Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake.  Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'

HABARI ZILIZOPOKEWA USIKU HUU NI KWAMBA MAMA YAKE MZAZI MSANII MAARUFU WA MUZIKI NCHINI, JOSEPH HAULE A.KA. 'PROFESA J' AMEFARIKI DUNIA USIKU HUU BAADA YA KUGONGWA NA GARI  MAENEO YA MBEZI JUU, JIJINI DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA ANAISHI NA MWANAE.

HABARI ZINASEMA MAREHEMU, BI. ROSEMARY MAJANJARA HAULE, ALIGONGWA NA GARI AKIWA ANAVUKA BARABARA KUELEKEA DUKANI KIASI CHA SAA MBILI USIKU, NA KWAMBA BAADA YA KUGONGWA WASAMARIA WEMA WALIMKIBIZA HOSPITALINI TUMBI KWA KUTUMIA BAJAJI AMBAKO ALIFARIKI DUNIA. TAARIFA ZA AWALI HAZIJATAJA AINA YA GARI NA KAMA BAADA YA AJALI HIYO LILISIMAMA AU LA.

PROFESA J AMETHIBITISHA  HILO MUDA MFUPI ULIOPITA, NA KUSEMA INAMUIA VIGUMU KUAMINI IMETOKEA KWANI ANASEMA MAREHEMU MNAMO SAA MBILI HIVI ALIMPIGIA SIMU NA KUMWELEZA KUWA AMEPATA AJALI NA KWAMBA WAKATI HUO YUKO KITUO CHA POLISI, BILA SHAKA KUPATA FOMU YA PF 3 YA KUMUWEZESHA KWENDA KUTIBIWA HOSPITALI.

"MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NA GARI....NJOO NIKO POLISI NAANDIKISHA....MWANANGU NAKUFA....ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU.

ANASEMA WAKATI ANAPIGIWA SIMU NA MAMA YAKE YEYE ALIKUWA KATIKA MGAHAWA WA NYUMBANI LOUNGE, NAMANGA, DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA KATIKA KIKAO NA LADY JAY DEE NA MUMEWE GADNA G. HABASH, AMBAO BAADA YA TAARIFA HIYO WALIMSINDIKIZA HADI HOSPITALI YA TUMBI.

"TULIPOFIKA HOSPITALI SIKUAMINI KUONA BADALA YA KUPELEKWA WODINI AMBAKO NILIDHANI MAMA ATAKUWA AMELAZWA NIKAPELEKWA CHUMBA CHA MAITI AMBAKO NILIMKUTA MAMA AKIWA MAREHEMU", ALISEMA PROFESA J KWA MAJONZI.

GLOBU YA JAMII INATOA MKONO WA POLE KWA PROFESA J KWA MSIBA HUU MZITO NA WA KUSIKITISHA. TUNAMWOMBA MOLA AMPE NGUVU YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. 

TUTAENDELEA KUWAPASHA KINACHOJIRI KADRI HABARI  ZAIDI ZITAPOPATIKANA. KWA SASA PROFESA J NA WADAU WENGINE WAKO NYUMBANI KWAKE MBEZI JUU.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Sijui Tanzania tunaishi karne ya ngapi??
    Badala ya kumkimbiza majeruhi hospital anapelekwa polisi kuchukua pf3 !!!!!
    Laiti wangelijua huo muda aliopoteza kwenda polisi ulikuwa wa thamani gani kwa maisha ya marehemu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2013

    sisi watu wa ajabu sana mtu kapata ajali mnamkimbizia Police badala ya hospitali...na hii imeua watu wengi sana hasa ukizingatia police wetu walivyo slow na kulinga kama miungu watu....

    pole sana Prof. Jay....R.I.P Mama

    ReplyDelete
  3. pole sana bro, soma ISAYA 52: 8

    ReplyDelete
  4. Pole sana kamanda, Mola amuweke mahali pema peponi mama.RIP

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 11, 2013

    Pole sana prof. Apumzike kwa amani Aamen

    ReplyDelete
  6. Pole sana Profesa J, pamoja na ndugu na jamaa wote. Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya mama yetu, amina.

    Pamoja na msiba huu, ni jukumu letu sote kuzingatia sheria na taratibu zote za matumizi ya barabara ili kuepuka ajali zinazotuondolea wapendwa wetu. Nawasihi bajaj, boda boda, daladala na wote wanaochomekea na kuvunja sheria waache mara moja.

