Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited
(TDL), David Mgwassa (kushoto) akifafanua jambo katika semina ya wajumbe
wa Kamati mbili za Bunge za Uchumi,Viwanda na Biashara pamoja na
Kilimo,Maji na Mifugo kuhusu baadhi ya vyombo vya habari vyenye uhusiano
na nchi jirani vinavyotumika kupiga vita viwanda vya ndani kikiwemo cha
Konyagi. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited
(TDL), David Mgwassa, akionesha kinywaji cha Afrika Kusini kilichofungwa
kwenye viroba kama ambavyo Konyagi inafanya hapa nchini.Vinywaji kama
hivyo vipo karibu nchi nyingi Ulimwenguni.
Meneja wa Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe akielezea jinsi vinywaji vyao vinavyochangia mapato ta serikali
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo, Said Nkumba
akichangia mada hiyo kwa kuviasa baadhi ya vyombo vya habari kuacha
kuandika habari za kudidimiza viwanda vya haba nchini. Kulia ni Idd
Azzan Mbunge wa Kinondoni na Dunstan Kitandula ambaye ni Makamu
Mwenyekiti was Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...