Kaka, 
Minaki Pamechoka. Nasikitika. The original structure hawaitunzi... 
It needs restoration!  - MDAU




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2013

    Akhsante sana Mdau kwa picha hizi, kwa kweli umenikumbusha mbali saana, shule yangu Minaki, ni kweli ipo choka mbaya, bwalo silioni, na bweni langu makongoro, wapi kinyanyiko, au trip za downtown kiwe kuhudhuria ngoma za kizaramo mwali kutoka na nyimbo kama vile, "Mjomba kumbe tapeli, kafika njiani kaniomba, kafanya kweli...." au "Naona tabu mie, naona tabu mie , naona tabu mie".
    Enzi za "kiburungutu", Mkorogo etc.
    Sweet good memories.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2013

    Hii shule nilihamia 1992 wakati niko Form V majengo yalikuwa katika hali mbaya hivi hivi! Kulikuwa na H/master akiitwa Mtesigwa. Mtesigwa alikuwa ameiacha shule ijiendeshe yenyewe. Huku yeye akitumia muda wake kufaidi ulabu. Leo ni miaka zaidi ya 20 imebaki vile vile! Kweli vipaumbele vyetu vimepinda. Kulikuwa na mashamba makubwa. Kazi kubwa ilikuwa ni kulima hayo mashamba badala ya kusoma. Maji tulikuwa tunatembea umbali mrefu kwenda kuchota na kuoga bwawani. Chakula kilikuwa ugali na maharage kwa muhula mzima. Ukweli ni kwamba nililazimika kuhama tena kutoka Minaki kabla ya kumaliza A-level.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2013

    Duuu

    1.Huduma mbovu za Elimu,
    2.Kuporomoka Kiwango cha Elimu,

    hayakuanza leo, bali vimekwenda taratibu vikididimia siku hadi siku hadi Meli inazama tunakuja kustuka ni Matokeo ya Mitihani Kidato cha 4 mwaka huu 2013.

    Mambo hayo mawili (2) hapo juu ''NI WAZI YATAKUWA NA MADHARA MAKUBWA SANA KWA MUSTAKABALI WA TAIFA NA WANANCHI KWA UJUMLA.

    KWA sababu, kazi uifanyayo inaakisiwa na Kiwango cha Elimu uliyoitapa, sasa kama umepata Elimu ya kubahatisha huku ukikabiliana na Ushindani kutoka kwa walio elimika vizuri (WEZNETU KTK AFRIKA YA MASHARIKI NA DUNIA KWA UJUMLA)wewe JANGALA utaambulia nini hapo?

    Pia MAMLAKA ITAPATA CHANGAMOTO ITAKAPOHITAJI NGUVU KAZI (WALIO ELIMIKA) UWA WATUMISHI KTK TAASISI ZAKE, MASHIRIKA NA IDARA PAMOJA NA SEKTA BINAFSI, NI WAZI PATAKUWA NA PENGO KUBWA LA (I)Ubora wa Viwango (II)Idadi wa wanaohitajika. yaani FISCAL GAPE/ FISCAL DEFICIT ktk Uchumi.

    Ni janga kubwa nchini sasa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2013

    serikali irejeshe shule hii kwa wamissionary wenyewe bado wanaitaka

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2013

    jamani hilo jengo ni zamani na halitumiki ni kama makumbusho tu ,ila kuna madarasa saafi na mbweni mnyapara, shabani mrobert, makongoro, lumumba, mirambo na nyerere

    ReplyDelete
  6. Lol....utafikiri Malecela na Kigoda hawakusoma hapo.....Mie nimemalisha hapo 2005 na hali ilikuwa hivyo hivyo. Tangu wajenge wa-missionary hakuna cha maana kilichofanyika kwenye hii shule. Lakini hata viwanda walivyotuachia wakoloni navyo si tuliua? kwahiyo ni kawaida yetu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 18, 2013

    mimi nadhani ni vema kwa wadau walipitia hapo shuleni kuorganize na kufanya support angalau kidogo.Kama walivyofanya Jiteute, Azania naskia nao wapo mbioni kuorganize reunion kwa ajili ya kuifufua shule yao,ni uzalendo na shukrani ya fadhila kurejesha katika jamii.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2013

    Hebu tuletee pia picha za majengo ya tambaza tafadhali

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 19, 2013

    Such a beautiful place, wonderful German setting, this could be one of the best schools in Tanzania, we need to do something about it, we cant just leave it like that..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...