    ReplyDelete
  7. POLE SANA KAKA. MUNGU AWAPE NGUVU KTK KIPINDI HIKI KIGUMU! TUPO PAMOJA. R.I.P MAMA!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 11, 2013

    Pole sana J, ila kaka michuzi unapaswa kutufikishia ujumbe kwa hao wakuu maana upo nao karibu sana, hii mambo ya kupelekwa police kuomba PF3 na gari imeshakimbia ina maana gani? hivi kama mtu anavujwa na damu nyingi na huduma za police wetu si mnazijua? hivi tukoje? hii ipo kwa wenzetu kweli? tunaomba utufikihie hili kwa wakuu , ikiwezekana pf3 ifiate hospital baada ya mgonjwa kuhudhuriwa na nduguze waelezwe wafuatilie pf3 wakati huo mgonjwa ameshapata matibubu THIS IS SCIK !!! TUNAISHI DUNIA GANI! watu wamelala usingizi mpaka kwenye vichwa ?! ndio maana karume akatuita SAMAKI

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 11, 2013

    Pole mpendwa Mungu akujaze nguvu na imani katika kipindi hiki kigumu, mshukuru na usichoke kumuomba kwani yeye humsikiza kila mja wake.

    RIP Mama yetu mpendwa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 11, 2013

    nimesikitishwa na kifo cha mama huyu.
    kusema ukweli juzi nilikuwa tanzania,hali inatisha kwa ajali ambazo zinazuilika.

    serikali imekaa wapi kuanza kuwa na mpango maalumu wa utoaji leseni na ukaguzi wa magari pia.

    jamani tuige hata wenzetu walio endelea kama wamarekani katika system nzima ya licenses,usalama barabarani pamoja huwezi kuzuia ajali lakni tunaweza kuzuia ajali zisijo na tija.

    Mungu amlaze mahala pema mama yetu.Na nakupa pole sana brother J.
    Mungu akupe nguvu.lakni ndio system hiz tuliochagua na viongozi in-competitive majawabu ndo haya kila siku katika jamii zetu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 11, 2013

    Pole sn Profesa J, Mwenyeezj MUNGU akutie kuvu kipindi hiki cha majonzi, R.I.P mama Profesa J!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 11, 2013

    Huu utaratibu wa PF 3 hauna maana kwa karne ya sasa ya teknolojia na mawasiliano. Inapasa majereuhi yeyote hata akiwa jambazi apelekwe hospitali mara 1 kisha mambo mengine ya,statements, kesi na ushahidi yafuate baadaye. Uhai ni muhimu kwanza kabla ya yote.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 11, 2013

    Urasimu wa sheria zetu utatumaliza,nini umuhimu wa PF3 katika kuokoa maisha ya majeruhi? Pole sana Prof. mama kapumzika ktk bwana. R.I.P mama yetu mpendwa!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 11, 2013

    Pole sana prof J. Kwa kweli hakuna sheria inayonikera kama ya kumpeleka majeruhi wa ajali polisi badala ya hospitali. Imefika wakati sasa sheria hii ibadilishwe au ifutwe kabisa maana imeondoa uhai wa watu wengi ambao wangeweza kunusurika. Tuungane kwa pamoja kuikataa sheria hii.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 11, 2013

    HIYO SHERIA YA KUPELEKA MAJERUHI POLISI KWANZA BADALA YA HOSPITALI IFIKIRIWE UPYA. MUDA HUO ANGEPELEKWA MOJA KWA MOJA HOSPITALI HUENDA ANGEOKOA MAISHA YA HUYO MAMA. HII NDIO BONGO DAKIKA MOJA KWA MGONJWA INA THAMANI KUBWA, HEBU WAULIZENI MADAKTARI WAWAAMBIE. MMHHW!!!***

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 11, 2013

    Im speechless, all i can say is pole na kukuombea

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 11, 2013

    Hakika inasikitisha sana pole sana Profesa J. Mungu atawapa nguvu na kuwainua katika wakati huu mgumu. Imefikia wakati serikali inatakiwa kuingalia upya sheria ya kutoa taarifa kwanza polisi katika majanga kama haya wakati taratibu za matibabu zingezingatiwa kwanza kuokoa maisha ya wengi na taratibu nyingine zifuate. Ni dhahiri kwamba hata nchi zilizoendelea taratibu hizi zipo na zinafuatwa lakini hatujafikia huko kwani wenzetu baada ya tukio huduma zote za muhimu na lazima zinakuwa tayari zimefika kwenye. Ambulance, police na huduma za moto zinafika kwa wakati mmoja na kuokoa maisha ya waliopatwa na janga. Tuamke!




    Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 11, 2013

    Hili suala la PF3 linahitaji kubadilishwa ilikuokoa maisha ya wahanga wa ajali. Ebu tuone wenzetu walioendelea wanafanyeje suala la polisi ili kundokana na huu mfumo unao ua watu. Na hili limefikia pahala watu wanamkimbia aliyegongwa ili kuondokana na jukumu la kuenda polisi kutoa maelezo ambayo wakati mwingine hayajui. Kwa mfano mtu amegongwa na aliyegonga amekimbia watu wanaanza kuogopa kufanya usamaria kwakuogopa suala la kwenda polisi, na polisi wakipigiwa huchukua muda mrefu kufika mahali pa tukio kwa sababu za uzembe, kutojali pamoja na ugumu wa kufikika kwa wakati mahali pa tukio. Hivyo, wahanga wengi wanakufa kwa hilo. Mabadiliko nimuhimu kufanya yanapohitajika kuboresha maisha ya wananchi. Polisi jukumu lao ni pamoja na kulinda usalama wa raia na usalama manake watu wasife, kwanini wasilione hili kama linauwa watu wake.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 11, 2013

    Wadau hapo juu nawaunga mkono kwa kweli haya mambo ya kupitia polisi ni mitahni hasa ya maisha, ila kama ni ajali bila form ya PF3 nadhani hospitali hawatampokea kumtibia unless ni private hosp. hizi hosp. zetu za serikali mambo yake ndio hayoooo! Nawapa pole sana familia ya marehemu kuondokewa na mama yao.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 11, 2013

    Poleni sana familia ya Haule.Jamani wabunge tunaomba msiangalie tu kodi ya sim card. Maisha yetu na usalama ni wa muhimu zaidi, Mkifika bungeni kazi ni kutukanana" siongei na mbwa naongea sijui na nani" wakati mambo ya msingi kama haya hayawahusu.Alafu tunabaki oooh kazi ya Mungu,hivi unadhani Mungu katutofautisha na viumbe wengine kwanini? Sasa unapewa akili huitumii, Mungu akusaidieje tena?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 11, 2013

    Pole sana Profesa J,familia, ndugu, marafiki na wote wanaoguswa na msiba huu. Mungu awapiganie katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 11, 2013

    Poleni sana familia ya marehemu. Inasikitisha sana mim nimepoteza marafiki,ndugu wengi kwenye ajali za gari. Kama wanavyosema wadau hapo juu kwakweli mfumo wote wa kuhudumia wagonjwa wa ajali urekebishwe. Mgonjwa anapshwa kuhudumiwa haraka ipasavyo. Dakika 10 ukipoteza zaua mtu.
    Badala ya kujenga majumba kama hekalu,majumba ya starehe kwanini tusiinvest na huduma ya Kwanza? 1) Ambulance 2) Wahudumu 3) Vifaa 4)Communication system - hospitali,polisi waweze kutaarifiwa moja kwa moja ajali ukitokea ili huduma ziharakishwe. 5) Usalama barabarani- traffic lights,leseni,cross walks,speed limit,kunasa walevi n.k

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 11, 2013

    Pole sana Prof J na familia yote!

    Tanzania ni nchi ya ajabu sana japo ni nchi yangu. Suala la PF 3 ni ujinga mkubwa sana kutumika ktk nchi maana ni kinyume na katiba na haki za binadamu ambapo majeruhi yoyote hata kama anahisiwa ni jambaz sugu anatakiwa kupatiwa matibabu ya haraka bila ujinga wa hiyo PF3. Afterall utasemaje mtu huyu ni jambazi wakati mahakama haijamhukumu??

    Nina uhakika si mapenzi ya Mungu huyu mama atutoke sasa hv..tuache kumsingizia Mungu kwa makosa yetu kama ya kupoteza muda kwenye PF3..pia kwa maelezo hata hiyo hospital ya Tumbi aliyopelekwa huduma zao kwa majeruhi wanaohitaj immediate care (maybe anayevuja damu ndani ya mwili) ni sifuri..maana kama wangekuwa na ICU yenye vifaa hakika wangemuokoa uhai wake.!

