Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
ZAIDI ya wakazi 1000 katika vijiji vya Chekereni, Mijongweni, Weruweru
na Kiyungi wilayani Moshi vijijini inadaiwa wameathirika baada ya
kutumia maji ya Mto Karanga yanayodaiwa kuwa na zinazotiririshwa
kutoka kwa baadhi ya viwanda vilivyoko kando ya mto huo.
Mbali na athari hizo za kibinadamu pia mifugo inadaiwa kuathirika
kutokana na kunywa maji hayo ambayo wakazi wa maeneo hayo wamekuwa
wakiyatumia kwa shughuli za kufulia, kuogea na kunyweshea mifugo hasa
kipindi cha kiangazi.
Uchunguzi uliofanywa katika mto huo umebaini mbali na kemikali hizo ambazo
zimekuwa zikitiririshwa kwa wingi toka katika viwanda hivyo, pia
shughuli za kilimo zinazoendelea pamoja na ujenzi ambao haukuzingatia
sheria za mazingira zinachangia uchafuzi wa mto huo.
Shughuli nyingine ambazo zinachangia uchafuzi wa mto huo ni pamoja na
wakulima wa karoti ambao wamekuwa wakiendelea na shughuli za kuosha
zao hilo jirani kabisa na daraja la Bonite kabla ya kusafirishwa
kwenda kwenye masoko ya ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro.
Wakizungumza na waandishi wa habari ,Azama Ally mkazi wa kijiji cha Weruweru na
Lusia Lucas mkazi wa kijiji cha Mijengweni wamesema maji hayo yamewaathiri kwa
kupatwa na magonjwa ya upele,kukohoa kutokana na kuvuta hewa sanjari
na kuumwa Macho kutokana na kutumia maji hayo kwa kufulia na kuogea.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Bombani katika kijiji cha
Chekereni/Werurweru, Leonard Munishi, amekiri kuwepo kwa hali hiyo
huku akisema uchafuzi wa mazingira katika eneo hilo ni wa hali ya juu
na kwamba wamebaini kuwa kemikali hizo zinatoka katika viwanda
vilivyoko kando ya mto huo.
Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Relini, Sadick Kubingwa, amesema kwa
zaidi ya miaka 15 sasa maji hayo yamekuwa yakitiririka katika mto huo
na kwamba yamechangia pia kwa kiwango kikubwa kuwepo kwa magonjwa ya
milipuko katika vijiji hivyo.
Shughuli za uoshaji wa Karoti zikiendelea kando ya mto Karanga,shuguli ambayo pia inatajwa kuwa chanzo cha uchafuzi wa mto huo ambao maji yake yanatumiwa na wakazi wa vijiji vya Chekereni,Mijongweni,Weurweru na Kiyungi wilaya ya Moshi vijijini.
Maeneo ambayo maji yenye kemikali kutoka viwandani yakiingia mto Karanga ,maji ambayo yanadaiwa kuwaathiri wakazi wa vijiji vya Chekereni,Mijongweni,Weruweru na Kiyungi wilayani Moshi vijijini.
Mmoja wa wakaz wa kijiji cha Chekereni akifua nguo kando ya mto Karanga ambao unaidaiwa maji yake yanawaathiri wakazi wa vijiji vilivyoko kando ya mto huo.
Hawa wa Karoti wakaoshee wapi? Serikali mmetenga miundo mbinu kuwawezesha hawa wakulima wadogo wadogo kutunza mazingira? Tumia Kodi kwa wananchi kumjenga mwananchi
ReplyDeleteBado wanachafua tu bwana, hiyo ya kwenda kuoshea wapi ndio njia inayopaswa kutafutwa na kila mwanajamii au kupendekeza ili serikali iigharimie, kulalamika tu!
ReplyDeletesesophy