CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAWI LA
UNITED KINGDOM.
Website:
www.ccmuk.org,
ccmuk.org/blog, Facebook – chama cha mapinduzi uingereza, Twitter CCM UK.
CCM UK INAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KUPINGA VIKALI KITENDO CHA KIGAIDI KILICHOTOKANA
NA ULIPUAJI WA BOMU KANISA KATOLIKI LA OLASITI JIJINI ARUSHA.
Uongozi na wanachama wa
Chama Cha Mapinduzi Tawi la Uingereza tunapenda kuungana na Watanzania wote wapenda
amani katika kuwapa salamu zetu za pole Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la
Olasiti jijini Arusha , kutokana na tendo shambulizi la kigaidi la kutupwa bomu
kanisani hapo lililosababisha Watanzania Wawili kupoteza maisha na zaida ya 60
kujeruhiwa.
CCM UK siku zote inawausia
Watanzania kulinda Amani yetu na kushikamana kwa pamoja wakati wa kufanya hivyo
bila ya kujali tofauti zetu za kiitikadi , kabila , rangi wala siasa .
CCM UK tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa Mwenyekiti
wetu wa Taifa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa
kuongoza kwa mfano bora pale alipokatiza Ziara ya muhimu nchini Kuwait na
kurudi Nyumbani kwa haraka ili awe pamoja na Wananchi wake katika kuomboleza na kukemea vikali shambulio hilo lililofanywa na
mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na
watu wake.
Aidha CCM UK inaishukuru Serikali na Vyombo Vya Dola kwa
hatua za haraka zilizochukuliwa katika kutafuta wahusika wa tukio hili la
kinyama na lisilo na msingi na kuwaomba watanzania kuwa watulivu
wakati huu na kuviachia vyombo vya dola kufanya kazi yake na kuchukua tahadhari
juu ya watu waovu wanaotaka kuwavuruga na kuwafarakanisha kwa misingi ya dini. .
CCM UK inatoa salamu za pole na kuwafariji familia za wale wote waliopoteza Maisha yao na kuwaombea majeruhi
wote walioumia katika tukio hili
wapate nafuu ya haraka na waendelee na
shughuli zao za ujenzi wa taifa.
Imetolewa na Idara ya
Itikadi, Siasa na Uenezi
CCM
- UNITED KINGDOM .
Poleni sana mliopatwa na janga tupo pamoja kama taifa na umoja wetu sote. Tunakemea kitendo cha kigaidi ni dhahiri kwamba vyombo husika vitafanya uchunguzi wa kina kujua ni nani au akina nani wamehusika katika kutupa bomu hilo. Nawapa pole nyingi wafiwa na kuwatakia majeruhi wote wapate nafuu ya haraka na kurejea katika utendaji wao wa kila siku. Mungu Ibariki Tanzania
ReplyDeleteKitendo hiki ni cha kinyama kabisa na hatuna budi Watanzania sote kuungana na vyombo husika ilikuwapa wale wote waliohusika na unyama huu. Vile vile natoa mkono wa pole kwa wafiwa pamoja na kuwatakia uzima wa haraka kwa walio jeruhiwa. Tulinde amani yetu kwani hii ni raslimali ya aina yake kwa dunia ya leo.
ReplyDeleteSalamu toka Northampton,
Kitendo hiki cha kinyama si utamaduni wetu watanzania tunaungana nanyi kukemea vikali tukio hili na hatua kali zichukuliwe ili iwe mfano na mtu yeyote asije dhubutu chezea utulivu wa Tanzania yetu.
ReplyDeleteMungu Ibariki Tanzania
Mdau Luton - Uingereza