    Mambo kama haya na mengineyo ndio yanayotufanya wengine tusifikirie kurudi tz sababu ya uzembe, ujinga uliokithiri..nimekasirika sana ankal..pole tena wafiwa!

    mdau
    J4
    Ujeruman

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 11, 2013

    Pole sana Prof na msiba huu ila fahamu kazi ya Mungu haina makosa. '' Hakika sisi wote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea''. Nilisikia tena ktk TV kuwa polisi wamebadilisha utaratibu huu hivyo ukipata ajali unakwenda hospitali na hiyo PF3 inafuata baadae, hii inanichanganya kidogo.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 11, 2013

    Mpaka lini huu mtindo wa kupeleka wagonjwa polisi utakoma? why taking people's life for granted? hakuna CPR, wala hakuna blood arrest, hakuna chochote, hakuna ambulance kukimbiza wagonjwa hospitalini. barabara zipo finyu kupita kazi, mpaka lini serikali yetu haitajali maisha ya watu wake?

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 11, 2013

    Kweli kumbe ukipata ajali unaenda polisi?????????? Nani alimpeleka polisi badal aya hospitali????? Anyway imeshatokea lakini kuna cha kujifunza hapa! Yaani sheria za bongo walahi!!!! Yarabi tupe nusura! Yaani uhai wa mtu sio kitu ila rushwa na ubadhilifu!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 11, 2013

    pole sana bro. yote hayo Allah ameshaandika...

    ReplyDelete
  28. Pole sana Kaka. Mungu akutangulie na akupe faraja ya roho katika wakati huu mgumu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amen.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 12, 2013

    PF3???? Huu ndo upuuzi gani? watu wangapi watakufa kwa kucheleweshwa na hii PF3??? Kwanini hao police wasifungue ofici zao hapo hospitali??? vitu vya haraka kama hivi kweli visifanyike, watu wasitibiwe kisa nini PF3. Kwanini suala la kuokoa maisha kwetu sisi hatulipi kipaumbele?? Kila kitu tunamsingizia mungu!! aaahhh mungu kampenda zaidi!!! huu ni uzembe,mungu anatupenda zaidi tukiwa hai siyo tukiwa tumekufa. serikali inabidi ibadilishe huu upuuzi wa kuwazuia watu kutibiwa kisa PF3. kama ni suala la usalama inabidi mlipitie upya kwani limepitwa na wakati. kazi ynu kama serikali ni kulinda watu hili suala la pf3 linaua watu. Pro J pole sana nina hakika heshima uliyonayo kwenye jamii unaweza kuhakikisha hakuna mtu atakae kufa tena kwavile ilibidi akachukue PF3 kwanza then ndo atibiwe. unaweza fanikisha hilo kwa kuanzisha kampeni dhiidi ya PF3. MATIBABU KWANZA THEN PF3. IF U DO THAT YOUR MOTHER WILL NEVER DIE FOR NOTHING.

    BINAADAMU AKIPATA AJALI AU DHARURA YOYOTE YA UGONJWA, APELEKWE HOSPITALI KWANZA THEN POLICE. HATA KAMA MTU NI MUHALIFU ANAYO HAKI YA KIMSINGI YA KUTIBIWA. WATU WA HAKI ZA BINAADAMU AMKENI, WATANZANIA WATAKUFA KWA NJIA HII MPAKA LINI????

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 12, 2013

    KUHUSU KUGONGWA KWA MAMA YAKE J, NIDHAHIRI KWAMBA KIFO CHAKE KIMESABABISHWA NA YEYE KUCHELEWESHWA POLICE. KUNA CHANCE KUBWA KWAMBA ANGEKUWA HAI LEO HII KAMA ANGEPELEKWA HOSPITALI KWANZA THEN POLICE

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 12, 2013

    MICHUZI KICHWA CHA HABARI HII KILITAKIWA KIWE 'MAMA WA PRO J AFARIKI BAADA YA KUCHELEWESHWA POLICI'
    MTU AKIGONGWA NA GARI NI LAZIMA ATAKUWA ANA TOKA DAMU NJE YA MWILI AU NDANI KWA NDANI(INTERNAL BLEEDING)
    BADALA YA KUWAHISHWA KWA DAKTARI ANAPELEKWA POLICE!!!!!!???? R U SERIOUS RIGHT NOW?

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 12, 2013

    System Ya PF3 ni ya AJABU sana, Hivi why kusiwe na hizo Fomu pale Hospital na kunakuwa na Polisi ana handle hizo kitu pale. Serious tunapoteza sana watu kwa hii System. Kwani mtu akipewa matibabu alafu PF3 ikafuata kuna shida gani. Pole sana Pro Jay, Tupo pamoja sana kaka. Mungu akutie Nguvu.

    Ndimi,
    Choka Babu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...