Hawa ndio watu watatu kati ya wanne wanaoonekana katika picha ya hpo chini. walibeba vibuyu vyenye udongo wa Tanganyika na Zanzibar na Chungu kilichotumika na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuchanganyia udongo huo ambapo mara baada ya zoezi hilo ndipo jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi miaka 49 iliyopita. Kutoka kushoto ni Mama Sifaeli Chuma aliyebeba kibuyu chenye mchanga wa Tanganyika, akifuatiwa na Bw. Omar Hassan Mzee aliyebeba chungu kikubwa na Bi Khadija Rajabu Abbas aliyebeba kibuyu chenye udongo wa Zanzibar.
Home
Unlabelled
TOKA MAKTABA YA GLOBU YA JAMI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nina hakika wanatunzwa vyema katika maisha yao kama kupatiwa huduma nzuri na kusaidiwa katika hali ya kimaisha
ReplyDeleteisijekuwa wametelekezwa kama alivyotelekezwa aliepandika mwenge juu ya mlima kilimanjaro na kuja kukumbukwa wakati hali yake ishakuwa mbaya na kukata roho.
Ayayepinga Muungano:
ReplyDeleteNa apinge kwa kutuhakikishia na kwa hoja na kwa vitendo kwa:
1.Kuutenganisha udongo uliochanganywa wa pande mbili kama ataweza kuutenganisha kipande cha mchanga hadi kipande.
2.Atuhakikishie kama atakuwa ameupata mchanganyiko sahihi wa huo udongo, kama atamudu kuupata kiukweli.
3.Kwa zile familia zenye wazazi mchanganyiko Bara na Visiwani, huyo mpinga Muungano atenganishe vizazi hivyo kama ni watoto walizaliwa atenge wasiwe na mchanganyiko wa wazazi Bara na Visiwani.
Mpinga Muungano kama ataweza hayo yote matatu (3) nadhani hatuna shaka TUTAOMBA UN iuvunje Muungano!