Hapa ni katika makutano ya barabara za Jamhuri na Azikiwe Avenue katikati ya jiji la Dar es salaam. Baada ya wajuaji kupora mfuniko wa chemba ya maji taka limebaki bonge la shimo katikati ya barabara na wasamaria wema wameweka jiwe la msingi ili kukutahadharisha na mradi huo ambao kila baada ya muda unatema maji taka yanayonukia si mchezo. Hii ni wiki ya nne sasa shimo hilo na mengine kadhaa pembeni yanakenua tu....


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hivi hao wanaopokea mifuniko hiyo na kuinunua, wana akili sawa? Ni sawa na mtu anayenunua cheni, saa, nk nk vya wizi. Ningekuwa serikali ningefunga viwanda vya vyuma chakavu vyote wapate adabu. This is vandalism. Na inaendelea for decades, serikali imelala usingizi.

    ReplyDelete
  2. Na mimi naungana na mdau wa kwanza hapo juu,naongeza kwa kuvilaumu vyombo vyetu vya dola(polisi na usalama wa Taifa),ni wajibu wao kumtafuta na kumkamata huyu anayenunua mifuniko na vyuma vingine chakavu.Atafutwe akamatwe huyu 'mnunuzi' wa hii mifuniko na afunguliwe makosa ya uhaini.Nilisoma Gazeti la Daily News majuzi, eti TBS wanakamata wanaouza Nondo FAKE!Kamata viwanda vinavyotengeneza nondo feki fungia.Finish

    ReplyDelete
  3. Wee vipi ufunge viwanda, jaribu uone hizi biashara za watu tena wana nguvu mfano hakuna. Leta mdomo mdomo wako likikutokea la kukutokea usije ukalaumu mtu buree.

    ReplyDelete
  4. mimi naona tujaribu kutafuta teknologia ya kutengeneza hivi vifunkio kwa "material" tofauti badala ya chuma.Hivyo basi hao wezi hatakuwa na sababu ya kuvichukua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...