Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akiwapungia maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Kasarani,jijini Nairobi Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete,Mabalozi na watu wengine mbalimbali.Picha zote kwa hisani ya Mike Kariuki wa Capital FM.
Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akisoma hotuba yake mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika ndani ya uwanja wa Kasarani,Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais wa nchi mbalimbali ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria.
Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Makamu wake William Ruto.
Rais Uhuru Kenyatta akila kiapo cha Urais,kuwa rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofana kwa kiasi kikubwa ndani ya uwanja wa kasalani.
Rais wa Uganda,Mh Yoweri Kaguta Museven akisoma hotuba yake fupi wakati wa kuapishwa kwa Rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofanyika ndani ya uwanja wa Kasalani,jijini Nairobi.
Tuwekee comparison na Kiapo cha Moi mwaka 2007
ReplyDeleteKwanini mnachanganya matumizi ya herufi "L' na 'R", ankal mara nyingi waandishi wetu hawako makini wanapotamka au kuandika neno Kujiuzulu wanasema Kujiuzuru, au kama ulivyosema hapo ankal KASALANI badala ya KASARANI. Je hiyo ni effect ya mother tongue au overdose ya Kiswahili?
ReplyDeleteThis is not fare michuzi ongeza picha
ReplyDeletewatanzania mngeijua histori ya chaliiiiii mngeshanga mafisadi daima wanakwenda mbele
ReplyDeleteShule jamani!, THIS IS NOT FAIR siyo 'this is not fare' kama huyo anonymous hapo juu.Walimu aheni mgomo na msipotoshe watoto au ninyi pia ni vilaza??????
ReplyDeleteKaka Hapo Juu matumizi ya L & R nakuunga mkono kabisa yaani ni aibu kabisa kwa Waandishi wa habari ambao hushindwa kutofautisha L na R, wengine ni wanamuziki wa bongo fleva yaani wale ndo mwisho kabisa kwa kuharibu kiswahili.
ReplyDeleteBAKITA mko wapi!!
Mlomry