Hassan Mzee aliyebeba chungu kikubwa na Bi Khadija Rajabu Abbas aliyebeba kibuyu chenye udongo wa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. nina hakika wanatunzwa vyema katika maisha yao kama kupatiwa huduma nzuri na kusaidiwa katika hali ya kimaisha

    isijekuwa wametelekezwa kama alivyotelekezwa aliepandika mwenge juu ya mlima kilimanjaro na kuja kukumbukwa wakati hali yake ishakuwa mbaya na kukata roho.

    ReplyDelete
  2. Ayayepinga Muungano:

    Na apinge kwa kutuhakikishia na kwa hoja na kwa vitendo kwa:

    1.Kuutenganisha udongo uliochanganywa wa pande mbili kama ataweza kuutenganisha kipande cha mchanga hadi kipande.

    2.Atuhakikishie kama atakuwa ameupata mchanganyiko sahihi wa huo udongo, kama atamudu kuupata kiukweli.

    3.Kwa zile familia zenye wazazi mchanganyiko Bara na Visiwani, huyo mpinga Muungano atenganishe vizazi hivyo kama ni watoto walizaliwa atenge wasiwe na mchanganyiko wa wazazi Bara na Visiwani.

    Mpinga Muungano kama ataweza hayo yote matatu (3) nadhani hatuna shaka TUTAOMBA UN iuvunje Muungano!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...