Mdau nimeletewa lalamiko toka kwa Kaka yangu Hashimu Tambala (pichani) wa Manispaa ya Lindi  kama ifuatavyo-Namnukuu akilalamika kwangu Nimelipia gharama zote zinazotakiwa Januari 14,2013 ili kuunganishiwa
Umeme lakini hadi leo 17 May 2013 soli yangu ya viatu inaishia kwa safari lukuki za kwenda TANESCO bila mafanikio. 

Sijui nimwombe nani ili nipate huduma ya Umeme wakati Taratibu zote nimefuata? Naomba nisaidiwe kupitia blog hii Tafadhali!

Na Mdau Abdulaziz Video

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2013

    kuna gharama moja muhimu sana bado; kalipe la sivyo utakaa giza hadi kiama; saa hii kilio hakisaidii tena, kalipe!!! kama unaona kulipa haiswihi basi unaweza kutengeneza kaumeme kako mwenyewe!! kalipe acha kulialia, ***

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2013

    Mimi pia nililipia tangu Februari 14 lakini bado sijaunganishiwa. Kuna tatizo la ukosefu wa nguzo TANESCO kwa sasa. Kama kazi yako inahitaji nguzo hilo linaweza kuwa ndilo tatizo.
    Mdau hapo juu acha kuhamasisha rushwa. Gharama moja muhimu unayotaka kusema ni ipi? Kwa taarifa nilizopata TANESCO ni kwamba wateja wa kuanzia January baada ya punguzo la gharama za kuunganisha umeme hasa wale wanaohitji nguzo kadhaa wamekumbwa na tatizo hili.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2013

    TANESCO hainabudi kuvunjwa. Ipatiwe washindani na wengine wapewe fursa ya kutoa huduma hiyo. Matatizo sio ya uzalishaji bali ni ya ukiritimba ambao hauna uzoefu wa huduma kwa wateja. Wanadhani huduma bora ni kujitangaza kwenye radio na tv kama mkakati wa kuficha udhaifu wao. Ni kioja na watu na akili zao wanafanya kazi hiyo kurubuni wananchi. Tujaribu njia ya kulivunja na mikoa ama kanda kuwa huru ili uzalishaji uweke kipaumbele katika kusambaza kwenye kanda hizo ambazo zitanunua na kuuza na kuhudumia wateja wake. Njia nyingine ni kuanzisha mashirika tofauti ya uzalishaji na usambazaji kwa wateja. Haya mawazo hawezi kuyapata TANESCO. Nchi zilizoendelea nyingi hazikutegemea shirika moja kama sisi ambao tumewaruhusu wajenge ukiritimba, wizi, huduma mbovu bila uwajibikaji wakati wakiendelea kudai ruzuku kutoka Serikalini!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Kweli matatizo ni ya ukiritimba...Mimi nimelipa toka machi, nimeambiwa WIRE wa mita 85, wa kutoa umeme kwenye nguzo hadi kwemye nyumba yangu hakuna. Sasa jamani TANESCO, au UMEME bila wire...halafu linaitwa shirika hai hapana, hapana, hapana. Mambo ya Nguzo, sijui Mita, sasa wire hakuna, sisi hatuhitaji kusikia. Tanzania bila TANESCO inawezekana bwana kha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...